Unawekeza kwenye dhahabu kwa kuipata wapi? Hapo ni sawa na kutunza fedha ila sio kuwekezaz crypto inaweza panda bei na ikawa stable zaidi ya mara 100 ndani ya mwaka mmoja ila dhahabu haiwezi kupanda hata mara mbili ndani ya miaka mitatu ingawa iko stable.
Crypto unanunua hela ndogo unahold baadae unauza kidogo kuirudisha hela yako na faida alafu unaacha zile coin zikae. Yule Mwingereza aliyenunua SHIB za $ 8,000 mwaka jana akaziuza mwaka huu kwenye transactions nne za $ 1, 200,000 kila moja amepata faida mara elfu ngapi sijui. Na bado kuna mamilioni kayaacha kwenye wallet yake. Alikuwa mfanyakazi wa store gani sijui na kwa mwaka asingeweza kupata hata $ 100,000 ila sahivi kastaafu kazi na miaka yake 35.
Sasa kwa dhahabu hilo haliwezekani. Alafu mafuta hayapandi thamani zaidi, kwa sasa yana bei kwa kuwa OPEC walishindwa kukubaliana ila hata yapande vipi hayazidi hapa mara mbili ya bei.