Usiniadhibu kwa kukupenda

Usiniadhibu kwa kukupenda

Wewe ni single mother imetokea nimekupenda.

Nakuta mwanao wa kiume hana nidhamu na hajalelewa kiume amelegea na mideko mingi, nakusaidia kumlea kwa kukupa ushauri. Unaniambia siwezi kujua mtoto analelewaje.

Haya unaniambia nikope pesa ili ufanye biashara uongeze mtaji nakwambia subiri mwaka wa bajeti uanze. Unasema sijakupa thamani ndio maana sioni sababu ya kukusaidia.

Unaamua kuninunia na kuniambia nijitathmini kama nakuhitaji nifanye mambo hayo ili uamini. Umeamua kuniadhibu kisa nimekupenda? Sawa, namimi natafuta njia mbadala ila utaja kumbuka.
Move on, tafuta option ingine
 
Punguza kua Mr NICE MAN,

Weka misimamo yako clear na yeye ajue,

Ukiendelea kulia Lia hivi uyo Mwanamke atakusumbua sana, na utajuta
 
Kila siku humu mnashauriwa single mamaz achaneni nao watu hamsikii.
 
Wewe ni single mother imetokea nimekupenda.

Nakuta mwanao wa kiume hana nidhamu na hajalelewa kiume amelegea na mideko mingi, nakusaidia kumlea kwa kukupa ushauri. Unaniambia siwezi kujua mtoto analelewaje.

Haya unaniambia nikope pesa ili ufanye biashara uongeze mtaji nakwambia subiri mwaka wa bajeti uanze. Unasema sijakupa thamani ndio maana sioni sababu ya kukusaidia.

Unaamua kuninunia na kuniambia nijitathmini kama nakuhitaji nifanye mambo hayo ili uamini. Umeamua kuniadhibu kisa nimekupenda? Sawa, namimi natafuta njia mbadala ila utaja kumbuka.
Kila siku tunaongea humu ndani jmn! Achaneni na mambo ya masingle maza. Watajisort wenyewe. Mbona hamtuelewi? Haya ina sasa.
 
Unaweza kumkumbuka mtu kwa upendo wake wa kweli

Upo wakati baada ya kupitia heart breaks za kutosha unajitathimini mahusiano uliyopitia na kukumbuka yule mmoja ambaye deep down unajua alikupenda kweli...ndio kukumbuka kwenyewe huko

Sio lazima iwe kodi ama kujengea nyumba
Umejibu vema. Mimi kuna mmoja hadi kesho anatamani nirejee lakini nilishamwambia imekwisha. Nilimpa thamani ambayo kabla sikuwahi kumpa mwanamke yeyote kimapenzi, akaniona lofa. Akawa anamleta bwanake nyumbani kwao (tulikuwa majirani) nikiwepo. Alifanya hivyo kama mwaka mzima mpaka nikapoteza uwezo wa kufikiri sababu niliamini siwezi kuishi bila yeye.

Nilimuaga naondoka akajibu tu "sawa" nikaondoka. Bado mbali naye nilikuwa nampigia simu, ila one day akaniambia "ùsinipigie simu wala sms, naolewa na mdogo wako kwahiyo kwasasa wewe ni shemeji yangu." Nikajaribu kufikiria huo ushemeji unatoka wapi na sina mdogo wangu anayeoa huko. Ile sms hadi leo ndio silaha yangu, akijifanya kunitafuta namkumbusha kwamba siwezi kuchangia mwanamke na mdogo wangu.

Alifanya vile kwasababu alijua muda wowote nitamtafuta na sifurukuti. Kama kawaida alitegemea meseji kama "kwanini unanitesa, nimekukosea nini, naomba usifanye hivyo" n.k

Akaona kimya day 1,2,3 akajua utani akapiga nikakata. Akatuma sms sikujibu. Ikawa imeisha na sijawahi kuwa na hisia naye tena tangu hapo
 
Hahaha nimecheka huku nahuzunika kwa hii comment yako...pole sana to yeye

Nimeelewa hoja yako kulingana na uliyopitia
Binafsi hadi sasa namshukuru Mungu wanaume bado hawajanifanyia jambo baya kiasi cha kuwa na chuki nao ya kudumu
Sikujui, hunijui. Lakini i swear ningekuwa single ningekutafuta kwa namna yoyote ile. Huwa una comments fupi lakini zenye kujenga%kutafakarisha.
 
Hao ndio wanao ongozwa Kwa kukumbukwa now days Sasa ,

Wewe peleka peleka mazawadi Yako then uwe kimoja Chali uone jinsi Dunia ya mapenzi itakavyo kunyoosha , [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Nimejionea Kwa macho yangu sio mara 1 Wala mara 2
Wanawake wakiwalilia wasimamia ukucha baada ya kuachana nao
Kwa mwanamke yuko radhi atafute mwanaume mwenye helaa ila sio kumuacha anayemkojozaa
 
Unaweza kumkumbuka mtu kwa upendo wake wa kweli

Upo wakati baada ya kupitia heart breaks za kutosha unajitathimini mahusiano uliyopitia na kukumbuka yule mmoja ambaye deep down unajua alikupenda kweli...ndio kukumbuka kwenyewe huko

Sio lazima iwe kodi ama kujengea nyumba
Achana na huyu @to yeye ...huyu akili zake kuna uwezekano zilishahama sio yeye tena.Materialist
 
Back
Top Bottom