Usiweke Hela benki zisizokuingizia chochote, Weka Hela zako kwenye masoko ya Hisa au fungua miradi

Usiweke Hela benki zisizokuingizia chochote, Weka Hela zako kwenye masoko ya Hisa au fungua miradi

BOB LUSE

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2014
Posts
3,738
Reaction score
3,199
Kawaida ya Waajiriwa wengi, kuweka Akiba, Saving account kwenye benki zetu, kwaajili ya usalama. Account hizo kuna ledger fee unalipa, huingizi chochote.

Nikushauri, wekeza kwenye masoko ya Hisa, akiba yako itaongezeka Kila mwezi, Kwa riba utakayokuwa unalipwa.

Usipate hasara, kusubiri mpaka ustaafu ndio ufungue Miradi, utafeli, Biashara Zina hatua za kujifunza na kufanikiwa, ambazo zinachukua miaka sio chini ya mitatu n.k.

Amka usingizini. Mungu akubariki.
 
Kawaida ya Waajiriwa wengi, kuweka Akina,Saving account kwenye benki zetu,kwaajiri ya usalamq.Account hizo Kuna ledger fees unalipa, huingizi chochote.

Nikushauri,Wekeza kwenye masoko ya Hisa,akina yako itaongezeka Kila mwezi,Kwa riba utakayokuwa unalipwa.

Usipate hasara,kusubiri mpaka ustaafu ndio ufungue Miradi, utafeli, Biashara Zina hatua za kujifunza na kufanikiwa, ambazo zinachukua miaka sio chini ya mitatu n.k.
Amka usingizini . Mungu akubariki
Uko sahihi nilipoteza muda wangu kuweka hela benk na kuanza kujenga..nilifanya kosa kubwa mno kumbe ningepaswa nijiimarishe kibiashara ndo niweke hela benk na kujenga
 
Ila kwa soko la hisa la kwetu, mh! bora ninyamaze.

Nimeweka fedha zangu nyingi kidogo kwenye Voda, mpaka leo wameingia mitini hatupati kitu, wala hatuwezi kuziuza hizo hisa, tumebaki njia panda.

Natamani hata fedha yangu ningeinunulia kuku au samaki nikala nikashiba mwenyewe,
 
Uko sahihi nilipoteza muda wangu kuweka hela benk na kuanza kujenga..nilifanya kosa kubwa mno kumbe ningepaswa nijiimarishe kibiashara ndo niweke hela benk na kujenga
Hata Mimi nimefanya Makosa hayo, unaona fahari kuona cash ipo benki, unajisikia upo salama, kumbe ni ujinga, unanufaisha benki tu.
 
Ila kwa soko la hisa la kwetu, mh! bora ninyamaze.

Nimeweka fedha zangu nyingi kidogo kwenye Voda, mpaka leo wameingia mitini hatupati kitu, wala hatuwezi kuziuza hizo hisa, tumebaki njia panda.

Natamani hata fedha yangu ningeinunulia kuku au samaki nikala nikashiba mwenyewe,
Hukupata Washauri wazuri wakati wa kununua hisa, ulipaswa ununue Treasury bond, thamani na Hela yako haipotei na inapatikana unapoitaka. Ndio Maana uliona hisa za voda hazikununuliwa zote, watu walijua hawana kipya. Unaona akina Rostam anauza hisa, elewa hakuna faida huko.
 
Kuliko nikanunue hisa huko DSE si bora niweke hela zangu CRDB maana DSE huko hamna volatility yeyote
 
When you save money banks smart people use your money to make more money..
Ukijifunza kuwekeza utapata matunda watz weng wavivu wanafikiri ukisave ndo unakua salamaaa kiuchumi.. save kiwango kidogo wekeza kiwango kikubwa..
Ndio Maana Watanzania wengi wenye Elimu ndogo ni risk taker, wanafanya Kila Ina ya Biashara, hawana muda wa kujilinda Kwa kuweka kitita benki kisichozalisha, matokeo Wana maisha mazuri na free stress, Kuliko wasomi, wanaosubiri pensheni waongezee ndio wawekeze, uzoefu wa Biashara zero, matokeo ni kufeli pakubwa.
 
Unaweza usijenge hela ukaingiza biasharani na ukaishia kuichoma vile vile mwisho ukajikuta huna nyumba wala biashara
Ndio Maana kwenye Biashara una asses risk, sio Kila Biashara unafanya, zipo unazofanya mtaji ukiwa salama, Mfano una kiwanja, umeanza na chumba Cha biashara. Huiapoteza kiwanja, mradi ukopotea.
 
Kuliko nikanunue hisa huko DSE si bora niweke hela zangu CRDB maana DSE huko hamna volatility yeyote
Stock exchange ziko kampuni ambazo Toka ianzishwe hisa zake zinapaa kama TBL,TCC. Kuna security/ Treasury bond, jishughulishe kupata Elimu hizo, utakuja kunishukuru. Mwenyewe niliamini hivyo, nimeona hasara niliyopata, ndio Maana nafundisha watu hapa buree.
 
Back
Top Bottom