Ertugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 14,705
- 30,041
Nimeamua kuandika uzi huu kutokana na yale ambayo yananisikitisha sana nionayo katika jamii yetu
Huwa tunapenda kushindana na watu katika maisha yetu bila kujua kwamba mwisho wa siku tunajiumiza wenyewe na kuathirika sisi wenyewe.
Katu hata siku moja wanadamu hatuwezi kuwa sawa,ridhika na majaliwa yako uliyojaaliwa na Allah,kinyume chake utatumia nguvu kubwa kuwaminisha watu kwamba wewe ni mambo safi kumbe kapuku tu
Shindana na wewe wa jana,shindana na wewe ambaye ulikuwa na husuda na sasa umeamua kuacha husuda,shindana na wewe ambaye hapo awali ulikuwa hujiamini ila sasa hivi unajiamini.
Shindana na wewe ambaye jana ulikuwa mlevi na Malaya na sasa umeamua kuacha tabia hizo zenye kutia aibu katika jamii yako
Shindana na tabia au jambo lolote ambalo lilikuwa kikwazo kwako kufikia pale unapotaka kufika na shindana na pambana uvuke kwenda upande wa pili ambapo unatamani kuwa
Kuna dada mmoja wallah ukiona status zake ni kupika vyakula vizur vizur lakini kiuhalisia kumbe hutumiwa na rafiki ambaye ni mambo safi,halafu kisha yeye hutamba navyo kwenye mitandao,kama sio utaahira ni nini?
Je anapata nini kuwaonyesha watu mambo ambayo hana,je siku asipotumiwa hizo picha ambazo hutamba nazo kuwaonyesha watu kuwa yupo vizuri itakuwaje?
Be your self and don't compete with any one except your self, jiamini na jikubali kwa hali yoyote utakayo kuwa nayo,huko ndiko kujitambua
Ni hayo tu!