Volatility
JF-Expert Member
- Aug 22, 2018
- 3,935
- 7,513
MGHWIRA AMTAKA DC SABAYA KUMPA TAARIFA MSAFARA WA LISSU KUSHAMBULIWA
19 Aug 2020
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, ametoa kauli rasmi ya serikali kuhusiana na vurugu zilizotokea katika mji wa Bomang'ombe wilaya ya Hai wakati mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Tundu Lissu alipofika wilayani humo kutafuta wadhamini.
Katika taarifa hiyo rasmi aliyoitoa leo Agosti 19, 2020, mkuu huyo wa mkoa ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo, amemtaka mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, kumpatia taarifa ya maandishi ya namna alivyoshughulikia suala hilo.
useless crisis management initiative.