Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Historia inaonesha kuwa hakuna Mwenyekiti wa CCM aliyedumu kwenye nafasi hiyo akiwa nje ya Urais.
Mwalimu alipotoka madarakani harakaharaka akamuachia Ally Hassan Mwinyi uenyekiti wa CCM akiwa Rais.
Mwinyi naye alipotoka kwenye Urais akamwachia Benjamin William Mkapa uenyekiti wa CCM ambaye wakati huo alikuwa Rais wa Tanzania.
Mkapa bila ya kupoteza muda Jakaya Mrisho Kikwete alipochaguliwa kuwa Rais wa Tanzania, akamwachia uenyekiti wa CCM Jakaya.
Jakaya naye akafuata nyayo za watangulizi wake kumuachia uenyekiti wa CCM John Pombe Magufuli.
Magufuli alipokutana na faradhi ya kifo, CCM haraka haraka wakamkabidhi Samia Suluhu Hassan uenyekiti wa chama Chao.
Kwa mtiririko huo inaonesha shayiri dhahiri kwamba wanachama wengine woote wa CCM hawatakiwi hata kwa bahati mbaya, kuwaza kuwa siku moja wanaweza kuwa mwenyekiti wa CCM Taifa.
Kwanza mfumo wa kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa hakuna kugombea. Kamati Kuu huteua mtu ambaye hupitishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho.
Kwa ivo wenye chama chao ( Kamati Kuu na Halmashauri) wameshaamua kuzuia wanachama wengine wote kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa mpaka wawe Rais. Tena Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania. Rais wa Zanzibar haruhusiwi.