Usitoe sadaka, umeshatoa

Umemjibu vema
 
Kaleta hoja kuhusu mambo ya Mungu, halafu hana reference kutoka andiko lolote, hatuwezi kusema yupo sahihi Ila tutasema ana roho ya korosho ama mkono wa birika.
Unataka kusema yule aliyegundua kibatari alete reference alitoa wapi wazo la kutengeneza kibatari, aliyegundua gari ane alete reference, aliyegundua kuvaa chupi nae aeleze katoa wapi, wewe kaka amka.

Hebu elezea namna sadaka yako ya sh. 10,000 iliyompa mtu wa Mungu itakavyomfikia Mungu huko mbinguni. Tueleze kama Mungu ana shida ya hela au nyama.

Tueleze hizo sadaka Mungu anaziweka wapi kwa kazi gani.
 
Apia
 
unaanzisha vita na wachunga kondoo
Nafahamu. Hii ni biashara kubwa sana ya wajinga kwa kutumia jina la mungu. We chunguza tu, kila mchunga kondoo anaposema na kutenda jambo (maombi, kuhubiri, kufynga ndoa, maziko, nk), mwishoweeee kulee ataishia na kukusanya sadaka.

Huyo MUNGU anatumbo gani la kula sadaka zote hizodunia nzima? ni upuuzi tu, ni heri wangeyaita malipo au ada ya kusema au kutenda jambo fulani kuliko kuita sadaka.
 
Ni kweli Mkuu

Kweli KABISA!

Sadaka KWA nyumba za ibada ni wizi uliohalalishwa KABISA na Taasisi!!

Hata zaka walizotoa Wana wa Israel zili liwa na hao watoaji na kubakiza kidogo KWA walawi AMBAO Ndio walipewa jukumu Sasa leo KILA mtu ni kuhani nani wa kumpa mwenzake sadaka!??

Tuwape WAZAZI tu Basi!
 
Bora wale wazee wetu.
 
hatari sana
 
Africa bila di....i uchuro ingefika mbali
Wakati waliotuletea dini wakiendelea na sera za ushoga na kutengeneza mabomu makubwa ya kuuwa watu sisi tunahangaika na sadaka. Wajinga hawataisha kaka endelea kuhifadhi kucha za majogoo unaowachinja, zitapata kazi.

Watu wanajenga msikiti na makanisa kila kona kwaajili ya wajinga wanaotoa sadaka.
 
Sadaka ina siri kubwa katika mafanikio yako,Hata hao wazungu wanatoa sana ndio maana wanafanikiwa
 
Sadaka ya kweli ni ile inayoliwa na wazazi wako pamoja na familia yako.

Nyingine ni ile inayoliwa na watu mbalimbali wasiojiweza
Hiyo sasa ndio sadaka pendwa na kusudiwa, ndio maana hata mitume na mababu zetu walikuwa wanatoa vyakula na wanyama wanaokwenda kusaidia watu na wanyama wengine kuongezea kile walichopewa na Mungu ambacho hakikuwatosha au kuwafikia kwasababu mbalimbali.

Mfano, mtoto kapewa riziki zake na Mungu lakini kupitia kwa wazazi wake, hivyo kama wazazi wake wamekufa wote ina maana mtoto huyu (yatima) atahitaji sadaka kwakuwa mzigo wake haumfikii kwakuwa lori la mizigo yake limetumbukia mtoni.

Mjane alikuwa akipata baadhi ya riziki zake kupitia Mume wake, sasa mume hayuko hivyo kuna baadhi ya mizigo yake haimfikii. Wazee walikuwa wanatoa sadaka kama kumwaga chini togwa, mbege na vyakula ili kusaidia wadudu na wanyama wa MweziMungu wapate riziki.

Walikuwa wanachinja wanjama na kuwapa watu wote wale hata wale wasiokuwa na uwezo wa kula nyama wale, hizi ndizo sadaka za kweli anazozifahamu Mungu. Hizi bahasha za khaki madhabahuni ni upuuzi na wizi ambao unahusishwa na jina la Mungu.
 
Sadaka ina siri kubwa katika mafanikio yako,Hata hao wazungu wanatoa sana ndio maana wanafanikiwa
Nilikwambia hata wazungu hawatoi pesa madhabahuni kaka, ndio maana sasa hivi kule ulaya na marekani makanisa yamebaki yaleyale na hayapati watu, unaweza kutoka Kariakoo kufuata kanisa Kibaha sasa hivi kule. Wakati huku kwetu kila mtaa una makanisa 4.
 
Maskini angeandika mzungu wangesema anajua siri Fulani kwenye haya maisha,tatizo umeandika wewe usishangae watu kukuona umechanganyikiwa . 🤣.

Hawa ndio wabongo sasa vichwa maji ,apa watakutusi ,wengine watakupinga bila hoja ,wengine wataleta vifungu uchwara hapa, lakin nkutie nguvu tupo tulio jikita kuyafanya haya na nilizan pekeangu ndio naamin hivo lakin Leo umeniongezea nguvu zaid kuona kwamba wenye mtazamo huu tuko wengi , juzi apa pastor Uko Kenya kafukuza waumin eti kisa hawana sadaka!!! Bado watu hawayaoni haya kuwa maigizo ..hao waumini wengine hawana kazi ,wengine msimu wa kilimo haukuwa mzuri kwao, wengine wanauguza ndugu zao, wanakuja kanisani kujumuika na kutafuta faraja na tumaini jipya kwa yale wanayopitia.

How comes mtumishi uwafukuze? Kwaiyo hapa wenye akili timamu wapo wataelewa, na wengine huwa wanachelewa kuelewa ila tunaimani wataelewa tuu siku si nyingi.

Jaman hii dunia sasaiv tunasisitizana sana kutafuta Hela, sasa kinachokufanya usiamin kwamba makanisa yamefunguliwa kutekeleza agizo la "tutafute hela" ni kipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…