Jamani wahasibu wenzangu mnafeli wapi?
Nipo na mrembo kawe Leo, mara akapita Kaka mmoja rafkiangu akasonya. Nikamwuliza shida nini, jibu nililojibiwa sikuamini
Mrembo: huyu Kaka bwana alinitoa out weekend, nikaenda nae huko Kwa hotel, tumeongea vizuri, tumekuwa, tumekunywa, tumefurahi, kanisumbua wiki 2 nikakubali kutoka nae out, alafu ananiletea mambo ya kizamani
Money Penny: mambo gan tenaaa?!
Mrembo: bili ilipokuja ananiambia tugawane malipo nusu Kwa nusu, yeye alipie nusu na Mimi nilipe nusu
Money Penny: bili ulikuja bei gan?!
Mrembo: laki 1 nanusu
Money Penny: na wewe 75 haukuwa nayo au?!
Mrembo: nilikuwa nayo, lakini yeye ndio kanisumbua, alitakiwa alipe yeye sio Mimi, Yani wanaume wengine ovyo Sana, anasema yeye NI mhasibu WA kampuni moja hapa mjini, nashangaa Leo kumkuta hapa Kawe🙄
Wahasibu WA skuhizi sijui wamekuwaje?!
Siwashauri wadada kutoka out na mhasibu
Money Penny: mkayamalizaje na Kaka WA watu?!
Mrembo: sikulipa, nikaondoka nikamwacha ananiangalia,
Jamani wahasibu wenzangu WA kiume mnafeli wapi?! Au ndio uchumi WA Kati?