Usiogope kujilipua kwenye kutafuta maisha, hakuna njia rahisi

get rich or die trying bro
 
Kibongo bongo wachache wanaeza kujilipua huku tunaanza ku calculate risk sana ooooh polisi wakinibamba nafia jela sasa unaogopa kufia jela unafia geto kama inzi kwenye glass ya bia.
Mtu ana risk kutafuta Nini? ilihali yupo comfortable na maisha yake anapata basic needs zote on time muda mwingine kuridhika sio ujinga.
 
Ushauri mzuri ila mtu asijiingize kwenye vitendo viovu, apambane katika vitu visivyo vunja sheria na kumkosea Mungu.
Kweli mkuu
Kama mtu unataka kujilipua nenda hata migodini huko kasake Madini ila sio kufanya uhalifu wa kuumiza wengine...
2 timotheo 3:1-5 ilitabiri Jinsi Zama hizi za wenye kupenda pesa kuliko Mungu zitakavyokuwa so ni unabii unatimizwa
 
Miaka ya gizani huko kabla hawajafanya pesa kua mfumo kuu wa biashara, barter trade ndo ilikua kila kitu so utajiri ilikua ni ardhi, madini, wanyama..miaka ya mbele utajiri itakua ni roho yako mkononi pesa inaenda kupotea, itakuja crpto nayo itapotea yaanze maswala ya popuation control.

Yote kwa yote ushauri wa mkuu una apply kwa bachelor tena umri kiaka 30 kushuka mana ukiwa na tegemezi automatically akili zinakukaa.. 30s kwenda mbele ni mwendo wa kucheza kwa step ukijilipua unalipuka kweli 💣
 
Sioni hata sababu ya kujilipua. Wela malengo yako sawa na kuwa na imnai kuwa Mungu atakuvusha kufikia malengo yako. Na usijiwekee muda Mungu ikifika wakati wake atatenda.

Tukubali tu kwamba pesa anayohotaji mtu ni ile ya kukuwezesha kununua kitu chochote unachohitaji kwa wakati wowote (Mavazi, elimu, makazi, afya, usafiri nk). Ndio maana kusaka pesa ni muhimu kuliko kitu kingine hapa duniani.

Na wewe ukishafanikiwa usisahau kumshukuru Mungu kwa kuwasaidia wenzako!!!
 
Kila kitu ni risk, ukiwa unatembea ni risk unaweza pata ajali, ukisafiri ni risk, mwanamke kwenda kujifungua ni risk, ukiwa unaendesha gari ni risk... Kila kitu ni risk katika maisha hata chakula tunachokula chaweza kuwa sumu mwilini, wangapi wamelazwa kwa ulaji usio sahihi?

Maisha yetu tumezungukwa na risks kila siku, ukienda mizungukoni ukirudi salama nyumbani ni jambo la kumshukuru Mungu...

Haina haja ya kuogopa ku risk either katika biashara au utafutaji lakini si kwa uhalifu.
 
Bonge la Uzi....Vijana inabidi tuwe na fikra za namna hii.

Mleta mada hajasema watu waibe au wafanye uharifu, amesema tafuta hela kwa udi na uvumba na usiogope ku-take risk.

Kuvuka border, kuvuka maji au kuzamia pits za migodini sio uharifu...huo ni ushujaa wazee.

Uharifu ni kuiba mali za umma ukiwa kiongozi, matumizi mabaya ya madaraka, tozo za ajabu ajabu, kuiba kura nk.

Vijana tukaze pamoja na changamoto nyingi lakini as long as tunapumua, tuna nafasi ya kutoboa....watu wanasema miaka 40 ni ya kuanza bata, utafutaji na muda wa kutoboa hatulingani mazee...Mi ntatafuta hadi siku nakata pumzi...maana wapo waliotoboa na miaka 40, 50, 60 mpaka 90 huko.

Vijana wanaogopa kuacha familia na kwenda hata mikoa ya mbali kutafuta hela. Sio lazima kwenda mbali ila pale inapobidi usisite kuliamsha.

Heshima kwa vijana wote tunao-hustle daily na tunaamini tutatoboa..Mwenyezi Mungu atusimamie.
 
*Kati ya kipindi cha uzee na ujana ni kipi hukuchukua muda mrefu wa mtu kukiishi?
* Kipindi kipi kati ya ujana na uzee huhitaji pesa sana?
 
*Kati ya kipindi cha uzee na ujana ni kipi hukuchukua muda mrefu wa mtu kukiishi?
* Kipindi kipi kati ya ujana na uzee huhitaji pesa sana?
Ujana NI miaka mingi na ujanani ndipo pesa inatumika Sana...ila sisemei uzee Sana hapana hata Kama miaka 40 pekee unaweza kuanza kujuta kwa uliyoyafanya kisa TU kutafuta pesa kwa njia mbovu.
 
Kuna mtu kataja uhalifu hapo
 
Tena miaka 30 kama bado muogamuoga nitashangaa sana unless uwe umetoboa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…