Uso kwa Uso(Nikiwa Sober) na Mwanajamiiforums mwenzangu ambaye huwa ni Mpinzani wangu sana humu ndani

Uso kwa Uso(Nikiwa Sober) na Mwanajamiiforums mwenzangu ambaye huwa ni Mpinzani wangu sana humu ndani

Siku ya leo imekuwa moja ya siku njema kwangu. Nikiwa katika shughuli zangu za kikazi nlifika katika ofisi moja kuonana na Mkurugenzi wa kampun flan. Nikiwa nimekaa Sehemu ya wageni nliamua kuchukua simu yangu kuingia jamiiforums kwa ajili ya kuweza kusoma na ku comment mambo mawili matatu. Pembeni yangu alikuwepo kijana mmoja nadhifu pia ametulia. Kumbe wakati naendelea kupost JF naye allikuwa akipepesa pepesa macho na ikatokea yakaja kutua kwenye screen yangu. Kijana uzalendo ukamshinda na kaamua kunisamilia “Habari za saa hizi Bro” nlimjibu kwa utulivu. Akanambia “ Samahani naweza kuuliza? “ nikamruhusu aulize.

“wewe ndo gudume?” nlishtuka kidogo kwa kuwa hakukuwa na mtu yeyote anayefaham kuwa mimi ni gudume si ndugu si rafiki. Nikamuuliza kwani vipi? Akajibu “kuna bro mmoja jamiiforums anajiita gudume nliona kama unacomment kwa kutumia ID yake” nikamjibu mimi ndiye. Tuliamka na kukumbatiana kama vile ni marafiki wa muda mrefu waliopotezana na leo wamekutana. Kwa furaha kabisa.

Nlimaliza mambo yangu na kurudi nikamkuta akiwa pale kwenye sofa nikamwomba kama hatojali na ana muda twende wote tukapate lunch.inaonekana naye alikuwa amemaliza lililomleta hakufanya hiyana. Pamoja tukaenda kupata lunch tukipiga stories mbalimbali na visa na mikasa ya jamiiforums.

Hakusita kuelezea mshangao wake.. na kwa kushindwa kuamini kabisa alisema pengine si mimi maana ni mtu tofauti sana na wa JF (alikuwa na bahati kunikuta sober sijavuta mabhangi yangu na kunywa gongo ya mchanganyiko wa Petrol,JIK,Maji ya Battery, Hydrolic,Viroba na sabuni ya OMO) Na kunitaka nimkumbushe visa na mikasa miwili mitatu.tuliongea na kucheka sana. Kiuhalisia hata yeye alikuwa anaonekana ni kijana mstaarabu na si mwenye matusi kama anavyoonekana humu JF. Tukaishia kupeana namba za simu na tukaagana kwa Amani na upendo.

Wadau tuishi kwa Amani na Upendo. Tunayokutana nayo huku yaishie huku huku tu. Tunapokutana nje tuwe watu wenye Amani ,furaha na upendo.tusibebe chuki au hasira za humu ndani na kuhamishia katika maisha halisi.



Nmefurah sana kwa tukio hilo na naomba tuzidi kushirikiana
Deo kisandu nini ...???au kuna mwingine..
 
Hata mimi jumanne nilikutana na dada anaandika msg nikaisoma na alipoipost nikaona na mada aliyokuwa anaichangia,nikaangalia muda aliopost na mimi nikaitafuta nikagundua ni yeye kwakuwa nilisoma alichoandika.
Wewe dada ulyekuwa Mzumbe University upanga,rangi ya chocolate,skirt fupi nyeusi inavifungo juupaka chini kwa nyuma,tup ya brown na vidot vyekundu.
Nilikupiga na picha wakati unachangia kwa sijui "DJ.NYUNDO"sijui Dj nani?.
Jitokeze au naweka picha.
 
Duh gongo ya mchanganyiko gani? Petrol, hydraulic hizi za magari au?
 
yani sikuiyo lazma patachimbika
b49bb7c2d990cdae7cb0eb5795891597.jpg
Hii picha alirusha Tyta zamani nilicheka sana
 
  • Thanks
Reactions: ywf
Ha ha mimi siwezi kukumbatiana na akina cocochanel
 
Ata pilau ikapikwa VIP ila ukisahau chumvi tu habar inakua nyingn,

Bhc ndo baadhi ya watu jf ,bro uko vzr San kweny sekta ii
 
Hata mimi jumanne nilikutana na dada anaandika msg nikaisoma na alipoipost nikaona na mada aliyokuwa anaichangia,nikaangalia muda aliopost na mimi nikaitafuta nikagundua ni yeye kwakuwa nilisoma alichoandika.
Wewe dada ulyekuwa Mzumbe University upanga,rangi ya chocolate,skirt fupi nyeusi inavifungo juupaka chini kwa nyuma,tup ya brown na vidot vyekundu.
Nilikupiga na picha wakati unachangia kwa sijui "DJ.NYUNDO"sijui Dj nani?.
Jitokeze au naweka picha.

Hahahah.. duh hili biti sio la kawaida
 
Hahaaaa. Gudume ukija leo hivi basi kesho unakuja vile.

Nakumbuka mwaka juzi nilishawahi kaa siti moja kwenye daladala na kijana mmoja ila baada ya kumuona anaperuzi jf nikajikuta natamani hata niongee naye ila nikashindwa halafu shida iliyokuja sina tabia ya kupiga chabo simu za watu maana ningeona hadi id yake.
Ungepiga tu chabo dada yangu
 
me mzima. nipo napambana na hali yangu.
nilikuwa kwenye forex kama hujajiunga karibu sana sitaki nikuache nyuma pacha
 
me mzima. nipo napambana na hali yangu.
nilikuwa kwenye forex kama hujajiunga karibu sana sitaki nikuache nyuma pacha
Sawa pacha itabidi nikutafute.

Uwe na jumapili njema pacha.
 
Back
Top Bottom