Usipuuze ndoto unazoota pindi unapokuwa umelala

Hakuna ndoto nimeiota mara nyingi kama ndoto ya kua madarasa ya nyuma tena hasa shule ya msingi. Mara chache kuota sekondari.
pole sana ,hiyo ni miongoni mwa ndoto mbaya.Kuna roho inayofuatilia ya kurudisha nyuma hatua zako ustawi/maendeleo/kukua/kuongezeka kustawi kwako(kiroho na kimwili)
Ukiombea ndoto hiyo kemea na kataa roho za kurudishwa hatua zako nyuma na kuimarisha mahusiano yako na Mungu na maisha ya sala na toba,ibada,na kuziepuka dhambi.Mungu atakushindia atakustawisha .Ameni.
 
Watakwambia ukiota umeokota hela maana yake kuna adui anakunyemelea, shetani yupo kazini zidisha maombi
Hakuna kitu cha bure katika ulimwengu wa Roho,unaweza ukaokota ukapokea pesa au zawadi ,ambayo imeniuziwa ina maagano ukawa umefungua mlango wa kumilikiwa na nguvu za giza.Au unaweza wewe ukatoa au kupekeka pesa yako,zawadi au sadaka watu wakaitimia kukudhuru.Mfano mtu anakupa zawadi mfano mavazi,pesa au chakula na kukufanyia uchawi kupitia hicho alichokupa au wewe unampa mtu zawadi pesa au mavazi viatu ,chakula na vikatumika kama sadaka ya kukudhuru inawezekana.Dawa ili haya yasitupate ni kuomba msaada wa Mungu ,ulinzi wa Mungu,kuimarisha madhabahu zetu kwa sadaka,fungu la kumi,maombi ibada,matendo mema na Mungu wetu ili kubatilisha nguvu ya madhabahu za adui wanaotutegea mitego kupitia kuokota pesa ndotoni,kupewa zawadi n.k,na kuweka ulinzi kwetu na mali zetu.Bila ulinzi wa Mungu wote tupo prone kushambuliwa na adui.HITIMISHO kuota unaokota pesa sio ndoto nzuri.Na hata kuokota pesa njiani ukiwa unatembea katika ulimwengu huu wa mwili physically nyingine zinakuwa zimenuiziwa au waswahili wanasema zometegwa.Japo kama una imani na nguvu ya Mungu hata ukute pesa imetegwa njia panda imetupwa hapo ,wamevunja nazi,wamechinja ndege,na kuna hirizi.Kama nafsi yako ina amani inakwambia okota hiyo pesa okota itolee fungubla kumi sadaka,chukua nazi kula ,ombea,hautadhurika.
 
Elezea kwa kina hapo kwenye roho ya umauti
roho ya mauti ni mapepo,majini,mizimu,wachawi,waganga wa kienyeji..(ufalme wa giza) umekusudiwa ufe,wakifanikiwa lazima watangulie kukuua ufe kwanza kwenye ulimwengu wa roho waue roho yako ndipo ifuatie kufa katika mwili.Infact shetani lucifer na washirika wake hao majini ,wachawi n.k hata shetani mwenyewe hawana uwezo wa kuua roho,ila wanachokifanya wanakuchukua msukule ,duniani tunaona kama umekufa ,ila inakuwa umechukuliwa msukule katika ulimwengu wa roho
NDOTO UTAKAZOKUWA UNAOTA
a)ndoto upo makaburini,majeneza,wanakuzika
b)hisia moyo wako utakuwa na HOFU KUU,wasi wasi sana woga uliopitiliza,huzuni kuu,kukosa amani,uzito moyoni,unaweza ukawa unaogopa kukaa hata chumbani,nyumba
c)sauti unaweza kusikia sauti zinakutamkia mauti
ni zinaweza zikawa ndoto za kujirudia rudia,inaweza ikaambatana na kuanza kuugua kuumwa mwilini.(hatua mbaya zaidi)
UAMUZI MBAYA UTAKAOUFANYA
Ni kwenda kwa waganga wa kienyeji,kuomba mizimu,kwenda kwa manabii wa uongo hawa wanaotumia vitu vya upako kama mafuta n.k mana nao ni mawakala wa kizimu ni sawa na wachawi au wagangabwa kienyeji.
SULUHISHO.
YESU PEKEE huyu Yesu yeye hana dini dininni za wanadamu ila mission ya Yesu ni kuokoa ulimwengu wote ,watu wa dini zote,kabila zote .Kuomba Yesu akuokoe na kuacha kushiriki ibada za mizimu wagangabwa kienyeji nankuacha dhambi.Toba na kusali.Mungu anaokoa.Shetani anaua kweli.
 
Ila katika vyote fanya ufanyavyo, ukiota unakata gogo jitahidi uamke la sivyo utakuta mashonde kitandani.

View attachment 3121674
ndoto za kuota unapuu hadharani,unapakwa kinyesi,umechafuka kinyesi ni ndoto mbaya ni kuvikwa VAZI LA AIBU uaibike katika maisha yako kazi yako mambo ufuatwe na ROHO ya KUAIBISHWA kufedheheshwa.Kukataliwa unanuka mavi.Pia ni uchafu mana safishabMATENDO yako,tubu dhambi uwe msafi.
Ndoto nzuri opposite ya hiyo KUOTA unaoga bafuni au unafua nguo zako chafu ziwe safi.KINYUME CHA HIYO.
 
Amen
Barikiwa sana.
 
Kitu inanitesa hii acha tuu
 
Nisaidie hii.. Nimekuwa nikiota napigana sana na watu na mara nyingi nakuwa mshindi,, pia naota nikiwa napaa kama ndege na nakuwa na furaha sana,, hiyo ya kuota madarasa ya nyuma ni kweli hii ndoto imenisumbua kwa muda sana ila ni kama mwaka na nusu sijaota naota tuu nikiwa uwanjani na wenzangu tunacheza ila kuwepo darasani sioti tena πŸ˜₯πŸ˜₯ni kweli pia maisha yangu yamerudi nyuma sana
 
1)kuota unapigana mana upo katika vita/mapambano na adui ,ukishinda maana yake Mungu akupa neema kwa uwezo wa Mungu umeshinda hiyo vita.(nzuri)ila lazima uji imarishe ulinzi wa kiroho kwa kuongeza ,kusali/kuomba,sadaka,matendo mema, ibada,na kumcha Mungu na kuziepuka dhambi,mana ukiendelea kuishi katika dhambi ni kuruhusu /kifungulia adui mlango wa kukusahambulia.
2)kuota unapaa ina maana a)una speed mbio kubwa umeshinda zaidi na nguvu zaidi,hatua kubwa ya mafanikio ikiwa unapaa ukiwa peke yako ukiwa mazingira ya asili,au unayoyafahamu na watu unaowafahamu b)japo kuota unapaa inaweza ikawa mbaya ni sawa na wale wanaoruka usiku kuwanga endapo utakuwa na watu usiowafahamu,mazingira ya kutisha,mfano unapaa makaburini? na je ?ukiamka unahisi nini moyoni furaha au huzuni lazima ikiwa suplemeted na hisia na sauti inaweza kuleta picha zaidi.
KWA CASE YAKO NI MAANA NZURI mana unakuwa na furaha ni tunda la roho mtakatifu,na kushinda mapambano naweza nika conclude ni postive ni MAANA NZURI KWAKO.
3)Pole kwa ndoto za kurudi nyuma,mana yake siyo mpango wa Mungu urudi nyuma,Mungu huwa ni baba wa kuongezeka ku multiply kizaliana anayeharibu,kuiba kuua,kutesa na kurudisha nyuma ,kuchinja na kuua ni ADUI.Mungu anatuwazia mema na anatupenda ndio maana akamtuma Yesu atuokoe tusipotee.YESU akustawishe akuridishie vyote alivyoiba adui,miaka iliyoliwa na iliyoibiwa,vyote vitarudi kwako kwa jina la Yesu.Omba kemea na kataa roho ya kurudishwa nyuma.Mungu atusaidie tuishi maisha ya ushindi aliyotukusudia tuishi
.Ameni.
 
Niliwahi kuota ninamfufua mtu ambaye watu walisema amekufa huku mimi nikimwangalia naona kama amelala tu. Hii tafsiri yake nini mtaalamu?
 
Niliwahi kuota ninamfufua mtu ambaye watu walisema amekufa huku mimi nikimwangalia naona kama amelala tu. Hii tafsiri yake nini mtaalamu?
Kama watu walisema amekufa (mfu) na kama ni kweli hapa duniani haishi tena anahesabika mfu.Ina maana mbaya kukutana na wafu ndotoni,ni roho za wafu/mauti wengine wanaita mizimu ila ni mapepo,majini ,au roho za mauti.
kufufuata mana yake kama alishakufa ukamfufua ni sawa na kumuita mzimu,roho ya mauti na akaja,hata wachawi,waganga wa kienyeji,majini nk huwa wana njia ya kuita roho ya maiti kaburini ikaja mfano wa kufufua na (ROHO YA MAUTI,MIZIMU ,MAPEPO,MAJINI)ni ndoto mbaya kukutana na wafu.
JE ilikuwa ni wapi makaburini? nanje huyo mtu alikuwa kafa kweli na alizikwa?au alipotea hajulikani alipo?

ila ingekuwa umeota UNASALI unaomba kwa Mungu halafu kupitia maombi yako Mungu akakupa neema ya yule unayemuombea ambaye watu walisema amekufa Mungu akamfufua akaopona kupitia maombi ingekuwa nzuri.Au huwenda ingekuwa na maana hajafa ila kachukuliwa msukule ,mana hawa misukule wana uwezo wa kurudi mana roho zao hazijafa ila wamechukuliwa tu.Maombi yakifanyika wanauwezo wa kurudi.(ndiyo hiyo wengine huita kufufua ila kiuhalisia inakuwa hajafa shetani hana uwezo wa kuua roho ila huwa anakuchukua msukule duniani mnasema kafa)
 
Sisi tusiokumbuka ndoto tulizoota usiku tufanye je?
 
Hizi tabiri na maana zake ni za mtu mmoja maana hazibadiliki?
 
Mie huwa sipuuzi ndoto, na nikiamka tu kitu cha kwanza huwa ni kufatilia maana ya ndoto.....mara nyingi ndoto zangu ni za kweli.


Bwana weee mwaka huu niliota naokota coins.....😁😁😁 Ncheke kwanza ndoto ni ujumbe wa kweli.
 
Hizi tabiri na maana zake ni za mtu mmoja maana hazibadiliki?
zipo tofauti
Mie huwa sipuuzi ndoto, na nikiamka tu kitu cha kwanza huwa ni kufatilia maana ya ndoto.....mara nyingi ndoto zangu ni za kweli.


Bwana weee mwaka huu niliota naokota coins.....😁😁😁 Ncheke kwanza ndoto ni ujumbe wa kweli.
hongera sana kwa kutambua umuhimu wa ndoto.Mimi huwa nafuatilia hata ndoto za watoto wangu wote lazima niwaulize wanisimulie walichoota.
Na kuna ndoto nikiota au watoto wakiota inabidi nifunge ,niongeze dozi ya maombi na sadaka nizotoa ,hata watoto nimewafundisha kusali kutoa sadaka,kusoma maandiko ya Mungu.Na wakati mwingine watoto wenyewe wananiambia leo nimeota ndoto nzuri,leo nimeota ndoto mbaya nilikuwa nakimbizwa nikaomba nikamshinda,nawaelekeza cha kufanya.
 
Kwakweli huwa sipuuzii kabisa, ndo jambo la kwanza kufanya nikiamka natafuta maana ya kitu nlichoota.....
 
Nimeona hapo kuota unavalishwa nyota ukitaka iwe tamu iwe ile ya TMA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…