Siku ya leo imekuwa moja ya siku njema kwangu. Nikiwa katika shughuli zangu za kikazi nlifika katika ofisi moja kuonana na Mkurugenzi wa kampun flan. Nikiwa nimekaa Sehemu ya wageni nliamua kuchukua simu yangu kuingia jamiiforums kwa ajili ya kuweza kusoma na ku comment mambo mawili matatu. Pembeni yangu alikuwepo kijana mmoja nadhifu pia ametulia. Kumbe wakati naendelea kupost JF naye allikuwa akipepesa pepesa macho na ikatokea yakaja kutua kwenye screen yangu. Kijana uzalendo ukamshinda na kaamua kunisamilia “Habari za saa hizi Bro” nlimjibu kwa utulivu. Akanambia “ Samahani naweza kuuliza? “ nikamruhusu aulize.
“wewe ndo gudume?” nlishtuka kidogo kwa kuwa hakukuwa na mtu yeyote anayefaham kuwa mimi ni gudume si ndugu si rafiki. Nikamuuliza kwani vipi? Akajibu “kuna bro mmoja jamiiforums anajiita gudume nliona kama unacomment kwa kutumia ID yake” nikamjibu mimi ndiye. Tuliamka na kukumbatiana kama vile ni marafiki wa muda mrefu waliopotezana na leo wamekutana. Kwa furaha kabisa.
Nlimaliza mambo yangu na kurudi nikamkuta akiwa pale kwenye sofa nikamwomba kama hatojali na ana muda twende wote tukapate lunch.inaonekana naye alikuwa amemaliza lililomleta hakufanya hiyana. Pamoja tukaenda kupata lunch tukipiga stories mbalimbali na visa na mikasa ya jamiiforums.
Hakusita kuelezea mshangao wake.. na kwa kushindwa kuamini kabisa alisema pengine si mimi maana ni mtu tofauti sana na wa JF (alikuwa na bahati kunikuta sober sijavuta mabhangi yangu na kunywa gongo ya mchanganyiko wa Petrol,JIK,Maji ya Battery, Hydrolic,Viroba na sabuni ya OMO) Na kunitaka nimkumbushe visa na mikasa miwili mitatu.tuliongea na kucheka sana. Kiuhalisia hata yeye alikuwa anaonekana ni kijana mstaarabu na si mwenye matusi kama anavyoonekana humu JF. Tukaishia kupeana namba za simu na tukaagana kwa Amani na upendo.
Wadau tuishi kwa Amani na Upendo. Tunayokutana nayo huku yaishie huku huku tu. Tunapokutana nje tuwe watu wenye Amani ,furaha na upendo.tusibebe chuki au hasira za humu ndani na kuhamishia katika maisha halisi.
Nmefurah sana kwa tukio hilo na naomba tuzidi kushirikiana