Usitoe sadaka, umeshatoa

sada haziendi kwa Mungu, na Mungu hali sadaka. Kila mtu anatoa na kupokea sadaka kila siku, na ukitoa zaidi utapokea zaidi, mfano kama wewe unatoa michango (sadaka) mingi ya harusi kwa watu wengi zaidi nawewe utapokea michango mingi zaidi kutoka kwa watu kama ukiwa na jambo lako, kama wewe unahudhuria misiba ya watu na wewe utapata watu wengi kwenye misiba utakayoipata. Maana sadaka ni msaada, pale zamani kulikuwa hakuna pesa hivyo sadaka ilikuwa ni chakula, wanyama, na mazao, baadae ikaongezeka nguo na fedha.

Sadaka usitoe madhabahuni kwenye vihenge, umeliwa. Anaekusanya ile sadaka pale madhabahuni kitu cha kwanza kabisa anakwenda kutoa sadaka kwa wazazi wake kwakuwa anafahamu umuhimu wa wazazi, maana kuna maandiko kabisa yanayomtaka mtu Awaheshimu Baba na mama yake ili siku zake ziwe nyingi zilizobaki anakwenda kufanyia mambo yake. Shida iko kwako ambae badala ya kumpa baba na mama yako sadaka umempa mla kondoo tu basi na kuwaacha wazazi wako.
 
Kila Mtu na life style yake, na kizuri zaidi maisha hayanaga kanuni unaweza usitoe na ukawa msindikizaji tu wa mafanikio ya wengine miaka nenda rudi [emoji124][emoji1]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Acha kubwia ugoro hiyo kitu huharibu kabisa akili 😜
 
Na mie naongezea "atawaacha baba yake na mama yake......."

Guess will happen
Uunawaacha inamaanisha unaanza maisha mapya na mkeo haimaanishi uwadharau.... Anamalizia uishi miaka mingi na upate heri katika nchi upewayo na BWANA Mungu wako
 
Uunawaacha inamaanisha unaanza maisha mapya na mkeo haimaanishi uwadharau.... Anamalizia uishi miaka mingi na upate heri katika nchi upewayo na BWANA Mungu wako
Siwezi kuwadharau wazazi wangu ila nitaenda kuanzisha familia pasipo kuwategemea wao (kiuchumi)
 
Waheshimu baba yako na mama yako ili siku zako za kuishi ziwe nyingi.

Hakuna upinzani ktk hilo

Ila mtoa mada hajui alisemalo ktk huu uzi wake.
na heri duniani, anawasema wanaomjali pastor kuliko wazazi
 
Hivi unaamini tunapotoa sadaka tunataka akazile Mungu?

!!!!
 
Kwa hiyo watoto yatima wapeleke hoja zoa kwa nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…