Usimchukie baba yako hujui sababu gani ilipelekea akaachana na mama yako

Usimchukie baba yako hujui sababu gani ilipelekea akaachana na mama yako

Mr George Francis

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2022
Posts
278
Reaction score
512
USIMCHUKIE BABA YAKO HUJUI SABABU GANI ILIPELEKEA AKAACHANA NA MAMA YAKO.

Chukua hizi busara zitunze kwenye moyo wako na uzitumie, zitaweza kukusaidia katika safari yako ya maisha.

Ni kawaida sana kuona watoto wengi waliolelewa na mama au ndugu wa upande wa mama kukosa mapenzi kwa baba zao.

Wengi wamekuwa wakiwachukia na kuwalaumu sana baba zao bila kujua ukweli halisi wa nini kilitokea hadi kuachana kwao.

Mambo mengi watoto hawa wanayoambiwa na mama zao kuhusu baba zao huwa sio ya kweli na yenye ukweli yanaongezwa chumvi.

Mama hawezi kumweleza mtoto kuhusu makosa yake yaliyomuudhi mwanaume hadi kufikia hatua ya kuachana kwao.

Mtoto anakuwa anaamini kuwa baba yeke ni mtu mbaya na shetani la kuzimu, haistahili heshima wala upendo wake hata kidogo.

Inafika wakati baba anahitaji kumlea mtoto lakini inashindikana kwasababu teyari mtoto huyo ana chuki ya ndani dhidi ya baba yake na hataki hata kumuona wala kumsikia.

Maranyingi huwa kuna mambo mengi ambayo watoto hatujui na hatutokaa tujue kwasababu mama zetu wanaamua kufa na siri zao.

Lakini pia hata kama ikitokea baba kweli alikuwa na makosa lakini sio sawa kuhamishia chuki hiyo kwa mtoto/watoto.

Ni wazazi ndio mliogombana au kuachana hivyo kama mtachukiana chukianeni wenyewe lakini sio kuhamisha ugomvi wenu kwa watoto.

Na sisi watoto tusimchukie baba wala tusimchukie mama. Kitendo cha kutoa mbegu na sisi kuzaliwa inatosha kuwapa heshima yao. Bila mama bila baba tusingezaliwa hapa duniani.

Msikilize baba yako, mpende baba yako, mthamini na muheshimu sana baba yako.

Kama alikosea na sasa yupo tayari kurekebisha na muishi vizuri, kubali kumsamehe. Kubali maisha mapya ya furaha na amani kati yenu.

Usiruhusu chuki hiyo ikufanye wewe uwe baba au mama mbaya kwa watoto wako hapo baadaye.

Tengeneza amani na vunja mzunguko wa chuki na visasi. Msamaha ni baraka.

Muheshimu baba yako, muheshimu mama yako utaishi miaka mingi na yenye heri hapa duniani.

Kama umeingia kwenye mkumbo wa kumchukia baba yako au mama yako tangaza msamaha leo na tengeneza upendo kati yenu.

Na wewe mzazi uliyetengeneza chuki kati ya mtoto na baba yake, rejesha umani na ivunje chuki hiyo haraka iwezekanavyo.

Mjengee mtoto hali ya kumpenda na kumueshimu baba yake. Mpe maneno mazuri na mjengee ile hofu ya mungu itakayomfanya awe na upendo kwa baba yake na upendo kwa kila mtu.

MUNGU akubariki sana. 🙏🙏🙏

#No_learnig_No_earning
So We Have To Learn.

Content By George Francis

 
Baba ukishiriki malezi ya mtoto kikamilifu ukajenga uhusiano na mwanao ,hata aambiwe nini hawezi kukuchukis
Sasa mtoto hakuoni wala kukusikia ataachaje kuamini anayoambiwa na anayemuona kila siku!
 
Baba ukishiriki malezi ya mtoto kikamilifu ukajenga uhusiano na mwanao ,hata aambiwe nini hawezi kukuchukis
Sasa mtoto hakuoni wala kukusikia ataachaje kuamini anayoambiwa na anayemuona kila siku!
Kuna wanawake mkishaachana hataki hata kukuweka karibu na mtoto hasa kama akiwa na uwezo kidogo anaamini anaweza kulea mwenyewe.
 
Huna unalojua we kiongozi Kuna wababa washenzi sana unakuta ana maisha mazuri katelekeza watoto wake wa damu na analea watoto wa kambo wa mke wake na wanaishi life zuri
 
Mwanaume mwanaume mwanaume M-ngu mwenyew mwanaume anajua tunachukiwa na wenetu kisa mama zao
 
Back
Top Bottom