Usitoe sadaka, umeshatoa

Kisa umevuliwa uchungaji unaanza kukandia wenzio wasipewe ,acha watu watoe wabarikiwe
 
Kujenga kanisa na kununua kiti inajulikana bei yake kama vile inavyofahamika gharama ya harusi. Kujenga kanisa na vitu kunahitaji michango kulingana na bajeti ya ujenzi, havihaji sadaka.

Tena makanisa mengine yalijengwa na mkoloni lakini watu wanadai sadaka kila siku. tofautisha kati ya sadaka na michango.
 
Yote hayo ni kazi bure kama hujui mzazi wako ana shida gani inayohitaji kutatuliwa na wewe kabla ya kuziona shida na tabu za watu wengine.
 
Reactions: Tsh
leteni sadaka gharani, maana alikusudia vyakula. Leo hii mabaladhuli hawataki sadaka za mihogo na magimbi, wanataka fedha. Mungu hapendi fedha na ameilaani baada ya kusababisha kifo cha Yesu.
 
Reactions: Tsh
Mungu hataki sadaka kama vile mmiliki wa kiwanda cha sukari isivyotaka sukari ya kutoka nje iletwe nchini. Mungu ana vitu vingi mno vyote ni original (the gold standard), kwanini atake kikondoo chako kilichokondeana? riziki amekupa yeye kwanini umrudishie? yaani mtoto wako umempa hela akalipe ada halafu baba huyohuyo amtake mtoto wake huyohuyo mwanafunzi amtumie hela ya matumizi. Hakuna Mungu mjinga wa aina hiyo. Sadaka wanakula wahuni na familia zao.

Kitakachokuponya wewe ni kushukuru kwa dhati na imani yako isiyotikisika kamwe. Imani iliyo imara inahitaji kugusa pindo la kanzu tu kupata uponyaji.
 
Reactions: Tsh
Jamaa ananunua dumu la mafuta ya korie na kuweka kwenye vichupa vya mils 10 na kuuza kila kimoja sh. 1000, hebu nambie dumu la lita 20 anapata sh ngapi? Lita 1 = 1000mls, kwahiyo 20 x 1000 x 1000 = 20,000,000/10 = 2,000,000
Wajinga hawaishi usitupe pembe zako.
 
Ibrahim alitoa sadaka kwa mungu. Wana wa Israel walitoa sadaka kwa mungu, daudi na Suleiman pia. Halafu anakuja hapa kutwambia tusitoe sadaka[emoji706][emoji706][emoji706]
Walipompa yiyosadaka Mungu aliipokea nakuiweka wapi?
 
Mchungaji akipata kazi sawa, ila vipi awe anachukua mshahara wake ananunua umeme, ulinzi, usafi, ujenzi, usafiri nk?
iko siku umesikia wakisema leo msitoe sadaka kwakuwa hela za kuwalipa walinzi, umeme na wanafanya usafi zipo?
 
iko siku umesikia wakisema leo msitoe sadaka kwakuwa hela za kuwalipa walinzi, umeme na wanafanya usafi zipo?
Ziwepo vipi wakati hizo huduma ni za kila leo. Wewe huwa unaacha kutafuta unatumia mpaka ziishe? Mbona huna common sense mkuu.
 
Baba hawi baba yako kwasababu ya kukutunza, bali anakuwa baba yako kwasababu ya kukuzaa, unayo damu yake, unao mhuri wake, amekubali kutumwa na Mungu kukuleta wewe. Unaweza kutunzwa vizuri sana na mjomba wako au hata jirani lakini mojomba na jirani hawawezi kuwa baba yako.

Hata Mungu haachi kuwa Mungu kwasababu wewe hujapata mtoto au gari kama wengine, baba atakuwa baba no matter how.

Viumbe vyote vya mungu havitunzwi na baba yao. Hebu ona jogoo, beberu, dume la simba, kondoo, nguchilo, panzi, kunguru. Wote hawa wanazaa lakini mama anatunza, kazi muhimu ya baba ni kuzaa.
 
Unamaanisha bira viongozi wa dini kazi za Mungu hazifanyiki
 
Walipompa yiyosadaka Mungu aliipokea nakuiweka wapi?
Kudanganywa huku sio kwa kawaida, Kumrudishia Mungu vitu vyake ni ibada au ni kumsusia na kumkejeli? Yaani mimi nina berkary ya kuoka mikate mingi ya kulisha nchi nzima, nikakupa wewe mkate mmoja halafu wewe unanipa mimi kipande cha mkate huohuo niliokupa ukidhani kuwa nitakusifu au nitakuongeza mwingine kwa wewe kufanya hivyo. Ukifanya hivyo ninajuwa kuwa wewe hukuwa na shida ya mkate, huutaki, hivyo sikupi tena.

Mungu wetu tusimsingizie upuuzi kwa faida zetu binafsi. Anaehitaji sadaka ni wazazi wako na watu wengine, sio Mungu.
 
Reactions: wwg
Yote hayo ni kazi bure kama hujui mzazi wako ana shida gani inayohitaji kutatuliwa na wewe kabla ya kuziona shida na tabu za watu wengine.
Huwezi kutatua ya wengine kabla hujatatua ya kwako. Huo utakuwa unafiki wa kujionyesha.
 
Kule sio ndio makao ya shetani awakamate mara ngapi,wao wanaabudu shetani kupitia dragon.Unaona wachina Wana utu? Kazi ya dini ni kuishape jamii kwa huduma za kiroho na kimwili.
Kwahiyo unamaanisha shetani ananguvu kumshinda Mungu
 
Nimeamini kwamba kuwa na uwezo wa kuandika hoja ni kitu kimoja na kujenga hoja yenye maana pia ni swala lingine.

Kwa wakristo wenzangu someni Malaki 3:8-12.
Watu wanaangamia kwa kukosa maarifa
 
Kwahiyo unamaanisha shetani ananguvu kumshinda Mungu
Kaka ni wajanya sana hawa, ili kupata sadaka nyingi huwa wanatumia 90% ya muda wa mahubiri kuongelea ubaya wa shetani na 10% kuongelea ukubwa, uwezo, nguvu na mamlaka ya Mungu kwa viumbe na ulimwengu mzima. Wanaogopa kama wakimzungumzia Mungu sana na maguvu yake yasiyomithilika kutakuwa hakuna shetani tena, maana hata shetani atakuwa amechinjwa na Mungu, hayupo.

Bila kuwepo kwa shetani mwenye nguvu, mwenye hila, mjanja kutakuwa hakuna dhambi hivyo hakutakuwa na sadaka. Ukweli ni kwamba, ni aibu kubwa kuhubiri ubaya na ukubwa wa shetani wakati Mungu aliyemuumba binadamu, shetani, viumbe wengine wote na ulimwengu yupo hai.

Siku moja nilimsikia "mtu wa Mungu" akisema "Umejaribiwa", nikamuuliza nimejaribiwa na nani? akasema na Mungu. NIkajisikia natoka jasho kila sehemu, kwakuwa hata mimi binadamu nisiyekuwa na akili siwezi kujaribu kubeba container tupu kwenye bajaj kwakuwa najua kuwa bajaj haitaweza kulibeba container hata kwa sekunde moja tu.

Nikamuuliza kwahiyo Mungu ananijaribu mimi kwakuwa hajui uwezo wangu wa kuweza au kushindwa kwenye hili? Ni Mungu gani huyo asiyejua matokeo ya majaribu yake kwangu? Hajui uimara na udhaifu wangu? hajui kama nitapona au nitakufa? hajui kama nitashinda au nitashindwa?

Kwani Mungu ni kama sisi ambao hatuijui kesho yetu?. Mara nikamuona yeye ndiye anaanza kutetemeka na kutoka jasho kila sehemu.
 
Maandiko yanayosema wasaidie yatima na wajane, wao watampa nani sadaka? We jamaa
 
Asilimia kubwa ya wanaokusapoti wanashinda kwenye vilinge kuchinja mbuzi na ng’ombe kafara kwa miungu yao. wengi mnaamini sadaka za wanyama mnaziacha kwa waganga wanawaaminisha wanapokea mizimu ila kutoa kanisani ndo zinaenda kubaya. Mungu awarehemu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…