Usiyaamini Machozi ya Mamba "Akilia Ujue Ana jambo Lake"

Nyamsusa JB

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2015
Posts
567
Reaction score
1,564
Habari Wanajanvi na Poleni na Msiba Mkubwa uliolikumba Taifa letu.

Tumekua tukiamini kila ukiona Mtu au Mnyama anatokwa na Machozi basi kaumizwa au ana huzuni.

Tunasahau sana kua kuna vitu viwili tu viwezavyo kumfanya Mtu au Mnyama Kutokwa na Machozi ama Kulia navyo ni Utamu au Uchungu.

Kwenye hili la Uchungu lipo wazi kua mtu anapopatwa na Uchungu na Huzuni basi huweza kulia na Kutokwa na Machozi.

Kwenye hili la Utamu na Furaha huwa halielewekieleweki kua kama ni jambo pia linaweza kumfanya Mtu au Mnyama Akalia na Kutokwa na Machozi.

Sasa basi napenda kumtambulisha kwako Mnyama Mamba na Machozi yake.

Ukimuona Mamba Analia/Anatoa Machozi basi tambua ana Jambo lake.

Ukimuona Mamba Analia/Anatoa Machozi ujue kuna Utamu anaupata.

Ukimuona Mamba Analia/Anatoa Machozi Ujue hayo sio Machozi ya Kweli bali ni ya Kutafuta Huruma ya Kinafiki.

Ukimuona Mamba Analia/Anatoa Machozi Ujue anaweka kilainishi Machoni Pake ili Aweza kuona Vizuri Kitoweo chake.

Ukimuona Mamba Analia/Anatoa Machozi Usidhanie ana huzuni, na Huruma huu ndio wakati anatafuna Kichwa cha Kitoweo chake

Huyu ndie Mamba ni Mjanja mjanja sana na Hutumia Machozi na Huzuni isiyo ya Kweli Kuahadaa Ulimwengu.

Kimtoacho Mtu Machozi sio Uchungu na Huzuni tu bali Hata Utamu na Furaha vyaweza Pia.

Tuwe Makini.
 
Kwahiyo huyo mamba ni nani sasa,unauitusi hadhira sio?
 
Kwani Mkalimani anasemaje kuhusu hili?
Mkalimani huyu hapa
  • fake cry
  • fake tears of regret
  • shed phony tears of sorrow
  • crying of grief that are hypocritical
  • show sadness that is not real or sincere
 
Mikuki yenye ncha kali imewekwa pembezoni mwa kitoweo kama ulinzj, sasa mamba anakazi ya kuitoa kisha ndo apate kitoweo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…