Anaitwa Nairobi fly,
View attachment 3242615
Anazalisha kemikali yenye sumu ambayo ikikutana na ngozi ya binadamu, basi ngozi inaungua na kuacha blisters.
View attachment 3242616
Hii kemikali inaitwa pederin. Unapomuua huyu mdudu wa vidole vyako basi hii kemikali hubaki kwenye vidole vyako popote utakaposhika kwenye mwili wako basi pata ungua ndani ya saa 24,
Vipele vyenye mchanganyiko wa maji maji na usaha vitajitokeza ndani ya saa 24,
Mdudu huyu Kwa kawaida hukaa mashambani chakula chake ni crop pests ila huja kwenye mazingira ya binadamu Kwa kuvutiwa na mwanga wa taa.
Huzaliana zaidi nyakati za mvua.
Pederin
Kwa sasa tafiti zinaonyesha kemikali hii ni muhimu Kwa kupunguza makali ya saratani na huenda ikatumika kutengeneza dawa Kwa magonjwa ya saratani.
Experience
Nilikutana na visanga vya huyu mdudu huko Arusha, wapo wengi sana, nilishuhudia mwanafunzi aliyemsaga huyu mdudu Kwa peni then akajisahau Ile peni akapeleka mdomoni, kilichomtokea kesho yake ni huruma tupu.
Tupe experience yako!!!
Reference
Narquizian R, Kocienski PJ (2000). "In The Role of Natural Products in Drug Discovery"