Usitegemee nguvu zako pekee kuna mambo ili ufanikiwa una hitaji neema ya Mungu

Usitegemee nguvu zako pekee kuna mambo ili ufanikiwa una hitaji neema ya Mungu

Wakusolve

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2020
Posts
561
Reaction score
997
Luka 5:5
Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu.

Luka 5:6
Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika;

Hii inafundisha nini, petro na wenzake walijituma sana kupitia nguvu zao kuvua samaki lakini awaku ambulia kitu,

alipofika yesu kristo na kuwambia washushe nyavu ndipo wakavua samaki wengi sana hii ina maana muda mwengine neema ndio itakayokufanya ufanikiwe sio juhudi zako pekee.

Katika maisha unaweza kuwa na akili nyingi, maarifa lakini ukikosa neema ya Mungu basi akili zako zinaweza zisikusaidie.

Hivyo usitegemee akili na nguvu zako mpe Mungu nafasi kwenye hicho unachokifanya ili upate neema ya Mungu, neema ya Mungu ndio italeta watu wakuamini kwenye hicho unachokifanya.

Petro na wavuvi wenzake walipata samaki wengi sababu ya neema ya Mungu.

Neema ya Mungu ndio inafungua milango ambayo kwa nguvu zako na akili zako usingeweza kufanikiwa kuifungua.
 
Back
Top Bottom