Usipokuwa Rais huwezi kuwa Mwenyekiti wa CCM!!??

Usipokuwa Rais huwezi kuwa Mwenyekiti wa CCM!!??

Ni utamaduni wa CCM

Na Rais anapomaliza mihula miwili humleta yule anayemwamini amrithi
Ni janja ya CCM kutaka ati dola ndo iwe kiongozi wa chama chao.

Katiba mpya ndiyo dawa yao hawa jamaa, Tanganyika si mali yao binafsi ya hiki kikundi kidogo.
 
Tanzania Hatuaminiani Ndugu yangu Hebu fikiria Kwa matukio yanayoendelea Chadema..

Lets Say Mbowe akawa mwenyekiti Halafu lissu akawa ndo Rais unafikir Kingetokea Nini?

Mbowe angemfuta Lissu uanachama na Akawa ndo amekoma kuwa Rais..

Ukiacha Hivyo Fikiria Kuwa Mpina Ndo angekuwa Mwenyekiti wa CCM halafu mama Samia ndo Rais Unafikiri Angeshindwa Kumpa Onyo Rais??
Ndo tunacho taka,chama kimuwajibishe pia mwana CCM mwenzao pale anapo fanya tofaut na matakwa ya wananchi.
 
Kwa ivo tuna mfumo dhaifu (Fragile) dhaifu wa siasa zetu.
Precisely..
Na hujakosea Kabisa..
Kwanza hatuna Mfumo wa Accountability hata Kidogo..
Alwayz Viongozi wanaamini Mkubwa huwa Hakosei na akikosea Ni haki yake Kusamehewa Akiomba Msamaha ila Mdogo hukosea na Akikosea Msamaha wake lazima apewe masharti..

Kwahyo ni Vigumu kumpa Cheo cha Mwenyekiti Mtu mwingine..
Sababu Akikosea Mnakuwa wakubwa Wawili na hicho hawakitaki
 
Ndo tunacho taka,chama kimuwajibishe pia mwana CCM mwenzao pale anapo fanya tofaut na matakwa ya wananchi.
TUkifika kwenye Hatua Hii Nitafurahi sana..
But Unfortunately Sasa Hivi chama Kinatetea Viongozi hata wakifanya Makosa...

Siku hizi kuna Slogan kama "Alikuwa Anatania", 'Ulimi uliteleza", "Alikosea" ila hakuna hata sehemu moja Chama kitamuwajibisha zaidi ya Kuunda Tume, Vijana na Machawa wa Kumsafisha..Tooo Bad
 
Kabisa Mkuu. Lakini wenzetu South Africa wameweza. ANC ina nguvu ya kumuwajibisha Rais wao, Maana mwenyekiti wa chama cha ANC siyo RAIS
 
Ni kweli kwamba huo ndio utamaduni wa CCM ambao wameiga kutoka kwa Watawala wadhalimu wa Kikomunisti/Ujamaa, hususani kutoka kwa Chama Cha Kikomunisti Cha China kilipokuwa chini ya Mwenyekiti wake Mao, ambaye pia ni Mwanzilishi wa chama hicho.

Hapo ndipo ilipoanzia falsafa potofu na ya kidhalimu ya 'Zidumu Fikra za Mwenyekiti.'

Chini ya Falsafa hii potofu na ya kidhalimu, Wakomunisti wanaamini kwamba 'Mwenyekiti wa Chama Tawala' ndiye mtu pekee katika nchi ambaye mwenye akili nyingi na akili kubwa zaidi kuliko mtu mwingine yoyote yule. Hivyo, hapaswi kukosolewa.
Aidha, chini ya falsafa hii Wakomunisti watawala wanaamini kwamba 'raia wote katika nchi ni kama mateka wa Mwenyekiti.'
Na mfumo huo ndo umefanya wahafidhina, ndani ya taifa hili kuona taifa kama mali yao binafsi na vizazi vyao.

Lakini chama cha kikomonisti cha china na Vietnam ni tofauti na hiki chama Cha mboga mboga.
 
Ooh Sawa sasa....
UNajua kwanini?
Mwenyekiti wa Chama Ni Mwamuzi wa wanachana wote, Sasa Imagine kama Mtu mwenye Power Kiasi Hicho hatoweza kuwa Nje ya Mfumo wa Serikali anaweza kwa matakwa yake aka Sabotage Baadhi ya Mipango ya Serikali, Sasa Ili kuepusha Hilo Ni lazima Awe Ni kiongozi wa Serkali pia Kwa hiyo TOP AT PARTY (Chama) TOP AT GAVOO
Hili jambo la Rais wa nchi kuwa Mwenyekiti wa Chama,baadhi ya viongozi makini wa bara hili walikataa mfano ni Nelson Mandela,lakini viongozi waliokuwa waroho wa madaraka, walilipenda hili.Ndio maana taifa lilikuwa bize kujenga ofisi za chama kila kijiji kuliko shule na ujenzi wa Viwanja vya mpira kila makao makuu ya mkoa kuliko vyuo vya Kati.
 
Kabisa Mkuu. Lakini wenzetu South Africa wameweza. ANC ina nguvu ya kumuwajibisha Rais wao, Maana mwenyekiti wa chama cha ANC siyo RAIS
Nelson Mandela alikuwa Mwalimu bora,katika kuleta balance of power,sababu mwanadamu hasa ngozi nyeusi ina ubinafsi wa kiwango kisicho Cha kawaida,hili lilimfanya kutenganisha hizo nafasi mbili,sababu hakuwa mroho wa madaraka au kujiona yeye bora kuliko wengine.
 
Rtd Brigedia Kinana amewahi kuwa na Fikra Za kutenganisha kofia Za Urais na Uenyekiti wa Chama ili chama kiweze kuisimamia na kuiwajibisha serikali inapokengekeuka..Sina hakika ikiwa bado anaamini ktk hili🔗
 
Hii hofu ya kutokuheshimiana chanzo chake ni kugeuza siasa ndiyo chanzo cha utajri.

Kama watu wangekuwa wanafanya siasa nje ya maslahi ya kifedha, mambo ya kuogopa kupinduana yasingekuwepo!!
 
Ingetikiswa na nani maana ilikua enzi ya chama kimoja
Ni kweli. Lakini unajua sababu yake?

Halmashauri Kuu ya CCM ilikuja na hoja ya "ujenzi wa chama" ambapo ilisemwa Mwalimu angeondoka ghafla CCM ingetikiswa.

Kwa ivo Mwalimu alichelewa kuondoka ili amalize Program ya Ujenzi wa chama.
eti
 
Historia inaonesha kuwa hakuna Mwenyekiti wa CCM aliyedumu kwenye nafasi hiyo akiwa nje ya Urais.

Mwalimu alipotoka madarakani harakaharaka akamuachia Ally Hassan Mwinyi uenyekiti wa CCM akiwa Rais.

Mwinyi naye alipotoka kwenye Urais akamwachia Benjamin William Mkapa uenyekiti wa CCM ambaye wakati huo alikuwa Rais wa Tanzania.

Mkapa bila ya kupoteza muda Jakaya Mrisho Kikwete alipochaguliwa kuwa Rais wa Tanzania, akamwachia uenyekiti wa CCM Jakaya.

Jakaya naye akafuata nyayo za watangulizi wake kumuachia uenyekiti wa CCM John Pombe Magufuli.

Magufuli alipokutana na faradhi ya kifo, CCM haraka haraka wakamkabidhi Samia Suluhu Hassan uenyekiti wa chama Chao.

Kwa mtiririko huo inaonesha shayiri dhahiri kwamba wanachama wengine woote wa CCM hawatakiwi hata kwa bahati mbaya, kuwaza kuwa siku moja wanaweza kuwa mwenyekiti wa CCM Taifa.

Kwanza mfumo wa kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa hakuna kugombea. Kamati Kuu huteua mtu ambaye hupitishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho.

Kwa ivo wenye chama chao ( Kamati Kuu na Halmashauri) wameshaamua kuzuia wanachama wengine wote kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa mpaka wawe Rais. Tena Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania. Rais wa Zanzibar haruhusiwi.
wanakula kijamaa ila wanaishi Kibepari!
 
Kumbuka kwamba CHAMA kinashika HATAMU, jee unajuwa maana ya HATAMU?
ukishajuwa maana ya hilo neno utaelewa ni kwanini Raisi wa Jamhuri lazima awe mwekiti .....
 
Back
Top Bottom