Usipuuze naomba ushauri wako wa hali na mali

james bendui

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2015
Posts
693
Reaction score
690
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 23 nina kazi nzuri kwa mwezi sikosi kama laki tano na kidogo na nina mwaka tu kazin na nimepata pesa kama milion 28 hivi na sina dira nzuri ya mafanikio endelevu na nina uwez wa kukop pesa bank sio chini ya milion 15 na bado sijajenga nyumba au kuwa na kitu cha samani zaidi ya hivyo.

Naomba ushauri wenu ndugu kaka na dada zangu na wote JF najua wapo watu makini na wenye uwelewa mzuri wa kimaisha zaid yangu kweli nipo njia panda sijui nifanye nini na ni mara ya kwanza kushika pesa ndefu kama hiyo naomba msinizarau na kunichukilia tofauti kwa kuniambia maneno ya kunivunjaa moyo kama wazalendo na wakubwa zangu naheshimu mawazo yn na ht walio chini yangu naomba ushauri wenu wa hali na malii naogopa kuja kujituia kwa fursa hii niseme niliyobahatika kwa sasa asanteni wote.
 
Ungeelezea hasa uelewa wako Mkubwa upo katika nini!
Kwasababu kuna fursa nyingi sana ila nyingine zinahitaji uelewa Fulani(elimu) lasivyo ukiingia kichwa kichwa utaishia kupigwa na wajanja!
 
kanunue bond za bank baada ya miaka miwili utapata faida na akili itakuwa imepata cha kufanya
 
Mkuu weka bank siku ukipata wazo lenye hesabu za kueleweka zitoe ulisukume
 
Unapendelea kufanya nn, fanya uchunguzi wa kitu unapendelea au kile una passion nacho take your time angalia opportunity ktk hcho kitu anza kufanya yani anziahapohapo unapoona sahihi, utajifunza kadiri muda unavyo songa
NB.,hakikisha unatuliza akili kwanza bwana mzee
 
kwanza usikope mkopo ni haramu utakomba hyo hela yote.kuna biashara nyingi tu za mtaji mdogo na zina return nzuri hata m 28 haitoisha.
kwa ushauri zaidi njoo pm ili tuonane nikushauri vizuri dogo
 
Fungua pharmacy inalipa sana na kama hutojali mm n professional nitasaidia kuoperate iyo pharmacy 0658047048
 
Angalia Bank yenye riba kubwa kidogo ukiweka fixed account then ukaziweke. Wakati huo uwe unafanya research ya kitu cha maana cha kufanya. Ukipuuza huu ushauri, mwakani muda kama huu utakuja kuaomba ushauri wa jinsi ya kukwepa kujiua kwa ugumu wa maisha.

Saiv sio muda mzuri kwako kwa kutafta kitu cha kufanya, tuliza akili na uzisahau hizo pesa kama vile hazipo.
 
kwanza usikope mkopo ni haramu utakomba hyo hela yote.kuna biashara nyingi tu za mtaji mdogo na zina return nzuri hata m 28 haitoisha.
kwa ushauri zaidi njoo pm ili tuonane nikushauri vizuri dogo
[emoji121]
Mshauri hapahapa! PM ni upigaji mtupu hako!
 
Mi nipo kibiti kuna kiwanja nauza bei simple tu Kama wahitaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…