raraa reree
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 11,504
- 35,520
kaka kama utajiri ni siri kwanini iwe siri huku kwetu africa lakini wenzetu wanaweka mambo wazi ?Role models. Sasa wewe mwenyewe hapo umeanza kukataa ushuhuda wa mtu alieanza kuuza karanga hadi kafungua supermarket.
Utajiri ni Siri vinginevyo kila mtu angekuwa tajiri.
Baada ya kusoma point yako, nikamkumbuka Yesu wa Nazareth aliposema,"Ni rahisi ngamia kupenya kwenye tundu la sindano, kuliko tajiri kuurithi ufalme wa mbinguni."Haiwezekani kuelezea kila kitu ulichopitia kwa sababu at some point unapitia a grey line ambayo wengine watakuona mbaya na wengine hawana shida nayo.
Kiuhalisia, kuwa tajiri kunatokana na kutengeneza unfair advantage na kukutana na bahati. Hao wote uliowataja katika sehemu flani ya maisha yao walimpindua mtu (angalia historia ya Musk na Tesla), waliua biashara za watu kwa makusudi (angalia historia ya Bezos) au walipata kitu kikubwa kwa gharama ndogo na kuishia kupata faida kubwa kutoka hapo (angalia historia ya Dewji). Ukielezwa mambo waliyofanya kutakuwa na ukakasi hivyo inakuwa bora tu uwalishe watu kuwa kufanya kazi kwa bidii inatosha.
Hamna njia ya moja kwa moja kupata utajiri kwa 100% wema. Ni jambo ambalo inabidi tukubaliane labda kama ushinde lottery. Hivyo kama lengo ni kuupata utajiri tambua kuwa itafika point katika maisha yako ambayo itabidi uchague utoboe au uendelee na wema wako.
Si lazima kila mtu akamuulize. The point is, huwa wanapata fursa za kuelezea kwa nyakati tofauti tofauti. Katika nyakati zote hizo ukiwasikiliza, unabaki na maswali mengi kuliko majibu. That's the point.Kwani ni tajiri gani ulimuuliza alikataa kukuelezea? Unataka wakalipie kipindi redioni kujieleza amepataje utajiri?
Siyo Ile ya kupotea Mo kweli ikihusisha SISI-TVmapichapicha, shida kila Tajiri anamapicha mapicha akianza kukuelezea ameupataje utajiri inakuwa kama report ya jeshi la polisi dhidi ya yule askari aliyejinyongea mahabusu...
Nani kaweka wazi?kaka kama utajiri ni siri kwanini iwe siri huku kwetu africa lakini wenzetu wanaweka mambo wazi ?
Mr. Azma, mifumo inayotumika kuendesha biashara Nchi hii siyo Imara. Ni dhaifu sana. Ukitaka ku-prove hili anzisha biashara. Utashuhudia. Kwa mifumo hii mibovu tunashuhudia biashara nyingi nchini, takribani 85%, huporomoka na kufilisika muda mfupi baada ya kuanzishwa. Ni msiba.Karibu Tanzania, nchi ambayo ukisikia mtu ametajirika basi wazo la kwanza linalokujia kichwani ni "michongo", au "unga", au "kafara", au "nyota", au "upigaji", au "sponsor" na maneno mengine ya dizaini hiyo.
Naomba mnisaidie, labda ni mimi peke yangu - lakini ni nadra sana kufikiria au kukubali kuwa ni BIDII ya mtu, au MAARIFA yake na kuzitumia fursa kihalali ndivyo vimemfanya atajirike. Swali ni kwanini?
Mimi nadhani yote hii ni kwasababu matajiri wengi Bongo ni wagumu kuelezea njia walizopita mpaka wanatajirika. Yes, huwa wanaongelea kidogo lakini wanaacha maswali mengi ambayo hayana majibu.
I mean, ukiambiwa Elon Musk ni muuza unga ndo maana ameweza kuwa tajiri namba moja duniani [emoji44] lazima ukatae: kwasababu njia alizopita mpaka alipo ziko wazi, in details. Ni rahisi kujua Jeff Bezos aliwezaje kuibadili biashara ya kuuza vitabu kuwa moja ya kampuni kubwa zaidi duniani. Ni rahisi kujua njia alizopita Dangote mpaka kuwa tajiri namba moja Africa. Ni rahisi kujua details za utajiri wa Strive Masiyiwa.
Hawa wa kwetu naona iko shida, ndio maana vijiweni kuna theory nyingi zinachekesha;
Kwamba Bakhresa alitajirika baada ya kuiona nyota ya Jaha. KwambaFred Vunjabei ni Mkinga you know [emoji6] na by default ni mchawi [emoji1745] hence utajiri wa ndere. Kwamba Mo Dewji amerithi tu utajiri wa babaake kwahiyo hakuna kikubwa alichofanya.
Kwamba Yusuph Manji ni decoy tu wa matajiri wa ughaibuni huko. Kwamba Joseph Kusaga amewanyonya sana wasanii kufika hapo alipo - kupitia jasiri muongoza njia. Kwamba huyo tajiri wa mtaani kwenu alimtoa kafara naniliu, mara paap akawa don. Kwamba yule mwingine alichukua nyota ya mwenzake ndiyo inamfanya aendelee kupiga mpunga mrefu, so mwenye nyota yake akiirudisha, mchizi chali![emoji6]
Na hizi theories zinasambaa na kuaminika kwasababu hakuna alternatives. Angalau Fred Vunjabei aliwahi kuongelea namna alivyofika alipofika na ika-make sense, vijiweni masela wakaelewa, wakaanza kuona kumbe mwana sio Mkinga Mchawi bali ni hustler [emoji1].
Madhara ya hii "mindset" ya kuamini huwezi kutajirika bila kuuza unga, au kupiga michongo, au kuwa mpigaji au kuwa na sponsor, au kuingia kwenye siasa na kula pesa za umma, au kutoa kafara n.k. ni makubwa sana. Yanafanya watu hawataki kujituma, bali wako standby kutafuta hizi shortcuts. Na huwezi kuwashauri vinginevyo, watakuuliza ni nani aliyetajirika bila shortcuts?[emoji848]
Hivi juzi juzi ndugu yetu wa damu kabisa, Benji, amefanikiwa kunasa kibunda cha Dola milioni 10! Utasikia tu mitaani theory za watu kuhusu namna alivyofanikiwa kuzipata hizo. Na I bet zitaanzia mtaa wa 'Silicon Dar'[emoji1787][emoji1787][emoji1787] (Am joking!)
BOTTOM LINE.
I wish wanaofanikiwa wangekuwa wako wazi zaidi juu ya njia walizopita mpaka kufika walipofika. Kutusimulia kwamba "Nilianza kuuza karanga, baadae nikafungua duka na saivi ninamiliki supermarket", haitoshi. Simulizi za hivyo zinaacha maswali mengi mno! Matokeo yake, mitaani watu tunakosa real models, na hatuwezi kuwatumia real models wa ughaibuni kwasababu mazingira ni tofauti sana kwa kila namna.
I stand to be corrected. Naomba kuwasilisha.
Tax Avoidance vs Tax EvasionBaada ya kusoma point yako, nikamkumbuka Yesu wa Nazareth aliposema,"Ni rahisi ngamia kupenya kwenye tundu la sindano, kuliko tajiri kuurithi ufalme wa mbinguni."
Ina-make sense.[emoji848]
Lakini akina Jeff, Mark Zuck, Musk n.k. huwa wanaweka wazi hata hizo rafu walizozicheza. Meaning that kama na wdwe unaweza - cheza tuone.
Mfano kuna mwaka Jeff alilipa kodi 0$ (Sifuri) na kwa nchi kama Marekani kukwepa kodi ni kisanga. Lakini it was an open secret kwamba jamaa alicheza na sheria za kodi kiasi ambacho ilionekana ni sahihi kwake kulipa sifuri. Magumashi ya kisomi.
mtoa mada azma amewataja matajiri wakizungu na story zao zipo wazi jinsi walivyopata utajiri wao, sasa iweje huku kwetu useme utajiri ni siri ?Nani kaweka wazi?
Hatari kabisa. Matajiri wengi Wakinga wana hiyo hulka... habadilishi mavazi, utamdharau mpaka siku ukimuona analipia Scania showroom... cash! Hatari kabisa.Matajiri wengi wanamakandokando mengi sna aisee na lzm uwe na roho ngumu na roho mbaya na mbanifu was Hali ya juu
Taijri afuji pesa kijinga jinga ila ss tukipata kidg tu lzm wahudumu wajue kuwa unazo ...
Kuna jamaa nilikuwa namchukulia POA POA tu kumbe anazo scania nne aise Tena mende za maana na Wala uwez juwa unaweza sema labd Ni dereva kumbe Ni zake nilikuja siku kujuwa nilpo mkuta garage tukaongea ndio akimbia kuw ananiona na mm na magari nikamuambia siyo zangu Ni jamaa fln namsimamia tu
Nakuelewa sana mkuu. Kwenye suala la mifumo hapo, ni msiba.Mr. Azma, mifumo inayotumika kuendesha biashara Nchi hii siyo Imara. Ni dhaifu sana. Ukitaka ku-prove hili anzisha biashara. Utashuhudia. Kwa mifumo hii mibovu tunashuhudia biashara nyingi nchini, takribani 85%, huporomoka na kufilisika muda mfupi baada ya kuanzishwa. Ni msiba.
Sasa, hali hii husababisha Wafanyabiashara kutumia mbinu mbalimbali ili kulinda biashara zao, ikiwemo, kukwepa kodi, wizi, kudhuru mu, kutumia nguvu za giza, na kadhalika.
Kama wa Dr.ShikaHebu mnitoe tongotongo kidogo, utajiri unaanzia bei gani...........ili nirudi kuchangia vizuri.