kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
- Thread starter
- #41
sada haziendi kwa Mungu, na Mungu hali sadaka. Kila mtu anatoa na kupokea sadaka kila siku, na ukitoa zaidi utapokea zaidi, mfano kama wewe unatoa michango (sadaka) mingi ya harusi kwa watu wengi zaidi nawewe utapokea michango mingi zaidi kutoka kwa watu kama ukiwa na jambo lako, kama wewe unahudhuria misiba ya watu na wewe utapata watu wengi kwenye misiba utakayoipata. Maana sadaka ni msaada, pale zamani kulikuwa hakuna pesa hivyo sadaka ilikuwa ni chakula, wanyama, na mazao, baadae ikaongezeka nguo na fedha.Ni kweli Mkuu
Kweli KABISA!
Sadaka KWA nyumba za ibada ni wizi uliohalalishwa KABISA na Taasisi!!
Hata zaka walizotoa Wana wa Israel zili liwa na hao watoaji na kubakiza kidogo KWA walawi AMBAO Ndio walipewa jukumu Sasa leo KILA mtu ni kuhani nani wa kumpa mwenzake sadaka!??
Tuwape WAZAZI tu Basi!
Sadaka usitoe madhabahuni kwenye vihenge, umeliwa. Anaekusanya ile sadaka pale madhabahuni kitu cha kwanza kabisa anakwenda kutoa sadaka kwa wazazi wake kwakuwa anafahamu umuhimu wa wazazi, maana kuna maandiko kabisa yanayomtaka mtu Awaheshimu Baba na mama yake ili siku zake ziwe nyingi zilizobaki anakwenda kufanyia mambo yake. Shida iko kwako ambae badala ya kumpa baba na mama yako sadaka umempa mla kondoo tu basi na kuwaacha wazazi wako.