Usitoe sadaka, umeshatoa

Usitoe sadaka, umeshatoa

Yaani watu wa Jf sijui huwa wanaogopa kuonekana wanapinga. Mna kazi ya ku like na kusema tu kweli, ni sawa kabisa. Yaani Mtu Kaja
Na story tu hana hata kifungu alicho
Quote.

Mimi Nataka mtoa mada unirekebishe kwenye hili neno La biblia ambalo ni
malaki 3:8-12 inamaana wewe ndo unaakili Kuliko hilo neno? Na nyie wengine Mnaomtetea. Someni kwanza hilo neno.
 
ZIFAHAMU AINA ZA SADAKA NA FAIDA ZAKE

Date: April 21, 2020Author: Peter Ogast4
Sadaka ni sehemu ya utoaji unaoacha pengo Katika Mali zako, yaani baada ya kutoa unaona mahali ulikotoa Mali hiyo pameachwa wazi.

Hata hivyo Biblia inasema utoaji Wa kweli ni kujitoa nafsi yako kwanza kwa Mungu kama dhabihu mtakatifu ya kumpemdeza Mungu.
“Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.”
(rom 12: 1)

Mungu anatengemea tutor nafsi, roho na miili yetu kama sehemu ya sadaka kwa Mungu. Itakusaidia nini kama utajitoa kwa ulimwengu na KUFANYA viungo vyako kuwa silaha za dhuluma kwa ulimwengu Bali tujitoe kwa Mungu kuwa sadaka kwa Mungu.(1Kor 6:13-16 )
————
13 Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili.

14 Naye Mungu alimfufua Bwana, na tena atatufufua sisi kwa uweza wake.

15 Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!

16 Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.

Mwili wako, nafsi yako na roho yako utoe kwa BWANA kama dhabihu takatifu kwa BWANA. Yafutayo ni mambo saba unayopaswa kujua KUHUSU sadaka yako, kama ifuatavyo;

1. SADAKA INANENA MBELE ZA BWANA
Sadaka yako unaweza kunena vena Mbele za Mungu ikawa UKUMBUSHO Wa Yale uliyomba kwa Mungu, Sadaka haiwezi kunyamaza hata kidogo.

Mfano:1. KORNELIO

1 Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia,
Matendo ya Mitume 10 :1

2 mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima.
Matendo ya Mitume 10 :2

3 Akaona katika maono waziwazi, kama saa tisa ya mchana, malaika wa Mungu, akimjia na kumwambia, Kornelio!
Matendo ya Mitume 10 :3

4 Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.
Matendo ya Mitume 10 :4

MFANO:2 DORKASI

(Mat 9 )
————
36 Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi (yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa.

37 Ikawa siku zile akaugua, akafa; hata walipokwisha kumwosha, wakamweka orofani.

38 Na kwa kuwa mji wa Lida ulikuwa karibu na Yafa, nao wanafunzi wamesikia ya kwamba Petro yuko huko, wakatuma watu wawili kwake, kumsihi na kusema, Usikawie kuja kwetu.

39 Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika, wakampeleka juu orofani wajane wote wakasimama karibu naye, wakilia na kumwonyesha zile kanzu na nguo alizozishona Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao.

40 Petro akawatoa nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, ondoka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi.

41 Akampa mkono, akamwinua; hata akiisha kuwaita wale watakatifu na wajane akamweka mbele yao, hali yu hai.

2.TOA SADAKA YAKO KWA IMANI.
Katika utoaji wako iwe fungu LA kumi,limbuko, sadaka ya nadhiri,au changizo lolote. Toa kwa IMANI. Toa kwa matarajio fulani kuwa MUNGU atakusaidia katika jambo Fulani. Hiyo nfiuo tafsiri ya IMANI. IMANI ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, hivyo tarajia kitu kwa BWANA YESU.

4 Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena.
Waebrania 11 :4

Unapotoa sadaka yako uwe unatarajia kitu kwa Mungu, unaona waliotoa hata kama wamekufa Mungu aliwafufua, wengine wananena sadaka yako inasema za Mungu.

3.USITOE KWA MANUNGUNIKO AU KUJISIFU.

Unapotoa sadaka yako unapaswa kukumbuka usitoe kwa kunungunika au majivuno au kwa huzuni maana Mungu anataka MTU anayetoa kwa moyo mkunjufu.

(2Kor 9 )
————
6 Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.

7 Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.

(Gal 6 )
————
6 Mwanafunzi na amshirikishe mkufunzi wake katika mema yote.

7 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.

8 Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.

9 Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho.

4. USIWE NA NENO NA MTU.

Moja ya kikwazo mbele za Mungu kuhusu sadaka ni kama hujapatana na uliyekosana naye. Hakikisha umepatana na mtu, maana kuna uhusiano kati ya sadaka na moyo wako hivyo MUNGU ana taka moyo wako. Patana na mtu uliyemkwaza.

(Mat 5 )
————
23 Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,

24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako.

25 Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani.

5.KILA AINA YA SADAKA KUNA BARAKA ZAKE/AHADI ZA MUNGU KUTUBARIKI.
Fungu LA kumi au zaka. Mungu ameahidi kufungua mbingu zako au vyanzo vipya vya mafanikio. Ukipata mapato mapya unatoa aslimia kumi kwa mfano 10% ya 100=10. Ukitoa fedha hapa usitarajie kupewa pesa Bali utapewa vyanzo vipya vya kipatia kipato(Mal 3 :8_11 Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.
9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.
10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
Malimbuko…Mungu ameahidi Baraka za malimbuko au uzao Wa kwanza.
(Met 3:
9 Mheshimu Bwana kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote.10 Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya..
NADHIRI
Nadhiri ni ahadi tunazomwekea MUNGU kuwa akitufanya jambo sisi tutatimiza jambo Fulani kwa moyo wetu Washukrani mbele zake “Akaweka nadhiri, akasema, Ee Bwana wa majeshi, ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume, ndipo mimi nitakapompa Bwana huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikilia kichwani kamwe.(“1Samwel 1:11)

SADAKA ZINGINE Mungu anaangalia moyo wako maana haina kiwango lakini haimaanishi utoe kidogo. (2Kor 9 )
6 Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.7 Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.
8 Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;

9 kama ilivyoandikwa, Ametapanya, amewapa maskini, Haki yake yakaa milele.

10 Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu;

11 mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu.

12 Maana utumishi wa huduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu, bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu.

5.USITOE SADAKA YAKO KWENYE MADHABAHU YA MUNGU MWINGINE.

Sadaka ni Ibada usije ukatoa ibada kwenye madhabahu ya sanamu au kwa makuhani baali. Nakumbuka siku moja wa ukoo wangu waliomba nichangie sehemu ya fedha kwa ajili ya kutimiza tambiko. Nilikataa kabisa.Nakumbuka kabla ya kuokoka tulikuwa tunatoa nia ya misa kwa ajili ya wafu, nakuomba waliokufa lakini nilipookoka macho yangu yalifunguliwa. Mpendwa usije ukafanya jambo ambalo litakuunganisha na madhabuhu ya Giza.

(Kuto 20 )

23 Msifanye miungu mingine pamoja nami; miungu ya fedha, wala miungu ya dhahabu, msijifanyie.

24 Utanifanyia madhabahu ya udongo, nawe utatoa dhabihu zako juu yake; sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani, kondoo zako, na ng’ombe zako, kila mahali nitakapotia ukumbusho wa jina langu, hapo ndipo nitakapokujilia na kukubarikia.

“Mtu atakayemchinjia sadaka mungu ye yote, isipokuwa ni yeye Bwana peke yake, na angamizwe kabisa.”
(Kuto 22: 20)

6. TOA SADAKA YAKO KWA TARATIBU ZA BIBLIA.

Biblia natoa taratibu kwa kila aina ya sadaka unatoa hivyo tenda vema utapata kibali na sadaka yako itasema mbele za MUNGU kama tulivyojifunza KATIKA namba moja.

Ukitoa vibaya MUNGU hapokei.(Mwa 4 )
————
1 Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa Bwana.2 Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi.
3 Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana.

4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake;

5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.

6 Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?

7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishnde.

MKUMBUSHE MUNGU KUHUSU AHADI ZAKE / DAI HAKI ZAKO NAWE UTAPEWA.

Mungu mwenyewe katuruhusu tumkumbushe ahadi zake. Mpendwa jipange usiwe na mpengo KATIKA UTOAJI wako.

(Is 43 )
————
25 Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.

26 Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako.

Ubarikiwe.
Tunakubaliana sote kuwa yuko mtu ambae ametuumba sisi wote, viumbe vyote, vitu vyote vilivyoko angani na ardhini. Kwa kifupi ni kwamba Mungu ameumba vyote na ni vyake yeye mwenyewe, ametupa bure na ataendelea kutoa kwa amtakae yeye. Swali ni je, huyu Mungu mwenye vitu vyote hivi anahitaji sadaka? je. sadaka tunazozitoa zinakwenda kwake? je, yuko anaekula sadaka hizi kwa niaba ya Mungu?

Ndiyo maana tunasema sadaka hizi yafaa ziwasadie watu kama mchango wetu katika kuziba mapungufu madogomadogo tuliyonayo kama binadamu.

Kama kuna mtu anaumwa na hana namna ya kujitibu ni vema tumtolee sadaka zetu akatibiwe, maana mungu hatamletea machela ya kumbeba kwenda kwenye matibabu kama vile ambavyo Mungu hatakubeba kwenda chooni ukajisaidie ila sisi binadamu tunaweza kumbeba mwenzetu kwenda chooni, mungu hatamletea mtu chakula ila sisi tunaweza kumpa mwenzetu chakula, nk.

Usitoe pesa madhabahuni isiyokuwa na maelezo ya nani anahitaji sadaka zetu.
 
Mungu wetu alishatuumba, akawakabidhi wazazi wako wakamilishe mchakato uliobakia wa kukuzaa, kukulisha, kukuvalisha na kukutunza kwa muda fulani kabla na wewe hujaanza kujitunza na kuzaa watoto wengine. Kama ni sadaka mpe mzazi wako anaeweza kuitumia hiyo sadaka sio Mungu, kwakuwa Mungu hana matumizi ya sadaka; fedha, chakula wala mifugo yako maana vitu vyote ni vyake vinatoka kwake na anavyo vingi kuliko baba na mama yako.

Wazazi wako wana matumizi, wana mwili, wana mdomo, na wana tumbo, hivyo wanajua nini cha kufanya ukiwapa pesa, nguo, chakula, mifugo. Mungu wetu anataka ushukuru tu na kumsifu kama vile unavyomsifu TOYOTA kwa kutengeneza aina ya gari lako unaloliendesha. Baada ya TOYOTA kutengeneza gari lako kazi yako ni kuisifu toyota lakini sio kutoa zawadi, malipo au kuiomba toyota ikupatie mafuta ya gari lako, ukupakie rangi gari lako wala kulifanyia matengenezo gari lako.

Kuna watu wanapoteza Muda wao mwingi kwa Kuomba Mungu badala ya Kushukuru mungu, Kuna watu wanapoteza mali zao nyingi kwa kutoa sadaka kwa Mungu badala ya kuwapa wazazi wao. Wanakosea sana na hawajui walifanyalo zaidi ya kuwatajirisha watu wanaozipokea mali (sadaka) zao. Mungu hana shida lakini wazazi wako wana shida.

Anza na wazazi wako kwanza uone mambo yako yatakavyokunyookea haraka. Kama kila mtu akihangaika na wazazi wake Mungu atasikia vilio na maombi yao haraka kwakuwa wazazi ndio bomba lako linalopitisha maombi kutoka kwako kupitia kwa wazazi, mababu, mitume, kupitia kwa Adam na Hawa hadi kumfikia Mungu, kwakuwa Adam na Eva wanamfahamu Mungu zaidi kuliko wewe, na babu yako yuko karibu na Adam, baba yako yuko karibu na babu yako, na wewe uko karibu na baba yako. Ndiyo maana kila anaewadharau wazazi na mababu zake hafiki mbali kwakuwa Mungu yuko karibu nao zaidi kuliko wewe.

kila mtu anatoa sadaka kila siku anapomsaidia mtu mwingine jambo, hata kumuonyesha mtu njia, kumpa mtu maji ya kunywa, kumbeba, kumpa chakula au soda, umeshalipa sadaka tayari, lakini mzazi wako ni wajibu sio hiari kumpa sadaka zako.

Sadaka unayotoa haifiki kwa Mungu bali inaliwa tu na wajanga wanaojifanya wanaipeleka kwa Mungu. Tafuta mayatima na wajane wape kama unataka kuwapa, lakini wajali zaidi wazazi wako, utaona mambo na miujiza wasiyoiweza "watumishi wa mungu" unaowapa hela zako kila siku. Unatapeliwa ndugu yangu, fumbua macho yako.
Sadaka unazopeleka kwa mizimu, je hiyo mizimu inatumia wapi sadaka? Unapoenda kuwasaidia yatima na wajane umetenda jambo jema kwa Mungu, unapowasaidia wazazi wako ni jambo jema mbele za Mungu na ndio anavyotaka lakini usijeacha kupeleka sadaka madhabahuni kwa kuhani ni agizo la Mungu kama unaamini katika Mungu, na kama uamini endelea na njia Yako, na ni kweli kuhani atakula lakini ukipatwa na shida ya kiroho mbona huwa hujiulizi ulizi, maswali ya sadaka yangu inaliwa??
 
Tunakubaliana sote kuwa yuko mtu ambae ametuumba sisi wote, viumbe vyote, vitu vyote vilivyoko angani na ardhini. Kwa kifupi ni kwamba Mungu ameumba vyote na ni vyake yeye mwenyewe, ametupa bure na ataendelea kutoa kwa amtakae yeye. Swali ni je, huyu Mungu mwenye vitu vyote hivi anahitaji sadaka? je. sadaka tunazozitoa zinakwenda kwake? je, yuko anaekula sadaka hizi kwa niaba ya Mungu?

Ndiyo maana tunasema sadaka hizi yafaa ziwasadie watu kama mchango wetu katika kuziba mapungufu madogomadogo tuliyonayo kama binadamu. Kama kuna mtu anaumwa na hana namna ya kujitibu ni vema tumtolee sadaka zetu akatibiwe, maana mungu hatamletea machela ya kumbeba kwenda kwenye matibabu kama vile ambavyo Mungu hatakubeba kwenda chooni ukajisaidie ila sisi binadamu tunaweza kumbeba mwenzetu kwenda chooni, mungu hatamletea mtu chakula ila sisi tunaweza kumpa mwenzetu chakula, nk. Usitoe pesa madhabahuni isiyokuwa na maelezo ya nani anahitaji sadaka zetu.
KILA kitu kipo wazi kwa aliyemuumini apotoki, zaidi unaweza jifunza zaidi kuhusu sadaka.Mayatima,wajane,wagonjwa, wafungwa na wahitaji wengine awajaachwa hewani namna ya kuwasaidia. Labda utambue kuna sadaka za aina gani. Mungu apokei cash yeye ni toshelevu bali upokea nia ( utoaji )
 
Humu kuna watu ni wabishi mno,

Wana akili ila hawataki kujifikirisha,
Ukitumia hio akili kichwa kitauma?
Mungu akukupa akili iwe mzigo.

Dini ni biashara kama biashara zingine..

Hakuna cha padri,mchungaji ama nani,wote yatupasa kufanya kazi.

Ni upuuzi kuona kanisa linakandamiza,linawanyonya masikini mpaka tone la mwisho bila hata huruma..

Mungu wetu sio masikini kiasi hichi wala haihitaji hizo pesa...ni wapuuzi tu wachache.
 
Sadaka unazopeleka kwa mizimu, je hiyo mizimu inatumia wapi sadaka? Unapoenda kuwasaidia yatima na wajane umetenda jambo jema kwa Mungu, unapowasaidia wazazi wako ni jambo jema mbele za Mungu na ndio anavyotaka lakini usijeacha kupeleka sadaka madhabahuni kwa kuhani ni agizo la Mungu kama unaamini katika Mungu, na kama uamini endelea na njia Yako, na ni kweli kuhani atakula lakini ukipatwa na shida ya kiroho mbona huwa hujiulizi ulizi, maswali ya sadaka yangu inaliwa??
Kuhani hata kwenye mazishi atazunguusha bakuli TU, hajali ni msiba au sherehe bakuli liko palepale, unapoumwa huhitaji maombi ya mtu mwingine, bali unatakiwa kumshukuru na kuamini kuwa Mungu anaujua mwisho wako na kupata msaada wa matibabu, chakula, na faraja kutoka kwa wenzio (sadaka).
 
Humu kuna watu ni wabishi mno,

Wana akili ila hawataki kujifikirisha,
Ukitumia hio akili kichwa kitauma?
Mungu akukupa akili iwe mzigo.

Dini ni biashara kama biashara zingine..

Hakuna cha padri,mchungaji ama nani,wote yatupasa kufanya kazi.

Ni upuuzi kuona kanisa linakandamiza,linawanyonya masikini mpaka tone la mwisho bila hata huruma..

Mungu wetu sio masikini kiasi hichi wala haihitaji hizo pesa...ni wapuuzi tu wachache.
Wanakuimbisha wimbo wa toa Ndugu toa Ndugu.... kipuuzi kabisa ili waokote hela yako.
 
Ibrahim alitoa sadaka kwa mungu. Wana wa Israel walitoa sadaka kwa mungu, daudi na Suleiman pia. Halafu unakuja hapa kutwambia tusitoe sadaka[emoji706][emoji706]
Kondoo aliyemtoa sadaka kala Mungu au watu waligawana nyama wakala wenyewe?
 
Naona kama vile mleta mada ndo haelewewi
Hebu nieleweshe, baada ya kuitumbukiza ile hela yako pale kwenye kihenge madhabahuni Mungu ataipataje, itapaa, Mungu atashuka kuichukua au itapotelea wapi? Tena wale mabaladhuli wala sadaka wanakutaka uitoe hata mkono wako wa kushoto usiione wala kujua ni bei gani, maana yake msijue mmetoa ngapi na hakuna audit wala record yoyote. mazuzu yanatoa na kuondoka zao. Mabaladhuli wanakwambia kuwa "Mungu atakuzidishia pale ulipotoa", Baada ya kuona kuna dalili ya maskini kuhoji kwanini wanakamuliwa, wanawajibu kuwa "aliyenacho ataongezwa" Hii yote ni mistari iliyochomekwa na wala sadaka.

Ukweli sadaka pekee itakayokuongezea muda mrefu wa kuishi na baraka ni ile unayowapa wazazi wako tu basi, kwakuwa kile walichokutendea huwezi kuwarudishia hata ungekuwa mwema au tajiri namna gani. Watu wengine wote unaweza kuwafanyia kama walivyokufanyia isipokuwa wazazi na Mungu tu.

Watu wengi huwa hawajui kuwa tendo la ndoa sio starehe hata kidogo, ni tendo la hatari sana na baya sana ingawaje watu wanalifurahia lakini wanaumia bila kujua. Yafuatayo ndiyo mabaya ya sex ambayo yanampa hadhi baba kuitwa baba na kustahili sadaka za watoto wake:

1. Kumtafuta na kumpata mwanamke wa kuoa ilikuwa na inapaswa kuwa ni shughuli nzito sana kwa wanaume. Atatabika sana hadi ifikie wakati anaweza kulala nae na kumpanda.

2. Tendo la ndoa (sex): Tendo hili ni la hatari mno kwa mwanaume kwakuwa linatumia nguvu nyingi sana za mwanaume, nguvu anayopoteza mwanaume kusex hadi kutoa mbegu mara moja tu ingeweza kutumika kwa kutembea umbali wa maili 11. takribani kilometa 16 hivi kwa miguu. baada ya tendo la ndoa baba atajisikia kuchoka sana, kiu, njaa na mwepesi. Baba ni lazima afike kileleni ili kutoa mbegu ili azae, lakini mama sio lazima afike kileleni ili kupata ujauzito, hivyo hatumii nguvu nyingi sana kama baba wakati wa tendo.

3. Mbegu (manii): Mbegu za kiume zinatengenezwa kwa protein ile grade I kabisa, yaani protein nzuri ya mwanaume baada ya balehe inakwenda kutengeneza mbegu za kiume, hivyo kusababisha mwili wake kuchakaa kama hatapata chakula kizuri na kupunzika, sababu hii inapunguza kinga ya mwili ya baba kiasi cha kumfanya ashindwe kuhimili misukosuko mingi kama hatapata chakula kingi na bora na matunzo yaliyokamilika. Wengi wanakonda wakati wa honey moon. Jambo hili linawapunguzia kinga ya mwili, kujenga mwili, akili, kuzeeka mapema na umri mfupi.

4. Magonjwa ya ngono: Ili kuzaa lazima baba ufanye tendo la ndoa pekupeku, kwenye huo mchakato wakina baba wengi huwa wanaambukizwa magonjwa mabaya.

5. Kutunza familia. Baba wengi lazima watoke wakatafute na kuleta riziki kwenye familia hata kama wanaumwa.
6. Ulinzi wa familia unamtegemea baba zaidi, ajenge mji na kuulinda.

Hii ndio maana atakuwa baba hata kama alikutelekeza.

Mama: Bila shaka kila mtu anafahamu namna mama alivyochangia hadi uwe ulivyo sasa. tendo la ndoa, mimba miezi 9, kuzaa kwa uchungu, kunyonyesha na kulea usife, usiungue, usitumbukie, usipasue jicho, nk.

mambo haya ndiyo maana Mungu mwenyewe alitoa agizo la kuwaheshimu watu hawa.
 
Wakati wa Yesu mjane alitoa sadaka senti mbili hekaluni Mbele ya Yesu. Na Bwana akasema huyu ametoa zaidi. Ilikuwa hekaluni ( kanisani) na walitoa fedha sio kuku
 
Wakati wa Yesu mjane alitoa sadaka senti mbili hekaluni Mbele ya Yesu. Na Bwana akasema huyu ametoa zaidi. Ilikuwa hekaluni ( kanisani) na walitoa fedha sio kuku
hiyo hela ndogo aliyotoa majene alikwenda wapi, umeliwa na nani, ilifanyia nini? utenzi huu umeandikwa na wanufaika wa sadaka, wanajua kuwa maskini kwenye jamii ndio wengi, hivyo waliwatengenezea ulimbo wa kunasia vijisenti vyao walivyovifundika kwenye pindo la nguo. Yaani hawaachi kitu, lete hata hiyo!!!! kwakuwa wa hivyo wako wengi basi wakikusanya senti 10 kwa watu 3,000,000 kila wiki kila mwezi na kila mwaka kwa miaka 20 wako mbali. Kaka jambo kubwa kwako ni uzito wa imani yako kwenye kila jambo. Imani yako kwa Mungu ikiwa kubwa ni sawa na kuwa Antena nzuri ya dish inayonasa mavimbi mengi na kupata sauti na picha angavu (crystal clear) lakini ukiwa na imani legelege ni sawa na kuwa na antena ya chadema inayonasa mawimbi hafifu ya sauti na picha na kupata chenga nyingi wakati wenzako wakifurahia matangazo. Juhudi, maarifa na Imani yako ndio itakayo kukutanisha na mungu, kukuponya na kukutendea miujiza kwenye maisha sio sadaka. Hata hiyo sadaka utaiona inafanyakazi kama juhudi, maarifa na imani yako ni kubwa na thabidi. Yaani kutoa sadaka ni "confounding factor" kwenye kupata mema. Haiwezekani utoe sadaka na kwenda kulala halafu usubiri kupata mazao mengi yaliyoletwa na sadaka.

Imani kubwa aliyonayo mtoto kwa wazazi wake ndiyo iliyosababisha anyonyeshwe, alishwe, atawazwe akijichafua, avalishwe, atibiwe na kusomeshwa bure na wazazi wake bila hata ya kuwaomba. Mtoto aliamini kuwa yule ndiye baba na mama yake na kuwakataa watu wengine hata kama wanafanana na baba na mama yake, hata kama walikuwa matajiri kuliko wazazi wake, hata kama walikuwa na nyumba nzuri kuliko ya wazazi wake. Mtoto aliamini na kukubali kuwa hawa ndio wazazi wangu sio wale, hapa ndio kwetu sio kule kwa wale. Hivyo, baada ya imani kubwa hii ya mtoto kwa wazazi wake, na wazazi walimpa vitu bure kabika bila kuomba. Wazazi wakajitwisha jukumu wao wenyewe la kumlea mtoto wao bila ya mtoto kuwaomba wamlee wala kumnunulia nguo ya sikuu, na mtoto kazi yake ni kusema asante baba, asante mama, asante kaka, asante..... Imani kubwa kwa Mungu ndivyo inavyofanyakazi pia, kazi yako kubwa ni kutumia uwezo aliokupa Mungu kwa 100%, kumshukuru na kumwamini Mungu tu baaaaaaasi!!! hakuna sadaka kwaajili ya Mungu, bali kuna sadaka kwaajili ya binadamu wenzako na viumbe wengine wenye uhitaji.
 
Nakaribia kukuelewa kumbe biblia huikubali, Kama huiamini itanisaidia namna ya kujadiliana, nilidhani naongea na mkristo asiyejua umuhimu wa kupelekea sadaka madhabahuni
 
Kama ungeamini biblia inasema wahashimu baba na mama yako update heri, uishi siku nyingi Duniani, hizi ni baraka za kimwili kwa yeyote atakayefanya awe mwabudu Shetani mchawi atazipata.

Yesu akaongeza: wapeni watu vitu na ninyi mtapewa na watu vitu vya kujazwa na kushindiliwa na kusukwasukwa. Hizi ni baraka kwa kila atakaewasaidia watu na yeye atasaidiwa na watu naam zaidi ya msaada aliotoa

Lakini kutoa madhabahuni Anasema: na sadaka yako ilipo ndipo itakapokuwepo na roho yako, ukitoa kwenye mashabahu ya kweli unatakaswa na ukifa roho yako itakwenda huko, ukitoa kwenye mashabahu ya majini, mizimu, masanamu nk roho yako itakwenda hukohuko utakapokufa

Kwa hio kuwasaidia wazazi, ndugu jamaa, marafiki na mtu yeyote mwenye shida kunakupa baraka, heri za hapa Duniani, hazikupeleki mbinguni, lakini kwenye madhabahu unamtolea Mungu mwenyewe, anabariki mwili na roho yako
 
kwenye uzi huu sikusudii kupinga vitabu vya dini, lakini siwezi kuacha kusema kuwa kwenye vitabu hivi kuna ukweli ambao umechanganywa na uongo kwa maslahi ya kundi fulani, lakini kuna ukweli ambao unahubiriwa vibaya kwa maslahi ya kundi fulani na kuna ukweli ambao unatumiwa vibaya kwa maslahi ya watu fulani. Lakini ni kweli pia kuwa Mungu ni mkubwa sana na mambo yake ni mengi saaana kuweza kuandikwa yote na mtu au kundi la watu yakaisha na kuwekwa kwenye kitabu kimoja tu ambacho unaweza kukibebea kwapani kama ukipenda.

Ukweli wote kuhusu Mungu haujulikani na hakuna awezae kuujua na kuuandika, bali ukubwa wa Mungu utauona, kuusikia, kuuonja, kuunusa, kuupapasa na kuu feel tu unapojiangalia, jisikia, kujigusa na ku ji feel wewe mwenyewe, viumbe wengine, anga na ardhi. Kilichoandikwa kuhusu Mungu ni kidogo sana kuliko mbegu ya haladali. Kuna watu wapumbavu wanaosema eti wanautafuta uso wa Mungu, wapuzi sana hawa ambao wanakimbia hata mende, mijumsi, nyoka, simba, na nge. kama unamkimbia jongoo unawezaje kusimama mbele ya uso wa Mungu aliyeviumba viumbe vyote wakiwemo mende, nyoka, panya, papa, tembo na mamba? Waache upuuzi wa kuutafuta uso wa Mungu.

Kifupi, Mungu yupo hata bila vitabu ambavyo hakuviandika yeye. Kuna siku nilimuona mtu anatumia kitabu cha Mungu kuagulia watu nyota zao!!! nikasema, heeee ni hivi vimo?
 
Kama ungeamini biblia inasema wahashimu baba na mama yako update heri, uishi siku nyingi Duniani, hizi ni baraka za kimwili kwa yeyote atakayefanya awe mwabudu Shetani mchawi atazipata.

Yesu akaongeza: wapeni watu vitu na ninyi mtapewa na watu vitu vya kujazwa na kushindiliwa na kusukwasukwa. Hizi ni baraka kwa kila atakaewasaidia watu na yeye atasaidiwa na watu naam zaidi ya msaada aliotoa

Lakini kutoa madhabahuni Anasema: na sadaka yako ilipo ndipo itakapokuwepo na roho yako, ukitoa kwenye mashabahu ya kweli unatakaswa na ukifa roho yako itakwenda huko, ukitoa kwenye mashabahu ya majini, mizimu, masanamu nk roho yako itakwenda hukohuko utakapokufa

Kwa hio kuwasaidia wazazi, ndugu jamaa, marafiki na mtu yeyote mwenye shida kunakupa baraka, heri za hapa Duniani, hazikupeleki mbinguni, lakini kwenye madhabahu unamtolea Mungu mwenyewe, anabariki mwili na roho yako
kama Yesu alikuwa anaipokea sadaka ya pesa basi alikuwa anaipokea kama msaada kutoka kwa wanaomuamini yeye na kile anachokisema, kihubiri. Lakini kile alichokuwa anakihubiri Kulikuwa na watu walikiamini bila kutoa sadaka na Kuna waliokiwa wanatoa sadaka lakini hawakiamini. Hivyo sadaka ni malipo kwa mhubiri sio kwaajili ya Mungu, Yaani mhubiri apate kula, apate kuvaa, pate kusafiri, apate kusomesha,apate kula na kusaza. Na unaweza kutoa sadaka kubwa TU kama fahari, mbwembwe, kujionyesha, kusafisha uharamia wako TU basi lakini sio kwamba unatoa kwaajili ya Mungu. Mungu na sadaka sio kitu kimoja bro.
 
Wengi wanakuja inbox kuuliza dalili za mtu aliyebarikiwa, Iko hivi. Watu waliobarikiwa wanazaliwa wakiwa wameshabarikiwa, wameumwa na Mungu wakiwa wmebarikiwa tayari. Ni muda ukifika watu wataziona alama na dalili za kubarikiwa kwake. Kubarikiwa hakutegemei sadaka na Wala sakada haisababishi mtu kubarikiwa, mwisho wa sadaka ni wewe pia kupokea sadaka kwa watu wengine ukiwa na uhitaji wa msaada. Ukitoa sana kwa wezakako na wewe utapokea sana kutoka kwa wenzako, sio kutoka kwa Mungu, maana Mungu alishamalizana na wewe kitambo, anachosubiri kwako ni kumshukuru na kumwamini,

Alama kuu za kubarikiwa ni wingi (quantity) na thamani (quality) kuliko wengine au kama wengine waliobarikiwa. Mtu aliyebarikiwa hawazei kuwa na vitu vichache au kukosa kabisa, na mtu aliye barikiwa hawezi kupewa vitu dhaifu hata kidogo.

Mali kuu mbele za Mungu ni watu, mifugo, mazao na busara (hekima). Hivyo, mwanaume aliyebarikiwa ana

1. wanawake na watoto wengi. Au mke mmoja lakini aliyezaa watoto wengi, zaidi 6 na kuendelea,
2. Watoto wema wasikivu, wenye afyav ya mwili na akili na wanaorithi tabia na kazi za baba na mama Yao. Like father like son. Mtu aliyebarikiwa hawezi kuwa na mtoto 1 au 2.
3. Mifugo mingi, inayozaa sana na isiyopatwa na maradhi mara kwa Bara. Mtu aliyebarikiwa hawezi kuwa na kondoo 4.
3. Mavuno mengi sana hata kwa eneo dogo TU la shamba, kame aliyebarikiwa hawezi kuvuna debe 3 kwenye Eka moja ya Mahindi.
4. Hakosi riziki pamoja na kuwa na wake, watoto na Ndugu wengi wanaomtegemea. Watakula na kusaza na ada ya shule hawatakisa.
Hekima na busara kubwa. Ni tegemeo kwa wanajamii katika kutatua mashauuri Yao mbalimbali kwa weledi na watu kuridhika na maamuzi na ushauri wake. Ni kimbilio la wengine pahala pa kazi au mtaani kwake.
 
Sadaka ya Ujenzi, chukua Kadi ya Ujenzi ujenge nyumba ya Bwana Mungu wako...
"Huu Ujenzi tunaufanya kwa ajili yenu na ya vizazi vyenu nyie waumini, watoto wenu ndo watakuwa kisali hapa, hili siyo jengo langu, kanisa siyo la mtu mmoja"... alinukuliwa nabii mmoja.

Sasa nabii mbona akaunti na hata hati ya hilo eneo la kanisa zina majina yako binafsi na si hilo Kanisa??? 😂😂😂

Hii ni biashara ya Ukoo, TB Joshua kakata ringi mkewe kashika hatamu (Mungu anapendelea kweli 😂😂 yaani MKE na MUME wote ni mitume).
Mama naye akikata ringi mtoto ataridhi UTUME 🤣🤣🤣... Yaani kama UFALME na UMALKIA wa Uingereza aiseeee.
Wacha tuendelee kuwa wateja wenu haina jinsi maana MAFUTA na MAJI yenu yanatufanyia UPAKO wa ajabu kwakweli...
Japo katika watu elf 20 tunaokanyaga Mafuta wanaopokea hawafiki 10 lakini unatutangazia kuwa wote tukija tutafunguliwa wewe una nguvu za Mungu wa kweli,, Tukiuliza mbona siye wengine tumekuja mara kibao hatupati UPONYAJI mnasema hatuna IMANI 😂😂😂... Sasa hizo nguvu unazojinadi nazo ni zipi tena???🤓🤓
 
Hata misikiti pia iko hivyohivyo, ina wenyewe. Mama Rwakatare pale mlima wa moto ni pake, Mwingira ni pake, mzee wa upako ni pake, nk. sadaka zote ni zao na mambo yao. Wajinga hawatakwisha usiyachome manyoya yako. Hebu fikiria mwenye tangu Yesu afe hadi leo zaidi ya miaka 2000 lakini wajinga tupo hadi leo.
 
Back
Top Bottom