Usitoe mahari, epuka mila potofu

Usitoe mahari, epuka mila potofu

Kwema Wakuu!

Nasisitiza, vijana kama ulikuwa ni mpango wako kutoa kuoa mwaka huu kwa kutoa mahari. Sitisha! Usitoe mahari. Ila ni vizuri kwenda kujitambulisha kwao na kwenu.
Kama kuna uwezekano fanyeni sherehe ndogo kulingana na uwezo wenu.

Kamwe Usitoe mahari.
Mahari ni kununua binadamu ambaye ni mnyama. Mtu kamwe hanunuliwi.
Mahari ni kununua mtu , hivi hii definition imeandikwa wapi?
 
Mahari inalipwa Toka enzi...

Biblia imeandika Mwanzo 34:12
Niambieni kiasi cha mahari na zawadi nitakayoleta, hata iwe kubwa kiasi gani nitawalipa chochote mtakachonidai.
Nipeni tu huyu msichana awe mke wangu.
Usiokote vifungu binti kuhalarisha uuzwaji wa binadamu.

NAKUPA SHORT STORY YA MAANDIKO ULIYOTOA
Shekemu mtoto wa Hamori alimbikiri mtoto wa Yakobo aitwaye Dina kabla hajamuoa.

Ndugu zake Dina wakakasirika sana.

Hamori baba ake Shekemu akanena na ndugu zake Dina mtoto wa Yakobo akiwambia mwanae amempenda ndugu yao.

Basi Hamori akatoa ofa ambayo imekaa kama deal (mapatano ya kidunia)

Deal lenyewe
Mwanzo 34:9
Mkaoane na sisi, mtupe sisi binti zenu, nanyi mkatwae binti zetu.

Msitari wa 10
Nanyi mtakaa nasi na nchi hii itakuwa mbele yenu, kaeni na kufanya biashara humo, mkapate mali humo.

Msitari wa 11
Shekemu akamwambia babaye yule msichana na nduguze, Na nikubalike machoni penu na mtakavyoniambia nitatoa.

12
Mjapoongeza sana mahari na zawadi, nitatoa kadri ya mtakavyoniambia, lakini mnipe huyu msichana, awe mkewangu.

Soma vizuri hapo utaona ni utamaduni wa hiyo jamii nasio miongozo ya Mungu kutoa mahari.
 
Africa ni Bara pekee masikini ambalo linachezea pesa kwa matumizi ya KIPUMBAVU kama mahari, sherehe za kipuuzi, n.k

Bibi yangu mwenye miaka takribani 103 alipata kunambia Haya

Miaka ya nyuma Mwanamke alikuwa kijakazi, alikuwa anaolewa kwenda kufanya kazi kama kilimo, ufugaji pamoja na kuzaa (huku kuzaa sio vitoto viwili kama njiwa). Yeye pamoja na watoto wake ni mali ya ukweni.

Kuthibitisha hilo, ilikuwa ni aibu na hasara kubwa mwanamke uliyemtolea mahari akashindwa kufanya kazi kama kilimo au kutozaa.

Kwahiyo walitoza mahari Kwasababu mwanamke alikuwa kijakazi. Na hili zoezi lilifanyika kibabe, wazee wakikubaliana Binti ataenda kuolewa na mtu ambae amemuona kwa mara ya kwanza siku ya kutoa mahari, awe anataka ama hataki ataolewa. HAPA NAHITIMISHA KWA KUSEMA HUU ULIKUWA NI UTUMWA NA UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU ambao sisi tumeubeba na kuendelea kuutukuza.

TUACHANE NA BIBI YANGU,
JE MWANAMKE LEO NI KIJAKAZI???
YUKO TAYARI KUWA KIJAKAZI ???

Ewe mwanamke wa sasa unaeshabikia utumwa uliobatizwa jina la Mahari, kataa huo ujinga unakwenda kuuza utu wako.

Hebu tizama,
Kijana aliyetoa ving'ombe vitatu kwenu anakumiliki ukiwa hai na hata maiti yako anaimiliki.

Ukifa yeye ndo mwenye mamlaka ya kuamua akuzike wapi na akuzikeje, eti yule mama aliyekuweka tumboni miezi9 hana sauti mbele ya mtu aliyekutolea ving'ombe vitatu. Upuuzi wa kiwango cha juu cha mwisho.
 
Huwezi na hautokaa kamwee kuelewa maana ya Mahari .

Kwa sababu Bichwa lako umelijaza ushetani .

Siku hizi wanaume Mnaopumuliwa mko mbele kabisa kupinga Ndoa.
 
Kanda ya ziwa ndio inaongoza kwa kuwatesa wanawake ndani ya ndoa
Hii ni kwasababu mwanamke ananunuliwa kwa mahari kubwa.
Pwani wanawake hawateswi kivile, na mahari yake iko chini
 
Kwema Wakuu!

Nasisitiza, vijana kama ulikuwa ni mpango wako kutoa kuoa mwaka huu kwa kutoa mahari. Sitisha! Usitoe mahari. Ila ni vizuri kwenda kujitambulisha kwao na kwenu.
Kama kuna uwezekano fanyeni sherehe ndogo kulingana na uwezo wenu.

Kamwe Usitoe mahari.
Mahari ni kununua binadamu ambaye ni mnyama. Mtu kamwe hanunuliwi.
Kifupi ulofa ndio unakusumbua tafuta Hela wewe

Hizi lugha za kimaskini zitaondoka kinywani mwako.
Umaskini ndio unafanya mtu kuwa na vimisimamo vya ajabu kama vyako
Hili andiko lako linaonyesha wazi wewe lofa shilingi inakupiga chenga sana
 
Ongeza hapo na ni attention seeker,baba'ake mwenyewe mkewe ambaye ni mama yake hakupewa bure lakini leo kinda lake linalia lia hapa habari za mahari.

Ujinga mtupu.

Tutawatoa gizani tuu kama sio ninyi basi watoto wenu.
Kama mlikubali kutoka gizani kwa baadhi ya ishu hata hili pia mtatoka tuu.

Kwa hiyo kama Babaako alikuwa mtumwa au mama yako alikuwa mtumwa au alikeketwa na binti yako ndio utamkeketa?
Kifupi ulofa ndio unakusumbua tafuta Hela wewe

Hizi lugha za kimaskini zitaondoka kinywani mwako.
Umaskini ndio unafanya mtu kuwa na vimisimamo vya ajabu kama vyako
Hili andiko lako linaonyesha wazi wewe lofa shilingi inakupiga chenga sana

Kwa hiyo kwa akili yako ukitoa milioni 2 kununua Mwanamke ndio kuwa na pesa? Au ndio ujanja?

Kuna Watu akili zenu zimepitwa na wakati walahi
 
Tutawatoa gizani tuu kama sio ninyi basi watoto wenu.
Kama mlikubali kutoka gizani kwa baadhi ya ishu hata hili pia mtatoka tuu.

Kwa hiyo kama Babaako alikuwa mtumwa au mama yako alikuwa mtumwa au alikeketwa na binti yako ndio utamkeketa?

Kwa hiyo kwa akili yako ukitoa milioni 2 kununua Mwanamke ndio kuwa na pesa? Au ndio ujanja?

Kuna Watu akili zenu zimepitwa na wakati walahi
Ww Kwa akili zako hio 2 M inatosha kumnunua mtu!?
Mahari haitolewi Kwa dhana ya kumnunua MTU.

Nafikiri unahitaji kusaidiwa uelewa juu ya mahari.
 
Kwema Wakuu!

Nasisitiza, vijana kama ulikuwa ni mpango wako kutoa kuoa mwaka huu kwa kutoa mahari. Sitisha! Usitoe mahari. Ila ni vizuri kwenda kujitambulisha kwao na kwenu.
Kama kuna uwezekano fanyeni sherehe ndogo kulingana na uwezo wenu.

Kamwe Usitoe mahari.
Mahari ni kununua binadamu ambaye ni mnyama. Mtu kamwe hanunuliwi.
 
Mahari io watu wanafanya kama biashara hasa hasa makabila ya kanda ya ziwa kama wajita na wasukuma unakuta binti mmoja analipiwa mahari na wanaume zaidi ya wanne na familia inapokea tu binti anaenda anaolewa miezi mitatu anafanya fujo anaachika kisha anaolewa kwingineko.
 
Unatetea utu wa wanawake lakini wanawake wenyewe watakupinga
 
Mahari io watu wanafanya kama biashara hasa hasa makabila ya kanda ya ziwa kama wajita na wasukuma unakuta binti mmoja analipiwa mahari na wanaume zaidi ya wanne na familia inapokea tu binti anaenda anaolewa miezi mitatu anafanya fujo anaachika kisha anaolewa kwingineko.

Wanunuaji, wauzaji, anayeuzwa wote ni wajinga
 
Ww Kwa akili zako hio 2 M inatosha kumnunua mtu!?
Mahari haitolewi Kwa dhana ya kumnunua MTU.

Nafikiri unahitaji kusaidiwa uelewa juu ya mahari.

Hata bilioni moja haiwezi kununua mtu.
Ila binadamu ananunulika/ananunuliwa ndio kama hao wanawake wanaonunuliwa, watumwa walinunuliwa kwa sababu hawakuhesabika kama Watu.

Mtu huwezi mtolea mahari. Ila binadamu unamtolea tuu kwa sababu binadamu akikosa utu sio mtu tena bali mnyama, na anaweza kuuzwa kwa bei yoyote tuu.
Hata gari linaweza kuwa na thamani kuliko binadamu
 
Mahari inalipwa Toka enzi...

Biblia imeandika Mwanzo 34:12
Niambieni kiasi cha mahari na zawadi nitakayoleta, hata iwe kubwa kiasi gani nitawalipa chochote mtakachonidai.
Nipeni tu huyu msichana awe mke wangu.
Dada unaelewa maana ya neno "msichana " kama lilivyotumika hapo kwenye maandiko maana kwa ulimwengu wa sasa hakuna wasichana ukae ukijua?
 
Mahari inalipwa Toka enzi...

Biblia imeandika Mwanzo 34:12
Niambieni kiasi cha mahari na zawadi nitakayoleta, hata iwe kubwa kiasi gani nitawalipa chochote mtakachonidai.
Nipeni tu huyu msichana awe mke wangu.
Quran nayo imeandikwa?

Asking for a friend
 
Back
Top Bottom