Mkuu
Mhandisi Mzalendo salam kwako.
Nimefurahishwa sana na bandiko lako ambalo umeliandika BILA kuinua mabega. Hongera sana (Nawapenda sana Wanyenyekevu). Kama hutojali naomba kukuuliza maswali machache
DINI
Tamaduni za waislam hapa ni tofauti sana na kwetu.
●Uislam ni mtindo wa maisha kwao ni utamaduni wao. Wanauishi uislamu na uislamu unaishi ndani yao.
●Asilimia kubwa hamna ubaguzi wa dini.
SWALI/HOJA
Naomba uweke nyama kidogo yamkini tukapata yakujifunza huku Tanzania
VYOMBO VYA USALAMA NA ULINZI
Unaweza kukaa miezi hata kusimamishwa na traffic usisimamishwe. Unaweza safiri Dar to Mbeya hakuna wa kukusimamisha.
AJALI
Madereva wa Senegal wanapenda kukimbiza sana magari. Sijui wanawahi wapi speed 120 kwao ni kawaida.
SWALI/HOJA
Mkuu kama huko Traffic hawasimamishi magari mara kwa mara JE hizi speed za magari hazisababishi ajali nyingi na maafa kwa watu wengi? Mkuu nimeuliza hili swali kwa mtizamo wa Kitanzania ambako tunaamini kwamba traffic wapo barabarani kutimiza majukumu mbalimbali KUBWA ZAIDI likiwa ni kudhibiti kutokea kwa ajali
Usishangae kukuta mwanajeshi na raia wote wamevaa gwanda wanapiga story.
Au konda kavaa gwanda za jeshi (si za nchi yao) na hakuna shida.
SWALI/HOJA
Mkuu kwa ulivyorleza kuhusu uhusiano wa askari na raia inaonekana ni uhusiano wa kirafiki wenye maadili. Je hebu tuambia vipi hiki KIRUSI cha RUSHWA huko kimedhibiwa kabisa?
UVAAJI WA HIRIZI, SHANGA VIUNONI WAZIWAZI NI KAWAIDA
Usishangae kukutana na mtu kajitwisha hirizi yake na hana muda na mtu. Hii inanikumbusha yule mchezaji wa Simba Pape N'daw kutoka Senegal alikutwa na hirizi kwenye moja ya mechi. Kwao ni kawaida kama bangili.
SWALI/HOJA
Mkuu kwa maelezo yako inaonekana hii nchi ni ya kidini sana SASA hii tabia ya kuvaa hirizi mbona inakinzana na Imani ya Kidini ambayo imetawala kwa sehemu kubwa ya wananchi wainchi hyo?
Ahsante