Kambaku
JF-Expert Member
- Nov 12, 2011
- 8,332
- 31,306
Hapo Mbecke wanauza viatu sandals za ngozi nzuri Sana halafu bei poa mno. Wanatengeneza wenyewe design poa SanaThies ni mji ulio karibu na Dakar, mji ule ni wa mzuri kuna samaki wa kutosha. St. Louis mji wa kitalii huu....
M'boro nadhani ni njia panda ya kuelekea Touba huko yani Mbacke....
Ulipata kupita miaka gani mkuu?
Kuhusu Amani na kutokuwa na wizi umesema kweli Sana mkuu. Hawa jamaa wako poa Sana. Wana usalama mno na hawana matendo ya kishetani kwa asilimia kubwa Sana.
Ile shopping mall yao inaitwa Sea plaza, Dakar bado ipo mkuu?