Usitoe sadaka, umeshatoa

Usitoe sadaka, umeshatoa

Kisa umevuliwa uchungaji unaanza kukandia wenzio wasipewe ,acha watu watoe wabarikiwe
 
Shambulizi kubwa kwa kanisa lilikuwa kumtundika Yesu msalabani, baada ya lile yote yalishindwa palelale msalabani, mtu anasema Mungu hali sadaka, hilo kanisa alijenga Bibi yako? kiti unachokalia kanisani umetoa nyumbani kwako, watumishi wanaokuhudumia wanalipwa na serikali? Hio biblia unayonukuu kuhusu kuwaheshimu wazazi ilidondoshwa na radi?
Kujenga kanisa na kununua kiti inajulikana bei yake kama vile inavyofahamika gharama ya harusi. Kujenga kanisa na vitu kunahitaji michango kulingana na bajeti ya ujenzi, havihaji sadaka.

Tena makanisa mengine yalijengwa na mkoloni lakini watu wanadai sadaka kila siku. tofautisha kati ya sadaka na michango.
 
Acha uongo.
Yaani mtu anayelisha walio na njaa, anayesomesha wasio na ada, anayelipia matibabu ya wasio na fedha za matibabu isitoshe kumpatia haki? Umesahau amri ya Upendo?

Endeleeni kudanganya ila yule anayetoa alichonacho na kugawana na asiyenacho ana haki kuliko yule anayepeleka sadaka kwa mchungaji.
Yote hayo ni kazi bure kama hujui mzazi wako ana shida gani inayohitaji kutatuliwa na wewe kabla ya kuziona shida na tabu za watu wengine.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Makanisa yanajengwa na hayataacha kujengwa sababu fedha za ujenzi wa makanisa hutolewa na waumini. Tena makanisa mengine yanatoa maelekezo kabisa, "MCHANGO WA UJENZI WA KANISA"

Hapa suala ni sadaka kila siku za ibada huwa zinafanya kazi gani huko kwa MUNGU ambaye ulimwengu na vyote ni vyake? Kwanini anazihitaji sadaka kuliko wagonjwa, wenye njaa na masikini? Aliposema leteni zaka kamili ghalani alitoa maelekezo kuwa baada ya kukaa ghalani zitafanyiwa nn? Au kuhoji hilo ni kukufuru?
leteni sadaka gharani, maana alikusudia vyakula. Leo hii mabaladhuli hawataki sadaka za mihogo na magimbi, wanataka fedha. Mungu hapendi fedha na ameilaani baada ya kusababisha kifo cha Yesu.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Makanisa yanajengwa na hayataacha kujengwa sababu fedha za ujenzi wa makanisa hutolewa na waumini. Tena makanisa mengine yanatoa maelekezo kabisa, "MCHANGO WA UJENZI WA KANISA"

Hapa suala ni sadaka kila siku za ibada huwa zinafanya kazi gani huko kwa MUNGU ambaye ulimwengu na vyote ni vyake? Kwanini anazihitaji sadaka kuliko wagonjwa, wenye njaa na masikini? Aliposema leteni zaka kamili ghalani alitoa maelekezo kuwa baada ya kukaa ghalani zitafanyiwa nn? Au kuhoji hilo ni kukufuru?
Mungu hataki sadaka kama vile mmiliki wa kiwanda cha sukari isivyotaka sukari ya kutoka nje iletwe nchini. Mungu ana vitu vingi mno vyote ni original (the gold standard), kwanini atake kikondoo chako kilichokondeana? riziki amekupa yeye kwanini umrudishie? yaani mtoto wako umempa hela akalipe ada halafu baba huyohuyo amtake mtoto wake huyohuyo mwanafunzi amtumie hela ya matumizi. Hakuna Mungu mjinga wa aina hiyo. Sadaka wanakula wahuni na familia zao.

Kitakachokuponya wewe ni kushukuru kwa dhati na imani yako isiyotikisika kamwe. Imani iliyo imara inahitaji kugusa pindo la kanzu tu kupata uponyaji.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Wazo lako zuri, wakifanyia kazi ambao ndio watoa sadaka wakubwa, akili ya kutafakari hawana. Mafanikio ya akina Mwamposa ni uwepo wa watu hao tena kwa wingi. Mafanikio ya wajanja wachache ni matokeo ya uwepo wa wajinga wengi. Na wajanja wanaitumia fursa vilivyo kwa kuitumia falsafa ya usimwamshe mjinga.
Jamaa ananunua dumu la mafuta ya korie na kuweka kwenye vichupa vya mils 10 na kuuza kila kimoja sh. 1000, hebu nambie dumu la lita 20 anapata sh ngapi? Lita 1 = 1000mls, kwahiyo 20 x 1000 x 1000 = 20,000,000/10 = 2,000,000
Wajinga hawaishi usitupe pembe zako.
 
Ibrahim alitoa sadaka kwa mungu. Wana wa Israel walitoa sadaka kwa mungu, daudi na Suleiman pia. Halafu anakuja hapa kutwambia tusitoe sadaka[emoji706][emoji706][emoji706]
Walipompa yiyosadaka Mungu aliipokea nakuiweka wapi?
 
Mchungaji akipata kazi sawa, ila vipi awe anachukua mshahara wake ananunua umeme, ulinzi, usafi, ujenzi, usafiri nk?
iko siku umesikia wakisema leo msitoe sadaka kwakuwa hela za kuwalipa walinzi, umeme na wanafanya usafi zipo?
 
iko siku umesikia wakisema leo msitoe sadaka kwakuwa hela za kuwalipa walinzi, umeme na wanafanya usafi zipo?
Ziwepo vipi wakati hizo huduma ni za kila leo. Wewe huwa unaacha kutafuta unatumia mpaka ziishe? Mbona huna common sense mkuu.
 
Kuna wababa wana watoto kila kona na hawawaudumii mama ndo anateseka nao, kwann wale watoto waanze na baba na sio mama?

Dini zisitufunge fikira zetu na kufata maagizo yake bila kutumia ubongo. Halafu sio kila andiko lililopo kwenye biblia limekulenga ww msomaji, Mfano: Elia aliua mabaali baada ya kusadiki je na sisi tuue watu baada ya kusadiki?
Baba hawi baba yako kwasababu ya kukutunza, bali anakuwa baba yako kwasababu ya kukuzaa, unayo damu yake, unao mhuri wake, amekubali kutumwa na Mungu kukuleta wewe. Unaweza kutunzwa vizuri sana na mjomba wako au hata jirani lakini mojomba na jirani hawawezi kuwa baba yako.

Hata Mungu haachi kuwa Mungu kwasababu wewe hujapata mtoto au gari kama wengine, baba atakuwa baba no matter how.

Viumbe vyote vya mungu havitunzwi na baba yao. Hebu ona jogoo, beberu, dume la simba, kondoo, nguchilo, panzi, kunguru. Wote hawa wanazaa lakini mama anatunza, kazi muhimu ya baba ni kuzaa.
 
Wingi wa hizi mada ina maana sio bahati mbaya lazima kuna kikundi kinawatumia. Hicho kikundi ni vyema kikawaelekeza kutumia akili.
Sadaka iko kwenye maandiko matakativu,leo muhuni anakuja na blah blah tu akiwaambia watu wasitoe sadaka bila kunukuu maandiko. Jitu hili hata likienda kwa shetani kuchanjwa chale za makalio linatoa sadaka.

Tumeelekezwa tukusanyike madhabauni kumwabudu Mungu. Kwa akili ya kawaida tu, hiyo nyumba ya Mungu itajengwa vipi, inatunzwa vipi, itajiendesha vipi. Wewe uko na mkeo asubuhi mnaelekea vibaruani. Mchungaji yeye anaenda kanisani kuandaa ibada na mafundisho. Atakula kwa baba yako bila sadaka?

Halafu wahuni hawa wanakuja na mikelele humu kuhusu sadaka. Mbona simple tu nenda kwa paroko/shehe wako kamwambie mimi siwezi kutoa sadaka. Kama hausali hizo sadaka zinakuuma nini?
Unamaanisha bira viongozi wa dini kazi za Mungu hazifanyiki
 
Walipompa yiyosadaka Mungu aliipokea nakuiweka wapi?
Kudanganywa huku sio kwa kawaida, Kumrudishia Mungu vitu vyake ni ibada au ni kumsusia na kumkejeli? Yaani mimi nina berkary ya kuoka mikate mingi ya kulisha nchi nzima, nikakupa wewe mkate mmoja halafu wewe unanipa mimi kipande cha mkate huohuo niliokupa ukidhani kuwa nitakusifu au nitakuongeza mwingine kwa wewe kufanya hivyo. Ukifanya hivyo ninajuwa kuwa wewe hukuwa na shida ya mkate, huutaki, hivyo sikupi tena.

Mungu wetu tusimsingizie upuuzi kwa faida zetu binafsi. Anaehitaji sadaka ni wazazi wako na watu wengine, sio Mungu.
 
  • Thanks
Reactions: wwg
Yote hayo ni kazi bure kama hujui mzazi wako ana shida gani inayohitaji kutatuliwa na wewe kabla ya kuziona shida na tabu za watu wengine.
Huwezi kutatua ya wengine kabla hujatatua ya kwako. Huo utakuwa unafiki wa kujionyesha.
 
Kule sio ndio makao ya shetani awakamate mara ngapi,wao wanaabudu shetani kupitia dragon.Unaona wachina Wana utu? Kazi ya dini ni kuishape jamii kwa huduma za kiroho na kimwili.
Kwahiyo unamaanisha shetani ananguvu kumshinda Mungu
 
Mungu wetu alishatuumba, akawakabidhi wazazi wako wakamilishe mchakato uliobakia wa kukuzaa, kukulisha, kukuvalisha na kukutunza kwa muda fulani kabla na wewe hujaanza kujitunza na kuzaa watoto wengine. Kama ni sadaka mpe mzazi wako anaeweza kuitumia hiyo sadaka sio Mungu, kwakuwa Mungu hana matumizi ya sadaka; fedha, chakula wala mifugo yako maana vitu vyote ni vyake vinatoka kwake na anavyo vingi kuliko baba na mama yako. Wazazi wako wana matumizi, wana mwili, wana mdomo, na wana tumbo, hivyo wanajua nini cha kufanya ukiwapa pesa, nguo, chakula, mifugo. Mungu wetu anataka ushukuru tu na kumsifu kama vile unavyomsifu TOYOTA kwa kutengeneza aina ya gari lako unaloliendesha. Baada ya TOYOTA kutengeneza gari lako kazi yako ni kuisifu toyota lakini sio kutoa zawadi, malipo au kuiomba toyota ikupatie mafuta ya gari lako, ukupakie rangi gari lako wala kulifanyia matengenezo gari lako.

Kuna watu wanapoteza Muda wao mwingi kwa Kuomba Mungu badala ya Kushukuru mungu, Kuna watu wanapoteza mali zao nyingi kwa kutoa sadaka kwa Mungu badala ya kuwapa wazazi wao. Wanakosea sana na hawajui walifanyalo zaidi ya kuwatajirisha watu wanaozipokea mali (sadaka) zao. Mungu hana shida lakini wazazi wako wana shida.

Anza na wazazi wako kwanza uone mambo yako yatakavyokunyookea haraka. Kama kila mtu akihangaika na wazazi wake Mungu atasikia vilio na maombi yao haraka kwakuwa wazazi ndio bomba lako linalopitisha maombi kutoka kwako kupitia kwa wazazi, mababu, mitume, kupitia kwa Adam na Hawa hadi kumfikia Mungu, kwakuwa Adam na Eva wanamfahamu Mungu zaidi kuliko wewe, na babu yako yuko karibu na Adam, baba yako yuko karibu na babu yako, na wewe uko karibu na baba yako. Ndiyo maana kila anaewadharau wazazi na mababu zake hafiki mbali kwakuwa Mungu yuko karibu nao zaidi kuliko wewe.

kila mtu anatoa sadaka kila siku anapomsaidia mtu mwingine jambo, hata kumuonyesha mtu njia, kumpa mtu maji ya kunywa, kumbeba, kumpa chakula au soda, umeshalipa sadaka tayari, lakini mzazi wako ni wajibu sio hiari kumpa sadaka zako.

Sadaka unayotoa haifiki kwa Mungu bali inaliwa tu na wajanga wanaojifanya wanaipeleka kwa Mungu. Tafuta mayatima na wajane wape kama unataka kuwapa, lakini wajali zaidi wazazi wako, utaona mambo na miujiza wasiyoiweza "watumishi wa mungu" unaowapa hela zako kila siku. Unatapeliwa ndugu yangu, fumbua macho yako.
Nimeamini kwamba kuwa na uwezo wa kuandika hoja ni kitu kimoja na kujenga hoja yenye maana pia ni swala lingine.

Kwa wakristo wenzangu someni Malaki 3:8-12.
Watu wanaangamia kwa kukosa maarifa
 
Kwahiyo unamaanisha shetani ananguvu kumshinda Mungu
Kaka ni wajanya sana hawa, ili kupata sadaka nyingi huwa wanatumia 90% ya muda wa mahubiri kuongelea ubaya wa shetani na 10% kuongelea ukubwa, uwezo, nguvu na mamlaka ya Mungu kwa viumbe na ulimwengu mzima. Wanaogopa kama wakimzungumzia Mungu sana na maguvu yake yasiyomithilika kutakuwa hakuna shetani tena, maana hata shetani atakuwa amechinjwa na Mungu, hayupo.

Bila kuwepo kwa shetani mwenye nguvu, mwenye hila, mjanja kutakuwa hakuna dhambi hivyo hakutakuwa na sadaka. Ukweli ni kwamba, ni aibu kubwa kuhubiri ubaya na ukubwa wa shetani wakati Mungu aliyemuumba binadamu, shetani, viumbe wengine wote na ulimwengu yupo hai.

Siku moja nilimsikia "mtu wa Mungu" akisema "Umejaribiwa", nikamuuliza nimejaribiwa na nani? akasema na Mungu. NIkajisikia natoka jasho kila sehemu, kwakuwa hata mimi binadamu nisiyekuwa na akili siwezi kujaribu kubeba container tupu kwenye bajaj kwakuwa najua kuwa bajaj haitaweza kulibeba container hata kwa sekunde moja tu.

Nikamuuliza kwahiyo Mungu ananijaribu mimi kwakuwa hajui uwezo wangu wa kuweza au kushindwa kwenye hili? Ni Mungu gani huyo asiyejua matokeo ya majaribu yake kwangu? Hajui uimara na udhaifu wangu? hajui kama nitapona au nitakufa? hajui kama nitashinda au nitashindwa?

Kwani Mungu ni kama sisi ambao hatuijui kesho yetu?. Mara nikamuona yeye ndiye anaanza kutetemeka na kutoka jasho kila sehemu.
 
Nimekosa pa kunukuu mkuu kwakuwa nukuu zote zilizopo zimeandikwa na wanufaika wa sadaka. Hapa nimetumia uncommon sense, ufunuo na kutazama viumbe wengine. Hebu niambie Mungu na hela vinaendana? atanunulia nini ukimpa fedha, je ana tumbo na mdomo? je, anategemea utakachompa?
Maandiko yanayosema wasaidie yatima na wajane, wao watampa nani sadaka? We jamaa
 
Asilimia kubwa ya wanaokusapoti wanashinda kwenye vilinge kuchinja mbuzi na ng’ombe kafara kwa miungu yao. wengi mnaamini sadaka za wanyama mnaziacha kwa waganga wanawaaminisha wanapokea mizimu ila kutoa kanisani ndo zinaenda kubaya. Mungu awarehemu sana
 
Back
Top Bottom