Mwanasayansi Kalivubha
JF-Expert Member
- Feb 4, 2024
- 344
- 926
MJINI ISHI KIMKAKATI LA SIVYO UTAISHIA KUZURURA NA KUTUMIKISHWA TU😔
Wimbi la vijana kupenda kuishi mijini hasa kwenye miji mikubwa lipo Duniani kote na hii ni kutokana na ukweli kuwa mijini kuna fursa nyingi zinazofanya matajiri wengi kutengenezwa huko.
Pamoja na ukweli huo ila unatakiwa mjini uishi KIMKAKATI la sivyo utakuwa mjini ndio ila kusindikiza tu wengine na usipokuwa makini utajikuta ukidumbukia kwenye uraibu na uteja wa madawa ya kulevya kwa sababu ya msongo wa mawazo.
Wapo watasema walienda mjini bila dira yoyote na wakataboa ila usidanganywe nao bali wewe hakikisha una mipango kabambe ya kukufanya uishi mjini kama MFALME.
Mjini ili uishi kama MFALME basi uwe na utajiri mkubwa tena kwa njia halali basi hapo utakuwa umefanikisha kuishi KIMKAKATI tofauti na hapo utakuwa mzururaji tu mjini huku ukishangaa magari mapya na nyumba mpya za wengine.
Mjini bila kuwa na mkakati basi utaishia kuwa Mtumwa wa watu ambao wapo mjini KIMKAKATI.
Kama ni mwajiriwa usisahau kuna gharama za nauli za kila siku huku ukiwa na muda mchache wa kupumzika kutokana na foleni za mjini utafika nyumbani saa nne usiku na ili kulinda kibarua chako itakulazimu uamke saa kumi usiku ili uwahi eneo lako la kazi na usipokuwa makini hata ndoa yako itakuwa hatarini kwa sababu purukushani za kugombania usafiri sio mchezo lazima ufike ukiwa umechoka hatari.
Na Mjini bila kuishi KIMKAKATI maisha yatakupiga hasa kwa sababu ukitaka kuendana na mji huku huna mikakati basi utakopa ili ununue gari na ukijitahidi sana utajenga umbali wa kilomita 30 kutoka eneo lako la kazi sass hapo utafurahia kuwa na usafiri na nyumba ila nyuma ya pazia maisha yanakuburuza hatari.
Mjini ishi KIMKAKATI kwa kuwa na malengo ya kuwa na ukwasi huku ukiyaweka kwa vitendo na usisahau kuwa Dikteta wa maisha yako mwenyewe yaani zile huruma za mikoani zipe kiasi kwa sababu mji huwa sio rafiki kwa mtu ambaye hana kiasi, Wekeza kwenye biashara huku ukiwa na nidhamu ya juu katika mtumizi ya pesa.
Mjini weka aibu pembeni kisha ingia ulingoni kutafuta pesa muhimu tu iwe kwa njia halali, usijionee huruma kama watu wa mikoani kwa sababu mjini akili inatakiwa iwe juu sana la sivyo wewe ndio utakuwa mtumwa.
Mikoani watu wakiwa na elfu kumi ni kubwa sana kwa siku ila kwa mjini ukiwa na elfu kumi itaishia kwenye nauli na kununua maji hivyo lazima uwe na akili ya kutengeza fedha zaidi ili uweze kulimudu jiji.
Mwanasayansi Saul kalivubha
Fikia Ndoto Zako.