shaks001
JF-Expert Member
- Feb 6, 2014
- 1,246
- 1,070
Jana nilienda hospitali moja kubwa hapa jijini Dar.Nilikuwa nasumbuliwa na homa ikiambatana na maumivu ya mara kwa mara ya tumbo.Kwa maelezo ya Dr. ilibidi aniandikie kipimo flani hivi kinaitwa OGD.
Mungu wangu!Katika siku nilihisi roho yangu inatengana na mwili ilikuwa jana, hicho kipimo unaingizwa "li-mpira"jeusi kubwa mdomoni linasokomezwa mpaka tumboni kwa muda kama wa dakika mbili au tatu.Kwa kipindi hicho huwezi kupumua vizuri, huwezi kuongea, huwezi kutema wala kumeza mate, macho yanakutoka kama fundi saa kapoteza nati.Yaani ni mateso jamani.Hayo yote yanafanyika baada ya kupuliziwa dawa ya ganzi lakini wapi bwana, hakuna ganzi kwenye kukata roho.
Na ndio maana kipimo hiki unatakiwa ufanyiwe kabla hujala chochote maana ukitumbukizwa ule mpira ni lazima utapike.Yaani leo hii nahisi ile mikwaruzo ya ule mpira bado ipo kuanzia kooni mpaka kwenye utumbo.Aisee sitakubali nifanyiwe hii kitu labda niwe mahututi sijitambui.
Labda wataalamu wa mambo haya mnijuze, je hata huko kwa wenzetu kwenye nchi zilizoendelea wanatumia njia hii ya kutumbukizana madude haya tumboni au kuna njia nyingine? Maana siamini kama mzungu anaweza kuvumilia mateso haya.