Usiombe uende hospitali ukafanyiwa kipimo hiki cha OGD

siku nyingine usiombe ufanyiwe kipimo kinaitwa FEMOLO..utaona kume hiyo OGD ni cha mtoto..
 
Si bora ya hicho! Nasikia ukifanyiwa cha tezi dume unaweza kuwa mteja wa vilainishi.
 
Mi nadhani kipimo kikali kuliko vyote ni kile cha angaza....maana ukiwa unangoja majibu utaomba ardhi ifunuke...kwanza ukiingia tu unaona wagonjwa wote wamekata tamaa yani balaa tupu..
 
Nimesoma tu maelezo yako nimesikia maumivu hadi kwenye utumbo, siku nikisikia wanataka kunipima takataa hadi dk ya mwisho.
 
Oesophago-gastroDuodenoscopy(OGD) kipimo hiki hutumika kupiga picha ya oesophagus,na utumbo mdogo wa mwanzo kutazama kama kuna matatizo yoyote kama vidonda au vivimbe.
Mbadala wa njia hii ni kunywa Barium then picha ikapigwa kea nje kwa x-ray.
Lakini faida ya OGD ni kuwa inaweza kutumika kuondoa vivimbe(polyps) endapo vitabainika kuwepo.
Kuhusu wazungu, kipimo hicho hutumika sana na nchi zilizoendelea kuliko hata huku kwetu, kwa hiyo usiogope kipimo hiki kiko very accurate, kinaweza kudetect hata kesi ambazo barium method haiwezi.
 
wakuuuu hiko kipimo kipo popote hasa hospitali kubwa na hicho kinafanya kazi ya kuangalia vidonda vya tumbo na ni kweli unapimwa kabla hujala chchote mana ni mpira unaingizwa kweny mdomo had kuzama ndani ya koo ili kuweza kuangalia ndani kukoje km unavidonda au lah na kunakuwa na video ya kutazama ulivy ndan ya tumbo lako.... ili waweze kuona ndan ila ww unaepimwa huwez kuonaa chcht utabak tyu kuambiwa labda uchungulie nd utaonaa ila kiukwel kinamaumivu makali sanaaa ila kabla ya hapo unapuliziwa dawa ili usiiumie wala kuhisi maumivu......ila pole sana mkuuu kwa kuwekwa huo mpira.....
 
kwel mkuuu unachosema nina imani na maneno yako upo sahihi......[emoji106]
 
Acha kabisa hicho kipimo ni kwere!! Sema tu ni kizuri kwani hakuna longolongo
 
Nn OGD bwana!!! ngoja siku upigwe PR tuone kama utaleta mrejesho humu.
 
Pole kwa yaliyokukuta, ila ni wajibu wa daktari ajiridhishe ni nini kinakusibu.
 
acha tuuu umenikumbusha mbali sana aise nilisumbuliwa na tumbo ilikuwa appendicity. ilikuwa bado kidogo ipasukie tumboni kwenda hospital nikamkuta nesi mdogo ata mimi nimemzidi kiumri eti ndie alieniaandaa ili niingizwe chumba cha upasuaji....dah siku na jinsi yule dada aliishika ikulu yangu akaingiza mpira maalum ghafra mkojo ukaanza kutoka wenyewe baada ya huo mpira kuingizwa. sio siri hadi leo nalikumbuka hilo tukio na kila nikimuona huyo dada najikuta nacheka tuu maana alifanikiwa kuyaona maungo yangu
 
Appendicity= appendicitis.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…