Usiyoyajua kuhusu Biashara ya Simu za Kariakoo, ukijua haya utakuwa mjanja…
Hii biashara inabidi uwe na cash ya kutosha kupambana na changamoto zake. Ukiwa na hela za mawazo ni biashara ya kukupa stress
 
Simu za "refurbished" ni simu ambazo zimetumika hapo awali lakini zimetengenezwa upya na kuuzwa tena. Hii inamaanisha simu hizo zimepitia mchakato wa ukaguzi, matengenezo, na kusafishwa ili zionekane na kufanya kazi kama mpya.

Mchakato wa "refurbishing" unaweza kujumuisha:

• Ukaguzi wa kina: Kila sehemu ya simu huangaliwa kwa kasoro au uharibifu.

• Matengenezo: Sehemu zilizoharibika hubadilishwa na mpya au zilizorekebishwa.

• Kusafisha: Simu husafishwa vizuri ndani na nje.

• Kufunga upya: Programu ya simu huondolewa na kuwekwa upya, mara nyingi kwa toleo jipya la mfumo wa uendeshaji.

• Upimaji: Simu hujaribiwa ili kuhakikisha inafanya kazi vizuri.

Baada ya mchakato huu, simu ya refurbished inapaswa kufanya kazi kama simu mpya, lakini kwa bei ya chini. Hata hivyo, ni muhimu kutambua kwamba ubora wa simu za refurbished unaweza kutofautiana kulingana na muuzaji na kiwango cha matengenezo yaliyofanywa. Kuna viwango tofauti vya refurbishment, hivyo ni muhimu kuuliza kuhusu hali ya simu kabla ya kununua.
 
Nili nunua simu refab line 2...baada ya mwezi slot ya simcard moja ikafa. Inasema emergency call tu. Bhas nikarudisha simu maana warranty ilikuwa mwaka mmoja. Jamaa wakazingua... Nikaona gharama ya urahisi.
 
Hujatoa siri mkuu, waambie mnauza used nyingi ambazo IMEI number zimechezewa..wajue status ya OFFICIAL na CUSTOMIZED.
Kampuni gani mtengenezaji wa simu ana official store Tanzania na anakupa hizo options, hayupo.
Therefore hakuna used official bali wafanyabiashara binafsi, na haimaanishi ni mbovu.
Waambie kuna samsung mnauza S8 hadi S10, nyingine zina charging port type C na nyingine port type B. Waambie zimepigwa spana sana na ndani unakuta betri ya za simu ndogo kama tecno na itel. Simu ni Samsung S9 lkn ndani unakuta betri la tecno.
Hakuna used Samsung S8 au S10 yenye port ya type B, originally hizo simu zinakuja na type C sasa unaanzaje kufanya disassembly uweke type B?
Kwamba type C port ina bei gani ya ajabu mpaka mtu ashindwe kuiweka aweke type B na inabidi abadili mifumo ya simu.

Wewe Toyota Harrier ikifa injini kipi rahisi kati ya kuweka engine ya Harrier na kuweka injini ya Brevis au Crown?
Waambie simu mnazouza, circuit zimefanyiwa looping kwa waya kama redio za mwaka 90 na kusababisha kupata moto sana kama pasi. Zimevalishwa body nzuri nje na boksi nzuri zinazotengenezwa na wachina.
Unawekaje waya kwenye simu. Simu ina hata space ya kuweka waya, au unanunua maredio njiani unaambiwa simu?

Au nyinyi ndio mnaoitwa mnunue Samsung Note 20 ya laki na hamsini na mnatoa hela?

Mara nyingi kinachosababisha simu ipate moto ni replacement display. Vioo vya Samsung kama Note na S series vile OLED vina bei, simu ikipasuka uko nje mtu akauza ikaja used wanachagua wakiweka OLED inakuwa na bei almost kama mpya, wakiweka LCD za kichina inashuka sana bei. Ikija yenye LCD sokoni ina bei ndogo sana na zile lights zinachemka hivyo simu inakuwa na joto lazima.

Sababu ya njaa za wabongo, wananunua simu ya bei nafuu.
Waambie, mkienda dubai mnauziwa kwa mafungu na ndani yake zipo mchanganyiko wa mbovu na nzima...hakuna kuchagua.

Ongezea uhuni mwingine......
Anayenunua simu za mafungu ni jamaa mmoja ametajwa humu. Na sababu wabongo ni wapumbavu, mbumbumbu na vilaza bado watanunua simu kwake.

Simu maduka serious yote yanaiuza kwa 700k to 750k wewe unaambiwa ulete 400k akuuzie unakurupuka mbio unampa hela. Yani ununue IST ya milioni 7 yenye mileage ya 160,000 km, utake kufanana na aliyenunua ya milioni 15 yenye 80,000 km?

Mnaongea sana ila hela za kununua simu mpya latest unakuta hamna, tamaa ya kumiliki brands kubwa mnayo, maduka makubwa yenye warranty na bei kubwa sana mnayajua ila hamuendi.
Sasa mtu unachagua maumivu yako mwenyewe.

Simu used nzuri zipo nyingi sana, mwenyewe mwaka wa tatu huu natumia flagships za mwaka 1-2 nyuma na hazijawahi sumbua. Siwezi fanya upuuzi wa kununua lets say Samsung A25 mpya wakati kwa bajeti hiyo napata S21 clean. Na simu natumia two years so ikifika huo muda naihesabu salvage value ni nill.

Kinachowaponza ni neno moja tu, tamaa.
 
Nili nunua simu refab line 2...baada ya mwezi slot ya simcard moja ikafa. Inasema emergency call tu. Bhas nikarudisha simu maana warranty ilikuwa mwaka mmoja. Jamaa wakazingua... Nikaona gharama ya urahisi.
Ilikuwa simu gani
 
Mpya laki5,used laki5,Kisa Cha kununua used!
Specs.

A25 mpya na S21 used zinaendana bei ila S21 inaizidi mbali sana A25 Infinix iliyochangamka.

Kama unajali lifespan unaenda na A25, kama unataka specs unaenda na S21 provided that simu used unazijua na sio "wakuja".
 
A25 mkuu.
A25 mpya zipo nyingi na sijaona refurb yake bongo hapa sasa ukiuziwa refurb ya A25 ni mshangao. Ungenunua refurb ya S22 au Note 20 sawa maana mpya hamna.

A25 itakuwa uliuziwa used bongo hapahapa.
 
A25 mpya zipo nyingi na sijaona refurb yake bongo hapa sasa ukiuziwa refurb ya A25 ni mshangao. Ungenunua refurb ya S22 au Note 20 sawa maana mpya hamna.

A25 itakuwa uliuziwa used bongo hapahapa.

Inawezekana Chief,

Kwa sababu pale China Plaza kila mtu anasema ametoa dubai. Hivyo ni ngumu kujua
 
Back
Top Bottom