Usiombe kuacha kazi kisa Forex. Nilivyofilisika na kukimbilia kijijini Tabora

Nilipochukua simu yangu na kufungua programu yangu ya MT5, niliona chati zinazozidi kupanda kwa rangi ya bluu, na hiyo ndiyo ilikuwa ishara ya kwamba biashara yangu ilikuwa ikipata faida kubwa.

Wakati huo, hisia za furaha na kuchanganyikiwa zilipigana ndani yangu. Furaha ya ghafla ya kugundua kwamba nilikuwa nimepata faida kubwa ilinifurahisha. Nilifurahi sana kiasi kwamba nilihisi kama ninapaa angani. Hii ilikuwa ni matokeo ya kazi nyepesi ya kubonyez kutufe cha Buy XAUUSD na kujikuta nimesahau, ila faida hiyo ilionekana kama zawadi ya ghafla kutoka kwenye soko la forex.

Hata hivyo, kwa upande mwingine, kuchanganyikiwa na wasiwasi vilianza kuniingia. Nilikuwa na hamu ya kufunga trade na kuchukua faida yangu haraka iwezekanavyo kabla ya soko kubadilika mwelekeo. Hali hii ilinifanya kuhisi kama ninacheza na nyakati.

Kwa sekunde zilizosalia, nilifanya uamuzi. Nilichukua hatua na kufunga biashara yangu. Niliona jumla ya faida iliyokuwa imeandikwa kwenye simi yangu ilikuwa 40k tena kwa mtaji mdogo tu nilioweka na kwa muda mfupi, na hilo ndilo lililozidi kuleta furaha yangu. Lakini kwa moyo ulivyokuwa unapiga kwa kasi Hivyo, nilivuta pumzi ya kuridhika na kuchukua muda wa kuadhimisha mafanikio yangu.

Baada ya kufurahia mafanikio yangu ya ghafla kwenye soko la forex, nilijikuta nikiwa na hisia za kujiamini na uhuru. Nilipofunga faida yangu, wazo lililonijia kichwani ni kula bata, nilienda kuonana na yule bidada pale chuo cha wasibu kisha nikamchukua, sikumwambia chochote kuhusu trade ila kupitia furaha yangu na tabasamu usoni alijua.
Mimi ni mgeni kidogo jiji la Arusha yeye akawa ananipa location, hapa Club D, kule Triple A, kipindi hicho kokoriko pale Arusha ilikuwa inavuma hatari, tulimaliziaa hapo.

Kiukweli Mimi na bata ni kama kachumbari na pilipili! Inavyounda msisimko wa kipekee na uchangamfu usio na kifani.

Kwahiyo Sikuishia hapo hela iliyokuwepo kwenye account ni nyingi sana, kiasi nilichanganyikiwa, niliamua kujipa raha na kufurahia matunda ya kazi yangu. Rasmi Niliamua kuanza safari ya kuvuna raha na starehe kutoka Arusha, jiji la utalii lenye mandhari ya kuvutia, hadi jiji la Dar es Salaam, moyo wa biashara na burudani nchini Tanzania.

Kwa Arusha, nilijipatia fursa ya kufurahia hewa safi ya milima ya Kilimanjaro, pia nilienda kuona mandhari ya ajabu ya mbuga za wanyama za Serengeti. Nilitembelea vivutio vya utamaduni na historia ya eneo hilo, nikijifunza mengi kuhusu utajiri wa utamaduni wetu wa Tanzania. Pia, nilijipa raha kwa kula chakula cha asili cha kimasai roshoroo na kushiriki katika tamasha za kitamaduni pale Masai camp Arusha.

( nilibadilisha apartment na kuhamia Ngurudoto, hii wengi mnaijua, na gharama zake)

Siku chache nikageuza Jijini Dar Es Salaam, Nikiwa bado na hisia za kufurahia mafanikio yangu, niliendelea na safari yangu ya kura raha jiji la Dar es Salaam. Jiji hili lenye shughuli nyingi lilikuwa ni mahali pazuri pa kufurahia starehe za kisasa na maisha ya jiji. Nilipata fursa ya kufurahia vyakula bora katika migahawa mashuhuri kama samakisamaki, kushiriki katika burudani za muziki wa live, Mlimani City ndo ilikuwa kijiwe changu cha kunywa kahawa, na mda ya jionijioni kujifurahisha na marafiki katika vilabu vya usiku(Hapa mpaka nikapewa jina la "Buda wa Raha."), jinsi nilivyokuwa naleta furaha kwa watu wanaonizunguka, hapa najua namanisha nini.

Nilifanya ziara za kuvutia katika maeneo maarufu ya jiji kama vile Coco Beach, Mikocheni, na Masaki. Nilijaribu mambo mapya kama vile kusafiri kwa boti hadi visiwa vya Zanzibar na kufurahia jua la bahari la Tanzania. Kwa kifupi, nilijinyakulia kila fursa ya kufurahia maisha, kutoa shukrani kwa mafanikio yangu ya ghafla kwenye biashara ya forex.

Safari hii ya starehe ilikuwa ni zawadi ya kujitolea kwa bidii yangu na jitihada zangu katika biashara ya forex. Nilijifunza kufurahia matunda ya kuacha kazi ngumu na kujiunga na forex, mafanikio hayo yalikuwa kama njia ya kujipa motisha na kuendelea kufanikiwa katika safari yangu ya kifedha. Kila kicheko na furaha nilichopata kilikuwa kama ishara ya kwamba safari yangu ya forex inasonga vizuri.

Yote haya yalikuwa ni sehemu ya safari yangu, na hii ilikuwa tu hatua moja kuelekea kwenye ndoto zangu za mafanikio katika ulimwengu wa forex.

( kweli palipo na mafanikio Makubwa uondoa wasiwasi kabisa, na ukikaa vibaya unajisahau na kuanguka anguko kuu)


(Sehemu inayofuata itaendelea...)
 
😊😊☺️☺️🀣🀣🀣🀣 mnaongea madude deep yaan ni ngumu kueleweka hasa Kwa watanzania wengi wa hali ya chini....πŸ€£πŸ€£πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Aluta continue
 
Ni
Please naomba uni pm tuyajenge Kama upo real kaka
 
Hedge fund or mutual fund even pension fund wanafanya kazi hizi pia Mana Wana hela nyingi mno za watu so wanazizalisha
 
Kilichkuponza ni tamaa na kujisahau period
 
Kwenye huu uzi The Best Of All Time ndo naona anauelewa na FX vizuri. Wengine wote mnapuyanga tu.
View attachment 2780303

See this beautiful usdchf movement to


Watanzania naemfahamu ni Franscesco Magnetics tu ndo milionea kupitia forex.

Wengine ni wauza maujuzi tu.
Wengine huwez wajua maana wapo lowkey hawana kujionesha me nawajua kibao
 
Unatumia nguvu nying sana kuwaelekeza hao wapumbavu achana nao ila hizo funded accounts watu ndo zituweka mjini yan usitumie nguvu nying kumwelekeza mtanzania mwache aamin anachoamin
 
Yani ulivyoelezea hivi hujatutendea haki kabisa wanajamvi wa Itigi na Nyarugusu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…