Usiri wa namna watu wanavyotajirika

Utajiri ni mchakato pia kila mmoja ana njia zake pili utajiri ni hobbies na sio KILA mtu anatamani kuwa tajiri
 
"Behind every great fortune,there is crime"...sijui kama niko sawa kwenye hako kasentensi, niliwahi kukasoma pahala

Mimi kama mimi naamini:-

Kuna utajiri wa bahati ( Mtu kuwa na bahati yake katika biashara au shughuli aifanyayo

Kuna utajiri wa juhudi na bidii katika kazi aifanyayo mtu,

Pia kuna utajiri wa dawa (kafara)

Kama njia mbili za juu hujafanikiwa njia ya tatu ndio kimbilio la wengi
 
Nilifanya kazi ya saidia nikapata teni nikauza karanga nikapata laki nikafunga mgahawa nikapata milioni nikafungaa duka nikapata milion kumi nikaingia shamba nikapata milion 30[emoji23][emoji23] fanya ww sasa,,,,,. kumbe mnachosahau watz ni mambo haya,muda, uvumilivu wa kurudia jambo hata kama likifeli, na imani hususan matambiko nk haya tu hamuambiwi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni choyo tu. Anaefika juu hataki na wengine wafike. Ya waganga sio siri, kila mmoja anayaelewa. Ila ya ukweli wanayaficha.
 
mapichapicha, shida kila Tajiri anamapicha mapicha akianza kukuelezea ameupataje utajiri inakuwa kama report ya jeshi la polisi dhidi ya yule askari aliyejinyongea mahabusu...
Kwa upande wangu huwa sioni kama Kuna Siri ya utajiri zaidi ya Kupiga kazi kwa nguvu na moyo. Nikiwa mdogo niliishi na ndugu yangu ambaye kwa Sasa ni bilionea. Huyu alikuwa anaenda kazini "porini" anakaa wiki 2 au 3 bila kurudi home, ofisi anamwachia secretary. Ni mtu wa kujituma haswaa, muda wowote kazi. Lakini history yake ya utafutaji inaanzia kuajiriwa, akaacha kazi Sababu ya mazingira then akaingia kwenye uchuuzi "machinga" wa sigara, nguo .......

Kwa Nini watu hamuamini njia alizopitia mtu?
Ni kwa sababu "no body can have the same feelings just like you". Nikikwambia Jana nimelala njaa, huwezi ku feel maumivu/stress/anxiety kama nilivyokuwa nayo Mimi wakati naenda kulala na njaa.
Ndivyo hivyohivyo mtu akikuhadithia alivyokuwa ananyeshewa mvua akikusanya mbao Kijijini Cha Igoda na kuzileta mjini kuuza mpaka akafikisha mtaji wa m200 huwezi kufeel the same. Ukisimuliwa ya Wakinga kuingia hifadhi ya Ruaha kuvua kambale wanaishi huko miaka 3 bila kurudi nyumbani wanatoka huko na mtaji wa m100 huwezi amini.
So do your things, shinda mechi zako.
 
Ni mpumbavu peke yake yake ambae hajui hisyoria ya manji anaweza kusema n decoy,manji baba yake amekuwa mjenga mabodi ya mabasi kwa miaka mingi sana,manji karithi tu

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Akuelezee wewe nani? Ni lazima waeleze jinsi walivyopata utajiri wao? Hata wakieleza hamuwezi kuamini kwasababu mshajiaminisha kama ulivyoelezea. Kila mtu ashinde mechi zake.
Mkuu hiyo ndiyo point,uwaambie watu njia ulizofanikiwa kwa mantiki ipi? sana sana labda mwenye shida ya kujua umefanikiwa vip atakufuata yey mwenyew na wew utamuelekeza ila suala la kuamin au kutokuamin yale uliyopitia had ukafanikiwa ni juu yake..
 

Ulimwengu unaoonekana unaongozwa na ulimwengu usioonekana.
 
Kuna siku nilikaa na jamaa mmoja mmiliki wa mabus ya kwenda Mikoani nikajaribu kumdadisi juu ya utajiri kwa ujumla, majibu yake yalikuwa kama ifuatavyo, "mdogo wangu mtu akiwa anakusimulia kuhusu njia alizopitia au mambo aliyofanya mpaka kuwa tajiri, kama una akili timamu utagundua kuna vitu/points anaruka(hakwambii) siku ukifanikiwa kujua ni vitu gani hajakwambia huo ndio utajiri halisi". Mwisho wa kunukuu.
 
Matajiri wa tz: mpaka anapata mafanikio yenyewe hajui kufanikiwa vipi sasa sijui unataka akuelekeze kitu gani zaidi ya kukuambia aliuza vitumbua na kingine msichokijua tz ukisha kuwa na jina na kampuni kubwa basi unakuwa kichaka cha wanasiasa kuwekeza kwako, hilo nina ushahidi nalo, mzee wangu alifutwa na watu aina hiyo hivii hamjiulizi kwann kila awamu za marais lazima aibuke tajir mpya?? Sasa watu kama hao ata kusimulia nn kuhusu utajiri wake ikiwa nyuma yake anajua kina nani wapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Enheee!! Hivi vitu wanavyoruka ndo kuvipata sasa... mtiti!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…