Usingizi wa kwa watoto wadogo

Usingizi wa kwa watoto wadogo

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
28,203
Reaction score
37,906
Habari wana Jamii!

Kwa kawaida watoto wadogo ni wepesi wa kupata usingizi baada ya matukio fulani mf. baada ya kunywa uji, wengine hupata usingizi baada kulia, wengine baada ya kubebwa tu, n.k.

Nimekuwa nikijionea njia za kushangaza ambazo huwapatia watoto usingizi, mf:

  1. Mwanangu hupata usingizi haraka sana, kama utampa taulo! Kuna kitaulo chake hapa nyumbani, huwa akipewa tu, anaanza kukinyonya, na hamalizi dk 10, analala!
  2. Rafiki yangu mmoja, kanambia Mwanae analala wakati wowote anapoona mtu, hata mtu mzima anasinzia, na yeye hupata usingizi!
  3. Kuna mwingine amenambia mwanae hupata usingizi kwa urahisi sana kama atahisi harufu ya mafuta ya gari, iwe ni kwenye dala dala ama hata gari binafsi!

MwanaJamii naomba tujulishhane vitu mbali mbali vinavyowapelekea watoto kupata usingizi haraka sana.
 
Kuna katoto ka dadangu hapa nyumbani huwa kanalia sana kakishikwa na mtu yeyote ila mie nikimshika tu ananyamaza, anatulia na kulala.
Sijui ni kwa nini hutokea hivyo!
 
Halafu pia!
Nakumbuka zamani kidogo mtoto wa shangazi yeye alikuwa analia sana akilala chumba cha mama yake na hapati usingizi kabisa ila akiwekwa sebuleni au kakilala chumba kingine kanalala usingizi fofofo na wala husikii kakilia lia!
Watoto wana viroja sana kwa kweli!!
 
Kuna mmoja wa jirani yetu yeye anakaa macho wazi mpaka awe na uhakika baba na mama yake wamepitiwa na usingizi, otherwise anataka kuona kinachoendelea.
 
Kuna katoto ka dadangu hapa nyumbani huwa kanalia sana kakishikwa na mtu yeyote ila mie nikimshika tu ananyamaza, anatulia na kulala.
Sijui ni kwa nini hutokea hivyo!

mnashare similar star Chitemo
 
Last edited by a moderator:
Kuna mmoja wa jirani yetu yeye anakaa macho wazi mpaka awe na uhakika baba na mama yake wamepitiwa na usingizi, otherwise anataka kuona kinachoendelea.

kaka tunamalizia swaumu, nimecheka sana mkuu Salamander
 
Last edited by a moderator:
Kuna mmoja wa jirani yetu yeye anakaa macho wazi mpaka awe na uhakika baba na mama yake wamepitiwa na usingizi, otherwise anataka kuona kinachoendelea.

mmmmh!!
kana umri gani hako katoto?
 
jamani mwanangu akitaka kulala nyumba nzima wanajua anataka kulala
analia jamani mpaka kero
 
mie kwa kwangu kanalala mchana usiku hakalali kabisa.
 
mie kwa kwangu kanalala mchana usiku hakalali kabisa.

Ndio hiyo hiyo mchana Evz, usingizi wake unasababishwa na kitu gani?
 
Last edited by a moderator:
mi wangu akitaka kulala lazima alie kwanza. saa 11 alfajiri anaamka naanza kupigwa mateke kaamka sasa hivi yupo nje anamsumbua mamake huko. aaargh mungu amjalie afya njema akue kimo na akili
 
mtoto akitoka kula na ukimwogesha usingiz hauchukui raundi pia kulia ni njia moja wapo.ya kuutafuta usingiz akilia wew mpe nyonyo tu anaanza kusinzia taratiiiibu
 
Back
Top Bottom