Usiyoyajua kuhusu Senegal

Usiyoyajua kuhusu Senegal

Umesema wanavaa irizi kama bangili si ajabu ndiyo maana no.11 wanaijua Thimba kuliko Yanga.
Hahaha mkuu....

Simba wanaijua kwa sababu kuna wachezaji wa Senegal wamepita hapo. No less no more.....

Hawa hawafuatilii hata mpira kivile.
Nimevaa jezi ya Yanga sana na wengi husema ni jezi ya Brazili.

Ila ya Simba wanaijua.
 
15. Wamekuwa na demokrasia inayokua sana japo Rais wao aliyepita na wa sasa wamejaribu kucheza na katiba kugombea muhula wa tatu kinyume cha katiba.
Ni sahii sana.
Macky Sall anajaribu kubadili katiba ili agombee kwa muhula wa tatu. Kumekua na upinzani mkali kutoka kwa kijana Ousmane Sonko.
Amempa kesi ya ubakaji.
Kila alhamis kuna maandamano na kila akipelekwa mahakamani kuna maandamano.

Cha kushangaza maandamano yao kama uhusiki polisi hakugusi unaweza pishana nao hawana shida...
 
Japo picha tu kiongozi
Hii ni sanamu ndefu zaidi barani Afrika ipp Senegal..

Hapo zinapatikana bendera za nchi zote Afrika.

Wanaiita Africa renaissance monument.

nitashare zaidi....
 

Attachments

  • 20221013_072610.jpg
    20221013_072610.jpg
    731.4 KB · Views: 17
Kulinganisha na bongo,ipi ni nchi masikini kuko yenzie?

Najua GDP tumewazidi,nataka kujua uchumi wa raia mmoja mmoja.
Uchumi wa mmoja mmoja ni wametuzidi. Wana matajiri wengi sana na raia wao wapo well off.....

Tunachowazidi ni kuwa uchumi wao mkubwa upo Dakar.
Ukienda mikoani ni hoe hae ila kwa miundombinu mizuri wametuzidi sana..

Tofauti na Tanzania kuna Mbeya, Arusha, Mwanza, Dodoma...
Huku wote wanawaza kuja Dakar....

Ukisoma hukosi hela huku....
Pia raia wao wengi hawapendi kazi ngumu. Vibarua wanatoka Gambia, Guinea n.k...
 
Back
Top Bottom