Usitoe mahari, epuka mila potofu

Sawa nimekuelewa Mkuu,ni sawa tu vyovyote tukichukuliwa,ila mahari inawapasa mtoe
 
Hii ni hatari sana

Mwanaume lipa mahali upate heshima kote kote lingana na uwezo wako
 
Kwa upande wa mahari ni hapana.
Hapa Tanzania na nchi zingine wapo mamilioni ya Watu wanaishi kama mke na mume na hawajatoa mahari.
Kama umenisoma ukanielewa,umri wako leo mwenye mawazo haya kama umeokota binti wa watu huko ukakokotana nae kwenu bure ukasema ni mkeo kuna umri unakuja utajiona mjinga kwa ulichokifanya.

Au kamuulize baba yako kama dada zako hakuwaoza kwa mahari?yeye kwanini hakuwagawa bure dada zako utajua namaanisha nini.
 

Kitu chochote kinachonunulika linafanana na bidhaa. Na thamani yake inapimika.
Mtu hanunuliwi.

Hapo mwisho nashukuru umesema wazi kuwa mke ni bidhaa bora kwa matumizi.
Lakini kwetu mke ni mtu na kamwe hanunuliwi wala kununulika.
 

Kwetu hatutoi mahari wala kupokea.

Zipo jamii nyingi hazitoi mahari hasa jamii za ulimwengu wa kwanza. Kwa hiyo hizo jamii nazo zikifika umri wa utu uzima zinajiona wajinga?

Embu kuweni serious Wakuu
 
Sawa nimekuelewa Mkuu,ni sawa tu vyovyote tukichukuliwa,ila mahari inawapasa mtoe

Kwa Watu waliogizani ni sawa kabisa kama ulivyosema. Ila kwa walionuruni huko tumetoka.

Hata zamani Wanawake wenzako walijivunia kufanyiwa tohara (kukeketwa) waliokuwa na mawazo tofauti kama sisi walionekana wajinga lakini mpaka muda huu ukweli umebainika kuwa nani alikuwa mjinga.

Sasa miaka 100 ijayo itafahamika kutoa mahari ni upuuzi au ni haki.

Huwezi mnunua mtu kwa visingizio vya kijinga, ati sijui heshima ya mwanaume, sijui kujua mwanaume anauwezo wa kuhudumia au kaa. Yaani sababu za bara la giza ni za kitoto sana
 
Sawa Mkuu
 
Huyu dogo ni mgonjwa wa akili asiyejielewa
 
Kwetu hatutoi mahari wala kupokea.

Zipo jamii nyingi hazitoi mahari hasa jamii za ulimwengu wa kwanza. Kwa hiyo hizo jamii nazo zikifika umri wa utu uzima zinajiona wajinga?

Embu kuweni serious Wakuu
As long as hatufahamiani kwamba utaweza kunithibitishia hilo na sizijui mila za kwenu tuhitimishe kwa kusema ninyi ni jamii ya kipekee.

Na kila jamii ina taratibu zake huwezi kuhamisha taratibu zenu kwa wasiohusika acha wale wenye tamaduni hizo wafanye ninyi bakini na tamaduni zenu.
 
Hili jambo inabidi liishe. Mila za kijinga inabidi zikomeshwe.
 

Hakuna cha mila wala nini.
Hizo mila zingekuwepo kusingekuwa na Ukristo na uislamu katika hizo jamii mnazoziita zinamila.

Mbona siku hizi hamkeketi na wakati ilikuwa mila?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…