Hujui nini kinaendelea nyumbani, ila kwa kuwa upo, unafahamu kuwa kuna nyumbani. Ukirudi nyumbani, hali yoyote utakayoikuta, ni kwa sababu upo. Ikiwa hukuweza kurudi nyumbani, kama bado upo, utakuwa unafahamu kuna nyumba uliacha, labda na familia na unaweza kutafuta namna ya kufika kuangalia nyumba au ukapiga simu kujua hali ya nyumbani. Ila usipokuwepo kabisa, usipoishi, hakuna namna yoyote utafahamu kuwa ulikuwa na nyumba. Kimsingi, kwako, hakuna kitu kama nyumba, wala familia, wala Mungu. Vitu tinavyoviona kuwa vipo, vitaendelea kuwepo ikiwa nasi tupo. Tusipokuwepo, hakuna chochote na wala hakikukaa kutokea kuwepo, hadi utakapokuwepo.