Tafasiri basi hiyo ndoto.
Mtu mweupe(mwenye mavazi meupe) kama theluji (Mweupe /mavazi meupe ni mtakatifu msafi asiye na dhambi kadiri wepe unavyozidi ku intensify ina maana utakatifu umezidi sana kiwangi cha uungu kuna waliomuona akin'gaa kama jua kiasi kwamba huwezi kumtazama au ukimtazama unaanguka chini kifudi fudi (sasa kiwangi cha kung'aa kikizidi kama jua anakuwa Yesu(tuseme huyo ni Yesu au malaika) ,ametokea mbinguni maana ufalme wa NURU wa mbinguni ,mbinguni wanaishi watakatifu.
2)amekupa zawadi zawadi kutoka mbinguni ambayo amekwambia unaweza kuitumia kushinda maadui ni (ROHO MTAKATIFU)inayowaka moto ni nguvu ya roho mtakatifu,ama neno la Mungu maandiko au neno la mungu pia ni ROHO (neno ni roho)na ni silaha ,ni moto ulao
ila fimbo pia inaweza ikawa ni ishara ya uongozi,(kwa scenario yako uongozi unaotakiwa ni kama uchungaji ,uinjilist kuhubiri neno)NENO la Mungu pia ni taa au torch inayomulika
totrch ya olympics sifahamu mana sifuatilii sana michezo ya kidunia tena kama olympics mingine ni ya kipagani ni ibada za kishetani huwa sifuatilii vitu vyenye asili ya giza(ila kama ina maana ya kombe au taji) hivi all in all umepewa kitu kizuri.
3)ukijumlisha na HISIA ya furaha,furaha ,amani,upendo hayo ni matunda ya ROHO MTAKATIFU moyoni ,kujazwa nguvu na kujiona umeongezdka nguvu ,naweza kusema umejazwa nguvu za Mungu au Roho mtakatifu,mana kila mtu ana roho wa Mungu ndani yake maana ufalme wa Mungu upo ndani yetu na huwa anatusemesha habari njema na kutukataza na kutuonya tuache mabaya na tukose amani ya kufanya mabaya.Ila kwa case yako wewe umehiishwa ROHO wako mtakatifu umejazwa zaidi.Na ukitaka aendelee kujaa zaidi ni kiendelea kupunguza mizigo ya dhambi uchafu moyoni ilia pate nafasi ya kujaaa na kutawala mpaka kufurika kadiri unavyopunguza dhambi uchafu moyoni unamuongezea room ya yeye kujaa na mpaka kufurika kama maji akifutumia mpaka kumwagika ndio nguvu huongezeka zaidi.
ANGALIZO
Hiyo state ni dyanamic yani Roho mtakatifu na hiyo hali ya furaha na hiyo nguvu inawezs ikaondoka kama utaendelea kufanya dhambi,na nguvu zikaisha.Ndio maana ni heri kumaliza vizuri kuliko kuanza vizuri na kumaliza vibaya.
HITIMISHO.
Shikilia sana hiyo imani yako na matendo yako mema ,ndoto hiyo uliyoota si rahisi mtu anayeishi maisha ya dhambi akaota ndoto nzuri kama hiyo.Hivyo shika sana ,linda sama moyo wako usianguke katika dhambi.Pia unaeweza ukatumia karama hiyo kusaidia wwngine mana umepewa fimbo uongozi uchunge kondoo sasa ili nao wafikie viwango vyako,hata kuombea wengine wakapona unaweza umejazwa nguvu nyingi ,hiyo karama isaidie sasa wengine isiishie kwako tu,mpango wa Mungu ni kuwaokoa watu wote na kiwaponya wengi(watu wote) sio wachache tu.