Usiyoyajua kuhusu Senegal

Kilichoniacha hoi, ni siku walipocheza mpira na Misri na kuchukua ubingwa February 2022 (ni kombe la AFCON kama sikosei), mji ulizizima usiku kucha kwa nderemo fataki na hoi hoi. Kitu ambacho sitasahau ni jinsi punda walivyovikwa bendera ya taifa lao. Viva Lions du Teranga!✌✌✌
 
Umeongeza kitu cha muhimu sana mkuu. Raia wana exposure sana hawa waliosoma. Wao kusoma America, France na pengine ni kitu cha kawaida....
 
Ongeza wanawake wao ni matapeli wa kiwango cha SGR! Ukijichanganya na mwanamke wa kisenegalise umekwisha
Wanawake wao wanapenda hela sana. Wanaamini mwanamke ni wa kupewa tu kutoka kwa mwanaume.
Siku ya mwanamke duniani wanawake walio kwenye ndoa Dakar hakuna kupika.... Baba utajua unakula wapi...
 
Duh kumbe Senegal Kuna madili ya vibarua, Huko wanalipa sh ngap kwa degree, diploma,masters,cpa,nk nk
 
Na labda kuongeza kidogo, waSenegal especially wenye uelewa wanamkubali sana JK Nyerere na Tanzania kwa ujumla. In fact kwa mataifa mengi ya West Africa, Nyerere anafahamika na kukubalika sana kuliko kiongozi mwingine yoyote wa Africa.
Nyerere anakubalika sana. Nilichoshangaa ukienda pale kwenye mnara wao wa africa renaissance monument kuna historia ya Wapigania uhuru wengi wa Afrika kama Kwame na wengine. Ila ya Nyerere sikubahatika kuiona. Nikifanikiwa kurudi nitatazama tena kiumakini....
 
Vipi kuhus biashara haramu za madaw ya kulevya wanatumia kwa kiasi gani
Na mbuga za wanyama zipo
Idadi ya mateja ni chache sana. Wa kubahatisha. Ila nasikia biashara hiyo ipo...
Kwa upande wa bangi nilienda kisiwa kimoja kipo maeneo ya Yoff watu wanavuta mpepe hadharani na karibu ya kambi ya jeshi.....
 
hapo kwa shilole inakuaje? Mie najua wimbo wa chura kaimba Snura.
 
Umesahau pia hao jamaa ndio watu wa kwanza kufunguka huko West kabla ya wanigeria. Na ndio wa kwanza kuwa matapeli wa kimataifa wanaigeria wanasubir.
Kwa ujanja ujanja na utapeli , mnigeria anasubiri kwa msenegal. Na wasenegal ndio wamachinga wa Paris, wanauza vitu vya mikononi na ndio pick pockets pia wao na wamorocco.
 
Umesahau pia hao jamaa ndio watu wa kwanza kufunguka huko West kabla ya wanigeria. Na ndio wa kwanza kuwa matapeli wa kimataifa wanaigeria wanasubir.
Labda utapeli huo wanafanyia nje ya mipaka yao.... Kwa hapa sijakutana na utapeli. Na wao wanawaogopa wanaijeria. Wakisikia unaongea kingereza wanakjua umetoka Nigeria ila ukijitambulisha MTZ wanafurahi.
Mabaya yapo kwanza ukifika Airport utapigwa bei za Tax, Utapigwa kwenye clearance, Utapigwa kwenye exchange rate. Lakini ukiwakomalia hawana shida...
Hamna nchi ina zero percent ya uhalifu. Tunatofautiana kiasi....
Na pia wanapenda hela nyingi kwa hiyo usipokua mjanja wa kunegotiate utauziwa bidhaa bei juu. Ukiambiwa elfu 2 kata nusu anza kunegotiate.... Mambo kama hayo yapo....
 
Twende mbele turudi nyuma, mie nimetembea karibu nchi nyingi ulaya na baadhi North na West Africa. Nchi zenye waislam wengi kuna upendo na ukarimu hilo halina mjadala. Guinea Conakry,Algeria, Morocco, Mauritania na Egypt, wizi wizi wa kipumbavu kama wa hapo bongo hamna. Huwezi kuvamiwa nyumbani kwako na panya road. Nachoona uislam wa bongo unaendana na umaskini maana nchi zote nilizotembelea za kiislam wizi hakuna kabisa.I might be wrong.
 
Siku ya mechi world cup wameweka big screen watu wanakusanyika....
 

Attachments

  • 20221129_173959.jpg
    1.1 MB · Views: 14
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…