Usipomtongoza Mwanamke Umtakaye ujue Umejipiga chaga Mwenyewe

Usipomtongoza Mwanamke Umtakaye ujue Umejipiga chaga Mwenyewe

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2023
Posts
382
Reaction score
687
Kama hujamfata kuongea naye.

Kama hupeleki mahusiano mbele.

Kama hufanyi chochote kumuonesha unamtaka.

Basi ujue hana haja ya kukukataa. Sababu umeshajitoa mwenyewe bila hata kutolewa.

Zile sababu kama “atakua bize”/ “atakua na mtu wake”/ “mi sitokagi na wanawake aina yake”/ “sina mstari mzuri bado”/ “hatonikubali” vyote ivyo ni visingizio tu ili ujifelishe mwenyewe.

Au unajikuta unamsubiri mwanamke akufate mwenyewe.

Au unasubiri muujiza mwanamke akufate mwenyewe, achana na muvi.

Kuhusu hayo, sahau.

Hata kama atakufata mwenyewe anakutegemea wewe kuwa kiongozi.

La sivyo hayo mahusiano hayatodumu.

Ukweli ni kuwa mwanamke hawezi kukufata kirahisi.

Kwake ni muhimu zaidi kutunza hadhi yake na heshima.

Ili asionekane rahisi mbele ya jamii. Mana utawahadithia tu marafiki zako.

Naye atajitoa kwako na kusema “ah itakua hajanipenda” sababu anaona huongozi kitu. Kisha ataenda kwa mwengine ambaye ataweza kumuongoza.
.
Na hata ukimfata usijitoe mapema.

Usijikatie tamaa mapema. Mwanzoni hatojiachia kwako haraka. Ili ailinde hadhi. Asionekane wa kirahisi rahisi.
Ni muhimu uendelee kumuongoza na kumfanya ajisikie amani kwako.

Na ukimzoesha kumuongoza inakua rahisi mnapoingia kwenye mahusiano kumuongoza.

Ila kwenye mchakato wote akijisikia ye ndo kiongozi au anajishobokesha sanaa ataanza kujitoa/ kupunguza kasi.

Hivyo ni muhimu usikate tamaa mapema kumuongoza wakati unamtongoza.

Naye atapata sababu ya kujitetea kwanini kajiachia kwako “mambo yalienda tu…”/ “tulikua tunaendana tu…”
Japo mwanamke anaweza kujiachia kwako hata kabla hujamtongoza, lakini mara nyingi ni yule ambaye humtaki.

Pia ikitokea kwa unayemtaka ni mara chache, au kwenye mahusiano ye ndo atakua kiongozi.

Ila sio ndo uombe ombe penzi bila mwisho kisa tu usikate tamaa.

Bali umtongoze kwa njia itakayomfanya awe na hisia nawe.

Jiwekee kwamba bora uende ujue amekukataa kuliko kujikatalia mwenyewe hiyo nafasi.
 
FB_IMG_16820621340743858.jpg
 
Mfano umwemwona binti mzuri aidha uko safarini, kwa bahati mbaya akawa labda yuko na wazazi!! Utatumia mbinu gani kuongea nae japo upate hata namba yake ya simu? Infinite_Kiumeni
Hii iliwahi nitokea aise.. nilimuelewa sana binti tatizo alikua na mama yake benet yani mama aachi mwanya na binti akawa ashaelewa shida iliku ni kumfata aise nipate namba yake.... Nilisimama zaidi ya masaa matano kumzungukia lakini aliishia kuondoka na mama yake bila hata kupata mawasiliano naye japo nilikua na muashiria kwa mbali na akawa anaelewa ila shida ni chance.. na yeye hakuweza hata kudanganya anaenda maliwato ili nikambanie huko... Japo naamini ipo siku nitakutana nae. Ila mama yake nakutana nae mara kwa mara sana..

Binti furaha popote ulipo jua bado nakukumbuka ila ndio hivyo
 
aise! Najaribu kufikiri itakuwaje ikiwa utamfuata kistaarabu mbele ya mama yake jinsi itakavyokuwa.. Je utakuwa ni utovu wa nidhamu na kumkosea adabu mama mzazi?? infinite_kiumeni njo apa bhana we si ndo umeleta mada?
 
Ila we jamaa ubongo wako umejaa mapenzi tu
mwamba mmoja maarufu kama KENGE 01 alituletea uzi akijaribu kuelezea fursa mbalimbali znazopatikana burundi ni zaidi ya siku 4 lakini ana kura si zaidi 50. Nyuzi za mapenzi huwa zinakuwa na pages kama dictionary[emoji3].. Sasa kwanini mtu asilete vinavyopendwa na wengi[emoji3]
 
Kwan kuna watu bado wanajifunza maenzi?
 
Back
Top Bottom