Usiogope kujilipua kwenye kutafuta maisha, hakuna njia rahisi

Usiogope kujilipua kwenye kutafuta maisha, hakuna njia rahisi

Mpwayungu Village

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
14,540
Reaction score
30,875
Huenda nikawa tofauti kimtazamo na wengine lakini kama kijana inabidi uwe mbunifu na risk taker. Usijali kuhusu hasara siku zote biashara ngumu zenye hasara kubwa ndobiashara zenye mafanikio. Ukipata fursa ya kwenda kutafuta maisha ughaibuni hata kama nikwakuvuka bahari kwa kutumia mashuwa vuka nenda katafute maisha.

Usiogope kufa kwenye kusaka life mtu wangu, jirisk jirushe tafuta pesa no way zaidi ya kuhangaika kwa udi na uvumba. Ndio mana wenzetu Wasomali wakiwa ugenini wanatoboa chapu kwasababu wanajua walifika huko kwa ku-risk maisha yao walipanda kwenye makontena ya matipa kwa umbali wa kilometer zaidi ya 5000.

Waarabu nenda huko Marekani, Italy na Uingereza wametoboa kwakuwa kuvuka kwao bahari kulijawa na dhoruba na harufu ya umauti maana kuingia kwao tu sio documentary wala legally wameingia kimagumashi na wametoboa. Kama utakufa kwenye utafutaji utakuwa umekufa kikamanda maana hiyo ni Trial and Error.

1660632667980.jpg
images%20-%202022-08-16T094853.417.jpg
images%20-%202022-08-16T094951.394.jpg
 
Kibongo bongo wachache wanaeza kujilipua huku tunaanza ku calculate risk sana ooooh polisi wakinibamba nafia jela sasa unaogopa kufia jela unafia geto kama inzi kwenye glass ya bia.
Kwanini ujilipue wakati fursa zimejaa tere hapa Tz.

vijana wengi wanao ende nje bila proper documentation, wengi wana shindwa kutoboa 80% wana kufa mapema wanafungwa jela au kujiunga kwenye magenge ya wahalifu, kwanini urisk maisha wakati "we live once"
njoo Johannesburg uoni jinsi wa bongo wa Somalia wa Nigeria wanavo taabika, wengi wanatamani kurudi nyumbani ila hawana documents na pesa.
 
Watu wengi tunafikiri kwamba pesa itatupa furaha na amani ya moyoni lakini ukweli NI kwamba ukishazipata hizo pesa halafu ukafikisha miaka ya uzeeni matazimio yote Yale yanapotea unaanza kuwaza kitu kingine kabisa isitose pesa hazishibiki huwezi kuridhika, afadhali uwe na Mali kidogo ila imani kwa mwenyeziMungu ndio iwe kubwa. Pesa zipo ardhini tunazikanyaga ardhi ardhi ardhi imebeba utajiri hakuna haja ya kufanya uhalifu au kuvuka bahari na vyombo visivyo na standard.
 
Hela inaleta peace of mind mkuu

Ukishafuata ushauri wa Ndege John fahamu kufanikiwa kwako itakua ngumu sana, siku moja nilisema vijana bongo hawajitumi ndio maneno kama hayo sasa, wasomali, waethiopia , wa nigeria wanapambana dunia nzima hata wakenya tu na warundi wanajitupa hadi mayotte wanauza matunda na wanatoboa kabisa
 
Ukishafuata ushauri wa Ndege John fahamu kufanikiwa kwako itakua ngumu sana, siku moja nilisema vijana bongo hawajitumi ndio maneno kama hayo sasa, wasomali, waethiopia , wa nigeria wanapambana dunia nzima hata wakenya tu na warundi wanajitupa hadi mayotte wanauza matunda na wanatoboa kabisa
Mkuu kufanikiwa una maana gani kumiliki vitu gani ndio kufanikiwa..Mimi nazungumzia habari za kuridhikiwa.yaani napinga hoja ya kwamba urisk mpaka maisha yako kwa ajili ya pesa TU...haifai kupambana sawa tupambane sijakataa ila sio kwa kiwango Cha kuvuka mipaka ya uhai.
 
Mkuu kufanikiwa una maana gani kumiliki vitu gani ndio kufanikiwa..Mimi nazungumzia habari za kuridhikiwa.yaani napinga hoja ya kwamba urisk mpaka maisha yako kwa ajili ya pesa TU...haifai kupambana sawa tupambane sijakataa ila sio kwa kiwango Cha kuvuka mipaka ya uhai.
Sawa mwenzetu utaishi milele
 
Hela inaleta peace of mind mkuu
Uko sahihi chief dunia ya leo mafanikio ya mtu yanapimwa kwa wingi wa pesa na Mali hata Mimi naona tofauti nikiwa na kibunda na nikiwa nimefulia..kweli pesa ndo uhai ndo maisha ila napingana na mbinu ya kufanya uhalifu maana Mara zote uhalifu means unamnyima mwingine haki unamfanyia ukatili huo ujeuri na ukaidi Mimi siuwezi.
 
Watu wengi tunafikiri kwamba pesa itatupa furaha na amani ya moyoni lakini ukweli NI kwamba ukishazipata hizo pesa halafu ukafikisha miaka ya uzeeni matazimio yote Yale yanapotea unaanza kuwaza kitu kingine kabisa isitose pesa hazishibiki huwezi kuridhika..afadhali uwe na Mali kidogo ila imani kwa mwenyeziMungu ndio iwe kubwa....pesa zipo ardhini tunazikanyaga ardhi ardhi ardhi imebeba utajiri hakuna haja ya kufanya uhalifu au kuvuka bahari na vyombo visivyo na standard...
Acha kutengeneza visababu mkuu!
 
Back
Top Bottom