.......uso kwa uso na mwana JF mwenzangu

.......uso kwa uso na mwana JF mwenzangu

Heaven on Earth

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2013
Posts
37,226
Reaction score
26,687
Mamboz wana cc.........

mmh ngoja niwaambie yalonikuta maana nimejikuta nakutana Live na member mwenzangu bila kutarajia

mie ni mtu wa JF sana hata ofisini huwa wananiita mama wa JF sasa jana niko ofisin
kuna kaka mmoja tunafanya nae kazi..akawa ananiambia hebu nitajie jina lako la JF
nikamkatalia...kumbe na yeye ni member tena active tu

YEYE;akasema wewe utakuwa King'asti
H.O.E; hapana bana sio mimi ila ID yangu hata sikutajii.....
YEYE; King'asti nae mtata yule.....Ila huwa napenda kusoma comments zake
H.OE nikamwambia kumbe wawafaham watu enhe

Nikajua yameisha akaendelea

YEYE:au wewe ni Heaven on Earth
H.O.E:wala sio mimi...ndio nani huyo kwanza maana mi siwajui watu wengi JF
YEYE:Kadada fulani hivi kana majibu ya mkato hako...ila kanaonekana kako charming
H.O.E nikacheka tu nikasema sio mimi......(Sijui kwanini alikuwa anasema "KA")

akaendelea tu

YEYE: au wewe utakuwa amu
H.O.E nikamwambia bana hapana huyo nae ni nani...wote siwajui na mie sio active kihivo
YEYE:Mhh sio active wewe......Unanidanganya Live LIVE
H.OE:Ndio na wote ulionitajia sio mimi..na ID yangu sikutajii

maongezi yakaisha baadae alikuja kwenye desk langu sa mie nishajisahau akaona ID yangu
kachekaje huyo kumbe wewe ndio H.O.E lol...

na mie sijakubali ka umejua yangu na wewe hadi nijue ID yake kuja kunitajia Lahaula kumbe wakati
tunapishana kona za JF na huku Ofisini tunapishana pia....nimecheka sana alivyonitajia ID yake........
na huku tunatanianaga sana.....ni mtu wa karibu pia ...Nilifurahi sana tu

basi siku hizi ananiita H.OE akinitext ndio anasema Heaven on earth......
Ila nilicheka sana tu

Long Live JF
 
Last edited by a moderator:
binamu upo....? naona furaha yako katika muandiko wako!
 
Usichokijua ni kuwa hiyo njemba Ina identity Mbili. Kwa hiyo bado inakuchora. Tehe tehe tehe....
Xmas tamuuuuuuu
 
Usichokijua ni kuwa hiyo njemba Ina identity Mbili. Kwa hiyo bado inakuchora. Tehe tehe tehe....
Xmas tamuuuuuuu

hahahaaa najua tu atapita huku...... He is a very friendly man

.....nasubiri mualiko wa X mas ujue
 
Kweli umefurahi best! Mana sijawah ona your thread! Ila hongera! Umepata rafiki mpya!!
 
Wengine wapo JF na mabosi wao, kama yule secretary wa makamba alivyokamtwa na makamba akimtukana makamba JF ...
 
Ha ha ha ila ujue huwezi kujificha siku zote kama mtu atadhamiria kukupata,tena wala haitaji kuwa hacker.

Cha maana ni play ur game safe n sound here,kwani huwa kuna wakati wote huwa tunajisahau na kuanza kureveal some hints of our true identities.
 
Back
Top Bottom