Usiri wa namna watu wanavyotajirika

Usiri wa namna watu wanavyotajirika

Izzi

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
553
Reaction score
1,144
Karibu Tanzania, nchi ambayo ukisikia mtu ametajirika basi wazo la kwanza linalokujia kichwani ni "michongo", au "unga", au "kafara", au "nyota", au "upigaji", au "sponsor" na maneno mengine ya dizaini hiyo.

Naomba mnisaidie, labda ni mimi peke yangu - lakini ni nadra sana kufikiria au kukubali kuwa ni BIDII ya mtu, au MAARIFA yake na kuzitumia fursa kihalali ndivyo vimemfanya atajirike. Swali ni kwanini?

Mimi nadhani yote hii ni kwasababu matajiri wengi Bongo ni wagumu kuelezea njia walizopita mpaka wanatajirika. Yes, huwa wanaongelea kidogo lakini wanaacha maswali mengi ambayo hayana majibu.

I mean, ukiambiwa Elon Musk ni muuza unga ndo maana ameweza kuwa tajiri namba moja duniani [emoji44] lazima ukatae: kwasababu njia alizopita mpaka alipo ziko wazi, in details. Ni rahisi kujua Jeff Bezos aliwezaje kuibadili biashara ya kuuza vitabu kuwa moja ya kampuni kubwa zaidi duniani. Ni rahisi kujua njia alizopita Dangote mpaka kuwa tajiri namba moja Africa. Ni rahisi kujua details za utajiri wa Strive Masiyiwa.

Hawa wa kwetu naona iko shida, ndio maana vijiweni kuna theory nyingi zinachekesha;

Kwamba Bakhresa alitajirika baada ya kuiona nyota ya Jaha. KwambaFred Vunjabei ni Mkinga you know [emoji6] na by default ni mchawi [emoji1745] hence utajiri wa ndere. Kwamba Mo Dewji amerithi tu utajiri wa babaake kwahiyo hakuna kikubwa alichofanya.

Kwamba Yusuph Manji ni decoy tu wa matajiri wa ughaibuni huko. Kwamba Joseph Kusaga amewanyonya sana wasanii kufika hapo alipo - kupitia jasiri muongoza njia. Kwamba huyo tajiri wa mtaani kwenu alimtoa kafara naniliu, mara paap akawa don. Kwamba yule mwingine alichukua nyota ya mwenzake ndiyo inamfanya aendelee kupiga mpunga mrefu, so mwenye nyota yake akiirudisha, mchizi chali![emoji6]

Na hizi theories zinasambaa na kuaminika kwasababu hakuna alternatives. Angalau Fred Vunjabei aliwahi kuongelea namna alivyofika alipofika na ika-make sense, vijiweni masela wakaelewa, wakaanza kuona kumbe mwana sio Mkinga Mchawi bali ni hustler [emoji1].

Madhara ya hii "mindset" ya kuamini huwezi kutajirika bila kuuza unga, au kupiga michongo, au kuwa mpigaji au kuwa na sponsor, au kuingia kwenye siasa na kula pesa za umma, au kutoa kafara n.k. ni makubwa sana. Yanafanya watu hawataki kujituma, bali wako standby kutafuta hizi shortcuts. Na huwezi kuwashauri vinginevyo, watakuuliza ni nani aliyetajirika bila shortcuts?[emoji848]

Hivi juzi juzi ndugu yetu wa damu kabisa, Benji, amefanikiwa kunasa kibunda cha Dola milioni 10! Utasikia tu mitaani theory za watu kuhusu namna alivyofanikiwa kuzipata hizo. Na I bet zitaanzia mtaa wa 'Silicon Dar'[emoji1787][emoji1787][emoji1787] (Am joking!)

BOTTOM LINE.
I wish wanaofanikiwa wangekuwa wako wazi zaidi juu ya njia walizopita mpaka kufika walipofika. Kutusimulia kwamba "Nilianza kuuza karanga, baadae nikafungua duka na saivi ninamiliki supermarket", haitoshi. Simulizi za hivyo zinaacha maswali mengi mno! Matokeo yake, mitaani watu tunakosa real models, na hatuwezi kuwatumia real models wa ughaibuni kwasababu mazingira ni tofauti sana kwa kila namna.

I stand to be corrected. Naomba kuwasilisha.

PS: CASE STUDIES
Hadija Jabiry
Reginald Mengi
Elon Musk
Aliko Dangote
 
Role models. Sasa wewe mwenyewe hapo umeanza kukataa ushuhuda wa mtu alieanza kuuza karanga hadi kafungua supermarket.

Utajiri ni Siri vinginevyo kila mtu angekuwa tajiri.
 
Mifumo ya Tanzania sio rafiki kuupata utajiri bila mapicha mapicha... ukinyooka hutoboi..

Huyo fred Vunja bei uliyemtaja, story yake ina matobo matobo kibao...na hapo ndio shida ilipo...ukianza kupiga story za kutajilikia china kama ni wakiume lazima wakulungwa wakuhusishe na poda na kama mdada basi itakuwa kudanga tu.... hakuna tajiri anayeweza kukwambia alikwenda kwa mganga au anakwepaga kodi nk..

Hata mabinti wengi wanaodanga uturuki, Nigeria, China, Malyasia, India nk watakwambie wanapiga mishemishe ila ukikanyaga hayo maeneo utaelewa hizo mishemishe...
 
Role models....sasa wewe mwenyewe hapo umeanza kukataa ushuhuda wa mtu alieanza kuuza karanga hadi kafungua supermarket. Utajiri ni Siri vinginevyo kila mtu angekuwa tajiri.
Ushuhuda una ukakasi, ndio maana nina doubts. Kwamba utajiri ni siri - hapo ndipo hoja yangu ilipo; mbona matajiri wa ughaibuni ni wepesi kueleza details za utajiri wao na bado hatuwezi kuwafikia? [emoji848][emoji848][emoji848] huku kwetu hizo siri ni siri gani?
 
Akuelezee wewe nani? Ni lazima waeleze jinsi walivyopata utajiri wao? Hata wakieleza hamuwezi kuamini kwasababu mshajiaminisha kama ulivyoelezea. Kila mtu ashinde mechi zake.
 
Huku mtaaan kwetu tajiri mmojai malori yake yanawaka Moto kimazabe Tu, yalikuwa km 40 sasa hivi amebaikiwa na mawili Tu tena mikweche..wazee wa za ndaaani kabisa wanakuambia alichagua utajiri wa kuku kudonoa mahind..punje moja mwaka mmojai,sasa naona idadi ya mahindi imekamilika wazee wanarudisha Mali zao.Ndy maana jamaa amefirisika

Alisikika jobles mmoja hivi.Yuponkwenye Kochi la shemeji huku anasikitika kuanzia Leo TV inawaka Kwa kuvizia vizia coz kuna mgao wa umeme na Hana pa kwenda!!
 
Akuelezee wewe nani? Ni lazima waeleze jinsi walivyopata utajiri wao? Hata wakieleza hamuwezi kuamini kwasababu mshajiaminisha kama ulivyoelezea. Kila mtu ashinde mechi zake.
I can feel your attitude bro! [emoji16][emoji16][emoji16][emoji119][emoji119][emoji119] Mimi ninashukuru kwa hoja yako. Ngoja nisikie mitazamo mingine.
 
Huku mtaaan kwetu tajiri mmojai malori yake yanawaka Moto kimazabe Tu, yalikuwa km 40 sasa hivi amebaikiwa na mawili Tu tena mikweche..wazee wa za ndaaani kabisa wanakuambia alichagua utajiri wa kuku kudonoa mahind..punje moja mwaka mmojai,sasa naona idadi ya mahindi imekamilika wazee wanarudisha Mali zao.Ndy maana jamaa amefirisika

Alisikika jobles mmoja hivi.Yuponkwenye Kochi la shemeji huku anasikitika kuanzia Leo TV inawaka Kwa kuvizia vizia coz kuna mgao wa umeme na Hana pa kwenda!!
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] kuna watu tuna-relate! Hapo unajaribu kumhakikishia babe kwamba mzee baba unapambana, sema mafanikio sio rahisi kama anavyofikiria [emoji23][emoji23][emoji23].
 
Mifumo ya Tanzania sio rafiki kuupata utajiri bila mapicha mapicha... ukinyooka hutoboi..

Huyo fred Vunja bei uliyemtaja, story yake ina matobo matobo kibao...na hapo ndio shida ilipo...ukianza kupiga story za kutajilikia china kama ni wakiume lazima wakulungwa wakuhusishe na poda na kama mdada basi itakuwa kudanga tu.... hakuna tajiri anayeweza kukwambia alikwenda kwa mganga au anakwepaga kodi nk..

Hata mabinti wengi wanaodanga uturuki, Nigeria, China, Malyasia, India nk watakwambie wanapiga mishemishe ila ukikanyaga hayo maeneo utaelewa hizo mishemishe...
Dizaini inakatisha tamaa eh? Unajaribu kupambana lakini kila ukikumbuka "Mifumo" na uhalisia... pumzi inakata [emoji848][emoji848][emoji848]
 
mapichapicha, shida kila Tajiri anamapicha mapicha akianza kukuelezea ameupataje utajiri inakuwa kama report ya jeshi la polisi dhidi ya yule askari aliyejinyongea mahabusu...
Nchi ya masinema [emoji38][emoji38][emoji38]
 
mtu akisha andika kiswaenglish huwa sielewi nasoma nini
 
mtu akisha andika kiswaenglish huwa sielewi nasoma nini
Nakuelewa sana [emoji38][emoji38][emoji38] niwie radhi, waneni walisema mazoea mabaya.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] kuna watu tuna-relate! Hapo unajaribu kumhakikishia babe kwamba mzee baba unapambana, sema mafanikio sio rahisi kama anavyofikiria [emoji23][emoji23][emoji23].
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tanzania hakuna uwazi, na hii inatokana na watu kuogopa kuigwa, vichwa vya hii nchi vimejaa copy and paste thuswhy mtu anaona bora abaki na siri yake
Hoja yako ina mantiki sana, yaani watu wanajua kucopy na kupaste sana, ukiwa na kitu ndo kinakupa ulaji ukiwaelezea watu hawatabuni zaidi ili kukupa changamoto bali wanakichukua Kama kilivyo ndo hiyo inawaangusha watu wengi.
 
Ndo hivyo ndugu Nchi hii ina watu wa hovyo sana
 
Back
Top Bottom