Usiyoyajua kuhusu Senegal

Usiyoyajua kuhusu Senegal

Kilichoniacha hoi, ni siku walipocheza mpira na Misri na kuchukua ubingwa February 2022 (ni kombe la AFCON kama sikosei), mji ulizizima usiku kucha kwa nderemo fataki na hoi hoi. Kitu ambacho sitasahau ni jinsi punda walivyovikwa bendera ya taifa lao. Viva Lions du Teranga!✌✌✌
 
Kuongeza kidogo,

Senegal ni nchi raia wana uvumilivu wa dini sana. Waislam na wakristo wanaishi kwa amani. Rais wao wa kwanza alikuwa Muislamu mzuri na mke wake mkatoliki mwaminifu.

Ni watu ambao wanasaidiana sana especially wakiwa nje ya nchi. Taasisi za kimataifa wamejaa wengi na wanapenda kusaidiana. Wakiwa nje ya Senegal wao cha kwanza ni Africa. Kwenye kazi Msenegal akiwa na fursa siyo rahisi kukutosa.
Kwao kila mweusi is a brother or a sister. Haijalishi umri.
Ni jamii ambayo dini ya mtu siyo kikwazo kabisa. Ni kawaida kugonga vyombo vyako jamaa akiwa anapiga kahawa yake au soda yake.

Mwisho, ni jamii ambayo raia wake wengi wana exposure na uelewa wa dunia kulinganisha na sisi.

Tanzania tuna changamoto kubwa sana linapokuja swala la kutafuta fursa nje ya mipaka yetu. Hata kutembea nje ya nchi waTanzania bado sana.
Siasa zao kama kwingineko zina mauzauza mengi lakini kuna heshima na Rais akishindwa uchaguzi anafunga virago tuu. Rejea, Abdoulaye Wade.
Senegal ina changamoto nyingi ila ina mengi ya kufunza wengine.

Asante mleta uzi kwa uzi powa.
Umeongeza kitu cha muhimu sana mkuu. Raia wana exposure sana hawa waliosoma. Wao kusoma America, France na pengine ni kitu cha kawaida....
 
Ongeza wanawake wao ni matapeli wa kiwango cha SGR! Ukijichanganya na mwanamke wa kisenegalise umekwisha
Wanawake wao wanapenda hela sana. Wanaamini mwanamke ni wa kupewa tu kutoka kwa mwanaume.
Siku ya mwanamke duniani wanawake walio kwenye ndoa Dakar hakuna kupika.... Baba utajua unakula wapi...
 
Uchumi wa mmoja mmoja ni wametuzidi. Wana matajiri wengi sana na raia wao wapo well off.....

Tunachowazidi ni kuwa uchumi wao mkubwa upo Dakar.
Ukienda mikoani ni hoe hae ila kwa miundombinu mizuri wametuzidi sana..

Tofauti na Tanzania kuna Mbeya, Arusha, Mwanza, Dodoma...
Huku wote wanawaza kuja Dakar....

Ukisoma hukosi hela huku....
Pia raia wao wengi hawapendi kazi ngumu. Vibarua wanatoka Gambia, Guinea n.k...
Duh kumbe Senegal Kuna madili ya vibarua, Huko wanalipa sh ngap kwa degree, diploma,masters,cpa,nk nk
 
Na labda kuongeza kidogo, waSenegal especially wenye uelewa wanamkubali sana JK Nyerere na Tanzania kwa ujumla. In fact kwa mataifa mengi ya West Africa, Nyerere anafahamika na kukubalika sana kuliko kiongozi mwingine yoyote wa Africa.
Nyerere anakubalika sana. Nilichoshangaa ukienda pale kwenye mnara wao wa africa renaissance monument kuna historia ya Wapigania uhuru wengi wa Afrika kama Kwame na wengine. Ila ya Nyerere sikubahatika kuiona. Nikifanikiwa kurudi nitatazama tena kiumakini....
 
Vipi kuhus biashara haramu za madaw ya kulevya wanatumia kwa kiasi gani
Na mbuga za wanyama zipo
Idadi ya mateja ni chache sana. Wa kubahatisha. Ila nasikia biashara hiyo ipo...
Kwa upande wa bangi nilienda kisiwa kimoja kipo maeneo ya Yoff watu wanavuta mpepe hadharani na karibu ya kambi ya jeshi.....
 
Umesahau pia hao jamaa ndio watu wa kwanza kufunguka huko West kabla ya wanigeria. Na ndio wa kwanza kuwa matapeli wa kimataifa wanaigeria wanasubir.
Kwa ujanja ujanja na utapeli , mnigeria anasubiri kwa msenegal. Na wasenegal ndio wamachinga wa Paris, wanauza vitu vya mikononi na ndio pick pockets pia wao na wamorocco.
 
Umesahau pia hao jamaa ndio watu wa kwanza kufunguka huko West kabla ya wanigeria. Na ndio wa kwanza kuwa matapeli wa kimataifa wanaigeria wanasubir.
Labda utapeli huo wanafanyia nje ya mipaka yao.... Kwa hapa sijakutana na utapeli. Na wao wanawaogopa wanaijeria. Wakisikia unaongea kingereza wanakjua umetoka Nigeria ila ukijitambulisha MTZ wanafurahi.
Mabaya yapo kwanza ukifika Airport utapigwa bei za Tax, Utapigwa kwenye clearance, Utapigwa kwenye exchange rate. Lakini ukiwakomalia hawana shida...
Hamna nchi ina zero percent ya uhalifu. Tunatofautiana kiasi....
Na pia wanapenda hela nyingi kwa hiyo usipokua mjanja wa kunegotiate utauziwa bidhaa bei juu. Ukiambiwa elfu 2 kata nusu anza kunegotiate.... Mambo kama hayo yapo....
 
Twende mbele turudi nyuma, mie nimetembea karibu nchi nyingi ulaya na baadhi North na West Africa. Nchi zenye waislam wengi kuna upendo na ukarimu hilo halina mjadala. Guinea Conakry,Algeria, Morocco, Mauritania na Egypt, wizi wizi wa kipumbavu kama wa hapo bongo hamna. Huwezi kuvamiwa nyumbani kwako na panya road. Nachoona uislam wa bongo unaendana na umaskini maana nchi zote nilizotembelea za kiislam wizi hakuna kabisa.I might be wrong.
 
Kilichoniacha hoi, ni siku walipocheza mpira na Misri na kuchukua ubingwa February 2022 (ni kombe la AFCON kama sikosei), mji ulizizima usiku kucha kwa nderemo fataki na hoi hoi. Kitu ambacho sitasahau ni jinsi punda walivyovikwa bendera ya taifa lao. Viva Lions du Teranga!✌✌✌
Siku ya mechi world cup wameweka big screen watu wanakusanyika....
 

Attachments

  • 20221129_173959.jpg
    20221129_173959.jpg
    1.1 MB · Views: 14
Back
Top Bottom