Usiufate Moyo sana hasa linapokuja swala la Biashara na Utafutaji

Usiufate Moyo sana hasa linapokuja swala la Biashara na Utafutaji

Mkuu hivi umeshajiona mfuko hauruhusu kusomesha mtoto international school

unajifanya kujikaza kisabuni,huwa unachokitafuta hasa hasa ni kitu gani mkuu?

Umeshaona biashara unayofanya haitoshi kulipa bills,kwanini usijiongeze ukaongezea

na vitu flani flani hapo ofisini ukauza, mkuu kwenye ushonaji ni vijora tu vinatoka mkuu?

kama vijora ndio habari ya mjini eneo ulilopo,Fanya kitu kimoja sio kila mteja anaweza

nunua kijora kwa cash, Usikopeshe ila kodisha vijora,mbona watu kwenye harusi wanakodsha magauni? kwanini usikodshe wewe vijora?

vijora ni simpo havna material mengi,shona vijora size tofaut weka hapo kodishia waswahili wenzetu,anakichukua anaenda kivaaa akimaliza anakirudsha,ukiwa na wateja aina zote kuanzia wa Cash mpka kukodisha kipato lazima kiongezeke mkuu.

tumia mbinu zote kuwaridhisha wanaokuzunguka,ukimaliza hiyo basi inabaki kukinga tu, kama ikigoma sio mbaya kuhama hiyo frem ukatafuta frem za 100k au chini yake zipo na zipo sehemu nzuri tu.
Nakushukuru Sana, maana pia umenipa idea nzuri Sana ngoja nione nafanyaje. Mungu akubariki Sana.
 
Maana nilikuwa hata sielewi nashona nguo zenye ubora hasa mashati ya kiume lakini sipati wateja. Au kwa sababu nimebase kwenye mashati ya vitenge na batiki? Labda pia nianze kuchanganya.
 
 
Je wat
Binafsi nimejifunza pakubwa Sana na hongera sana. Sasa vipi kuhusu Mimi mwenye ofisi ya kushona nguo na eneo langu si la kishua but nalipa Kodi 150,000 je nikisema Leo nianze kushona vijora kwa kuwaridhisha wateja wanaonizunguka kwa 5,000 ntamlipa nini fundi, ntalipa nini umeme, ntalipa nini usafi na faida ntaipataje? Naomba unishauri ndugu.
Je wateja waliokuzunguka wanataka vijora? Kama ndio basi shona uuze huku pia ukiendelea na kushona hizo za bei ghali
 
Unaweza usielewe kichwa ya habari ila maana yangu ilikua ni moja tunapoongelea moyo tunaongelea kile kitu unachopenda, katika vile tuvipendavyo ndio vina fursa nzuri ndani yake.

Nimewahi na nitaendelea kusema unapofanya biashara au unapotaka kuanzisha biashara fata au angalia moyo wako unapenda nini,maana kwa kufanya hivyo kuna faida 1 kubwa ndani yake.

Faida pekee ya mimi kushauri watu wafanye au waanzishe biashara kutokana na vitu wanavyopenda ni ili aweze kuwa "mvumilivu" biashara haiwezi kwenda bila uvumilivu,

kwanini? kwenye biashara (hasa mwanzoni) huwa ni pagumu sana kufungua biashara kukaa mwezi mzima hujauza kitu ni jambo la kawaida sana, kukaa miezi hujauza kitu ni jambo la kawaida mno, sasa utawezaje kudumu na hiyo biashara kama hukuipenda?

Unapofanya kitu ulichokipenda ni rahisi kukivumilia na kuwa subira nacho ukiamini ipo siku mambo yatabadilika.

Lakini kuna kitu huwa hatuambiani na mimi napenda niwambie ili isije tokea mtu akasema nimekua motivational speaker nisie ongea au andika uhalisia wa biashara.

Katika haya mahaba yetu na biashara tunazotaka zifanya au tunazozifanya,Je umewahi kujiuliza kama hapo unapopapenda pesa ipo au haipo?

Yawezekana umeshafahamu unachokipenda eneo ulilopo pesa hamna na ukisema uende fungua hiyo kitu eneo lingine hutatoboa, ufanye nini sasa?

Tunafungua biashara ili tupate pesa tufanye maisha yetu,lakini hapa kwenye biashara gani ya kufungua wengi wetu tunaangalia zaidi mapenzi yetu na jambo husika.

Tunasahau kuangalia uhitaji wa hicho tunachokipenda eneo hilo, Nina rafiki angu mmoja ni mdada yeye ki ukweli ana Kipaji ya kusuka, ana suka kiasi kwamba akikusuka unaweza ambiwa umevalishwa wigi.

Akawa ananiuliza namna yakufungua salun nzuri ili asuke watu binafsi nilimuuliza ana uhakika wa wateja wangapi wa kusuka kwa siku/wiki akanipa jibu na kiasi anachopata kisha Tuka calculate pamoja tukatoa gharama za matumizi yake kwa siku hela iliyopatkana ni ya kawaida sanaaaa..

Lakini pale pale alipo kuna fursa nyingine nzuri sana ambayo haitaki mtaji mkubwa nikamshauri nikamwambia pita na hii kitu ifanye hiyo kusuka iweke ''pending" utairudia tu wote twajua "kipaji hakipotei" kweli akafanya hivyo Maisha yanasonga.

Muda huu kaniambia anakaribia kufikia malengo yake ya kufungua saloon aliyokua akiiwaza na kurudi kwenye biashara aliyokua akiipenda siku zote.

Hii maana yake nini? Tunapotaka kufanya biashara tuangalie nini watu wanahitaji kwa wakati huo, usiangalie nini wewe unahitaji au nini wewe unaweza au unapenda.

Achana na kufanya biashara unayopenda fungua biashara wanayopenda watu"wateja" utafanikiwa, yawezekana unapenda sana biashara ya nguo special lakini eneo ulilopo watu wanavaaa sana mitumba, Uza mitumba Special achana nazo.

Huu mwanzo tuutumie kutafuta pesa ili hizi pesa zitufikishe kufungua biashara tulizokua tukiziota na kuzifikiria katika maisha yetu.

Hakuna namna tutaweza toboa haya maisha kama tusipofanya wanachotaka waliotuzunguka ''jifanye mjinga upate pesa kwanza'' binafsi ni mfanya biashara nina fanya biashara tofauti tofauti lakini katika hizi biashara zote ninazofanya hakuna hata biashara 1 niliwahi iota kwamba siku 1 nitakuja ifanya.

Mpaka na leo hii nabangaiza kutafuta pesa za kuja fungua biashara yangu ambayo ndio nitakayosema YES hiki ndicho nilikua nakihitaji, kwasasa hivi biashara zote ninazofanya nafanya kwasababu nimeona eneo hilo linahtaji hicho kitu.

Muda utafika nitafungua biashara ambayo mimi kwanza naipenda, moyo wangu upo hapo sasa kazi yangu itakua kukushawishi wewe upende ninachofanya, taka usitake utanunua maana nitakushawishi hadi uipende.

ila kwasasa sina kiburi hicho bado sijafikia ndoto hizo, umeshawahi ingia maduka ya TV huko mjini ukakuta wanauza BRAND aina 1 tu,duka zima lina tv lets say za SONY tupu, siku nzima wanaweza wasiuze na hawashtuki its ok with them.

Duka la jirani kuna mtu anauza TV aina zote,sony,hitachi,nikai,bravo,nk unafkiri huyu mwenye duka la sony tupu hatamani kuuza kama mwenzake? unafikiri kwanini hashtuki wala mshipa hautikisiki kuona mwingine anauza zaidi?

kwasababu ameshavuka level za kufanya wateja wanataka nini, yupo kwenye hatua za kufanya biashara anayoipenda yeye kisha akushawishi utumie anachoona yeye ni bora,utake usitake utanunua maana hauzi kitu kingine tofauti na anachokiamini yeye ni bora.

Kwa sisi ambao hatujafika level hizo,tuache mahaba na vitu tunavyopenda tujikite kufanya biashara na vitu wanavyopenda waliotuzunguka. Tukizipata pesa tutakuja kufanya yale tuliyoyapenda.

Unapika mama ntilie wateja wako wengi n wa ugali, kwann usipike ugali tu na uachane na huo wali unaobaki kila siku?

Fine unapika wali wateja wamezoea wali wa buku, kweli huwezi kuuza wali BUKU kwasababu mchele unaonunua ni SUPER, acha mbwembwe za kununua mchele SUPER wateja wanataka wali wa buku tafuta mchele kilo buku jero,nenda huko tafuta mchele grade Z wapikie wali wao wauzie BUKU. Acha mbwe mbwe za kupika mchele wa mbeye SUPER kama unampkia mumeo home.

Unauza Supu 2500 wakati wateja wanataka supu za buku, acha kununua nyama kilo 8000 hutoweza ona faida,nunua nyama machinjioni kilo 4000 uzia wateja wapenda supu za buku, usi complicate mambo, kwasasa upo kwenye hatua zakutafuta pesa,

wape wateja bidhaa wanayotaka wao si unayotaka wewe, kweli Chakula kizuri ni sabuni ya roho (hiyo ndoto yako itatimia siku 1) utafungua mgahawa utauza vyakula vizuri super Grade, ila kwasasa Mahaba pembeni,Fanya kile kinachohitajika kwanza.

Mifano ni Mingi ila thread itakua ndefu sasa..
Hii ni rule no 1 unapoingia katika soko lolote! Wasome wateja wanata nini kwanza!

Kwa Tanzania watu wengi huangalia kwanza bei kuliko chochote kile!! The cheaper the price, the higher your sales and profit.

Once i mastered this rule, my journey became easy.
 
Ila umeongea point muhimu sana. nina ndugu yangu yeye tangu makuzi yake alikua anapenda sana simu, yaani S ngapi itoke hata kama hana hela atanunua hata ya wizi tu ilimradi awe nayo.
Sasa kapata goli kinondoni kalitengeneza ile haswaa push door na vitu kama hivyo.
Kutokana na mapenzi yake na simu akajiingiza direct na biashara ya simu na vitu vyake. Japokua kwa mazingira yale na biashara hiyo haviendani hata kidogo. Jamaa karidhika na analipa kodi kubwa ukimtembelea ukimuulizia biashara inaendaje Daah utamuonea huruma. lakini still bado ana moyo mambo yatakua sawa. Ila akilini unawaza kabisa huyu hili goli angefanyia biashara nyingine mfano vyakula angeuza sana kutokana na mazingira haya yaliyopo.
 
Back
Top Bottom