Mahari inalipwa Toka enzi...
Biblia imeandika Mwanzo 34:12
Niambieni kiasi cha mahari na zawadi nitakayoleta, hata iwe kubwa kiasi gani nitawalipa chochote mtakachonidai.
Nipeni tu huyu msichana awe mke wangu.
Usiokote vifungu binti kuhalarisha uuzwaji wa binadamu.
NAKUPA SHORT STORY YA MAANDIKO ULIYOTOA
Shekemu mtoto wa Hamori alimbikiri mtoto wa Yakobo aitwaye Dina kabla hajamuoa.
Ndugu zake Dina wakakasirika sana.
Hamori baba ake Shekemu akanena na ndugu zake Dina mtoto wa Yakobo akiwambia mwanae amempenda ndugu yao.
Basi Hamori akatoa ofa ambayo imekaa kama deal (mapatano ya kidunia)
Deal lenyewe
Mwanzo 34:9
Mkaoane na sisi, mtupe sisi binti zenu, nanyi mkatwae binti zetu.
Msitari wa 10
Nanyi mtakaa nasi na nchi hii itakuwa mbele yenu, kaeni na kufanya biashara humo, mkapate mali humo.
Msitari wa 11
Shekemu akamwambia babaye yule msichana na nduguze, Na nikubalike machoni penu na mtakavyoniambia nitatoa.
12
Mjapoongeza sana mahari na zawadi, nitatoa kadri ya mtakavyoniambia, lakini mnipe huyu msichana, awe mkewangu.
Soma vizuri hapo utaona ni utamaduni wa hiyo jamii nasio miongozo ya Mungu kutoa mahari.