Kiraka
JF-Expert Member
- Feb 1, 2010
- 4,285
- 4,074
Kipindi nakuwa enzi za primary, seko hadi chuo nilikuwa mtazamji bora wa CNN na BBC.
Lakini sikujua kuwa vyombo hivi vimekaa kimlengwa zaidi, yani vinakupa habari zile wanaziona wao ndio muhimu katika itikadi yao huku wakiwa wana-criticize wasio na itikadi kama zao.
Na nilihabarika kupitia CNN na BBC kwa uhakika hadi hapo Trump alipokuja kugombea uraisi na kushinda uchaguzi. CNN walinifanikisha kufanya nimchukie Trump ila kwa baadae sasa nikawa nashangaa inakuwaje CNN wanampinga Trump kiasi hiki na kumtetea Hillary to the maximum.
Ndio nilipofanya uchunguzi nikagundua kuwa CNN ni chombo cha habari chenye mrengwa wa kushoto ama liberals ama woke ama far-left.
CNN na BBC kama mrengwa wa kushoto ndio wanao-promote haki za utoaji mimba, uhamiaji usio na mipaka, kubadirisha jinsia watoto, haki za mashoga na wasagaji, pro-palestine, etc
Ila Trump aliingia madarakani na
alifanya vizuri sana na sera zake nilizikubali sana.
Hii ni guide ya baadhi ya vyombo vya habari na itikadi zao.
CNN: Mrengwa wa kushoto,
BBC: Mrengwa wa kushoto
FOX: Mrengwa wa kulia
Al Jazeera: Mrengwa kushoto usio wa mbali, pro-Radicalism, pro-palestine
Chombo cha habari maarufu kisichokuwa na mrengwa ni REUTERS
Samahi mkuu, hivi Mrengwa ni neno la kiswahili? maana hii lugha yetu inatambaa na kukua kwa kasi sana. Nielekeze mkuu maana ya neno hilo nimejikuta natoka kwenye mada kwa kutatizwa na hilo neno.