Usipokuwa makini na unywaji wa pombe maeneo ya starehe, unaweza kupata mahusiano yasiyokuwa na tija

Usipokuwa makini na unywaji wa pombe maeneo ya starehe, unaweza kupata mahusiano yasiyokuwa na tija

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Kuna siku nilikuwa nimechoka sana, kutokana na changamoto za kidunia, nikaamua kwenda kiwanja na jamaa yangu kwa ajili kupiga kinywaji pamoja na kuosha osha macho kwa kuangalia watoto wazuri. Siku hiyo tulipiga pombe sana huku tukibembelezwa na ‘ live band’. Baada ya kukaa masaa kazaa, tukaona bora tupadilishe kiwanja mida ya saa sita usiku.

Tulipoingia hichi kiwanja kingine, mambo yalikuwa moto sana, utafikiri mchana kumbe ni usiku. Wenye kutumia ile mitungi ya moshi, pombe kali, watoto wazuri n.k vyote vinapatikana; muhimu mfuko wako tu uwe vizuri. Uzuri wa hiki kiwanja wote ni wastaarabu, hakuna fujo na ulinzi ulikuwepo wa kutosha.

Sasa, kutokana na pombe nilizokuwa nimekunywa huko nilikotoka kichwa kilikuwa kimechanganya nikawa mchangamfu sana. Kila mrembo niliyekuwa namuona, ilikuwa nilazima nirushe maneno mawili au matatu. Mnavyojua tena, watoto wazuri huwa hawasumbui, wanakukaribisha mnapiga stori mbili tatu, maisha yanaendelea.

Sasa, kuna meza moja ilikuwa na nafasi na kulikuwa na walimbwende watatu; nikaamua kuisogelea tu ili iweze kunipa sapoti hapo ukumbini, Muhudumu akaja kunihudumia, nikaona si vizuri pale mezani nijiagizie mwenyewe wakati wale niliowakuta, chupa zao zilikuwa zinakaribia kuisha. Ikabidi nao niwaagizie ili meza ichangamke.

Tukawa tunabadilishana mawazo ya hapa na pale, pia kujua wanafanya mishe gani n.k Sijakaa sawa, nikamuona huyu mrimbwende aliyekuwa karibu na upande wangu, anatikisa nyonga, kwa sababu mimi ni mtu mzima, sikushtuka kwa sababu ndio mambo ya mjini haya. Akaniomba simu yangu anataka aandike namba yake, nami nikampatia kwa sababu sikuona cha ajabu kutokumpatia. Kisha akajitumia meseji, ili namba yangu aweze kuipata.

Muda unavyozidi kwenda, ndio kama mchana unazidi; jamaa yangu akaja kunidokeza, hapa tuondoke kwa sababu tumelewa sana, tukizidisha sana tunaweza kujishushia heshima. Ikabidi nizuge, muhudumu alipokuja kuhudumia, nikamwambie awaletee huduma huku nayeye achukue chupa mbili, nikamlipa kinyemela, tukatoka kimya kimya bila kuwaaga pale mezani.

Siku iliyofuata, nikawa nasumbuliwa kwenye simu na warembo niliokutana nao kiwanjani; nikajitafakari, nikaona hakuna ulazima wa kuanzisha mahusiano mapya, kwa sababu yataniharibia mipangilio yangu. Kwa sababu mahusiano mengi yanahitaji kutoa pesa, kuliko kupokea pesa kwa mwanaume. Ila mmoja alikomaa sana, baada ya kumtathimini na kumuona hana madhara sana, na ni mtu wa mishe za kibiashara (madini); akaingia kwenye kumi na nane.

Kwenu, wakuu; kunywa pombe maeneo ya starehe yalishawaletea mahusiano ya kudumu na yenye tija?
 
NAPIGIA MSTARI MKUU

FB_IMG_16461513006897064.jpg
 
Kuna siku nilikuwa nimechoka sana, kutokana na changamoto za kidunia, nikaamua kwenda kiwanja na jamaa yangu kwa ajili kupiga kinywaji pamoja na kuosha osha macho kwa kuangalia watoto wazuri. Siku hiyo tulipiga pombe sana huku tukibembelezwa na ‘ live band’. Baada ya kukaa masaa kazaa, tukaona bora tupadilishe kiwanja mida ya saa sita usiku.
Ukisikia kwenye Pombe kuna ufisadi ndio huo sasa,inatoa nafasi ya wewe kujaribiwa na shetani wakati uwezo wako binafsi wa kumshinda umeshavurugwa,hapo usitegemee kingine zaidi ya anguko......
 
Ukisikia kwenye Pombe kuna ufisadi ndio huo sasa,inatoa nafasi ya wewe kujaribiwa na shetani wakati uwezo wako binafsi wa kumshinda umeshavurugwa,hapo usitegemee kingine zaidi ya anguko......
Ni kuwa makini tu pamoja na kujihadhari ukiwa kwenye hayo mazingira.
 
Back
Top Bottom