Usitengeneze kawaida dari la nyumba yako, karibu tukupendezeshee

Usitengeneze kawaida dari la nyumba yako, karibu tukupendezeshee

IMG-20240207-WA0008.jpg
 
Attachments

  • Screenshot_20240207-213914.jpg
    Screenshot_20240207-213914.jpg
    52.6 KB · Views: 7
Nina changamoto ya paa fupi mnafanyaje Ili kubaki na nafasi
 
Nina changamoto ya paa fupi mnafanyaje Ili kubaki na nafasi
Mita ngapi?

Maana huwa tunashusha cm 15 tu kutoka juu. Nyumba nyingi huwa zina kimo cha cm 350.
 
Aisee sijui mm ni ushamba kitu chochote kikishakuwa na makorokoro mengi huwa nakikinahi fasta...... so na prefer zaidi simple kwa kila kitu katika maisha yangu!!
Agree yaani sebule maurembo kibao mpaka inatisha, we weka gypsum yako flat white shushia taa ya milioni mbili zile za urembo! Ukutani kuwe flat piga rangi nyeupe madirisha makubwa tia pazia za bei mbaya! Sebuleni tia kochi isiyo na makorokoro na meza ya mbao kali! Sehemu ya tv usiweke makorokoro tia ukutani tv ya inch 60 chini show case isiyo na mambo mengi. Katikati ya sebule tia zulia la bei mbaya!!! Sio hayo mapicha picha hata usafi unakua shida.
 
😅 Tunatofautiana katika kupenda vitu. Ndio maana mwingine anajenga ghorofa. Mwingine ñyumba ya chini.

Wewe unataka tv nchi 65 mwingine atakwambia yote hiyo ya nini me nataka nchi 43 tu inatosha.
 
Hii imekaa unyama.
gharama ni sh? kwa sebule 4m x 5m na dining 4m x 4m
Gypsum board = pc 20 @ 20000
Angles channel = pc 60 @ 4000
Screw = box 6 @ 7000
Labour charge 400,000

Jumla 1082000

Inabaki kazi ya finishing tu. Skiming na rangi.
 
Back
Top Bottom