Usomi wa Slaa una maswali kuliko majibu! Doctarate yake ni ya Kupewa - Kigwangala

pamoja na kuwa kingwangala hana moral authority ya kuhoji elimu dr slaa ngoja tumjibu kw faida ya wengi.
mosi, suala siyo phd ya kupewa au kusomea - suala ni mchango wa mhusika kwa taifa. Marehemu chachage aliwahi sema uprofesa au phd bila mchango wa maana kwa taifa ni sawa na sifuri. Slaa haheshimiki siyo kwa sababu ya phd yake bali mchango wake.
pili, dunian kote, japo kuwa mimi si mkatoliki lakini elimu ya wakatoliki na elimu zinazotolewa n a vyuo vingine vya kawaida ni sawa. Mfumo wao unaaminika kuwa wana elimu bora iwe seminary au chuo kikuu. Hilo nalo lielweke vizuri.

tatu, hoja ya kingwagala imeelemea sana kwenye muda. Muda si hoja. Wapo watu wengi mimi ninawafahamu wamemaliza phd ndani ya miaka miwili ktk vyuo vikubwa duniani. Nakupa mfano moja tu, yupo dr charles ( nimesahau jina la pili) alimaliza phd ndani ya miaka 2 hapo udsm, kutokana policy ya udsm akaambiwa asubiri kwa kuwa amemaliza phd kabla ya muda. Sasa kama dr slaa anazo kichwani, na chuo alichosomea hakina tatizo na muda huo, tatizo liko wapi? Mwa maelezo zadi dr charles anafanya kazi na dfid taasisi inayoshughulikia misaada ya uingeraza hapa tanzania.
mimi nadhani kingwangala angejibu kwanza utata wa jina lake na hatima ya magamba ya ccm kabla ya kuja na hoja isiyo na mashiko.
 
jAMAA NAONA KAMALIZA ALIYOWAAHIDI WANANCHI WAKE SASA ANAINGILIA ELIMU ZA WATU! NA HUYU NI MBUNGE ANAYETARAJIA KUTIMIZA AHADI ZAKE! NAKIHAHAKISHIA MKUU HUWEZI TIMIZA LOLOTW JIMBONI KWAKO WEWE.
 
Watu wote wanaong'ang'ania paper credentials wanakosa kuelewa maana halisi ya usomi.

By his work, man shall be known. Tujadili Slaa kafanya nini, sio ana paper credentials gani na kazipata wapi.

Nipe mtu mwenye credentials ndogo lakini aliyefanya makubwa anytime over mtu mwenye credentials kubwa lakini anafanya madogo.

Hii worshipping ya paper credentials actually ina expose ulimbukeni. Elimu ya kweli haipimwi kwa karatasi jamani.
 
pole my school mate Hamisi Andrew from Kigoma sec school, kwanza hongera kwa kufikia elimu yako ya Dr ila napenda kukueleza kijana una dharau sana huna mwisho mzuri katika siasa, usishangae ukawa katika huo ubunge kwa kipindi kimoja kama L. Masha.
 

Vyema sana, tujadili kafanya nini:

1) Kafanya nini mpaka kufukuzwa upadri?

2) Kafanya nini mpaka kuenguliwa ccm katika kura za maoni?

3) Kafanya nini mpaka kaoa hali yeye ni padri wa kikatoliki na kanisa hilo haliruhusu mapadri waoe?

4) Kafanya nini mpaka kashitakiwa kuwa anatembea na mke wa mtu na ilhali ana mke mwingine?

5) Kafanya nini mpaka katelekeza mke wa awali wakati kanisa haliruhusu?
 
hahahaha kiboriti hicho. Huyu kingwangala ndo alikuwa anaongoza migomo pale MUCHAS miaka ile kumbe alikuwa anaipenda CCM. Ha ha cheti cha nnini sema chichwa... Aaash bichwa maji kubwa jinga. Anapingana na mgodi wa resolute nzega kafukuzwa kama mbwa na mzungu. What a **** is he. Ndo wanalala bungeni.
 
ukicheka na nyani utavuna mabua,kigwangala aliyebebwa juzi leo nae anaongea! Kweli hii ni jamii ya kambale hata ukizaliwa leo tayari unasharubu!!!


You are so much deprived of logic and arguments that I pity you. Kwani nisingekuwa Mbunge kuna mtu angenizuia kutoa maoni yangu?
Nenda darasani ukasome haki za binadamu, flasafa na mantiki vitakusaidia kidogo!
 
pole my school mate Hamisi Andrew from Kigoma sec school, kwanza hongera kwa kufikia elimu yako ya Dr ila napenda kukueleza kijana una dharau sana huna mwisho mzuri katika siasa, usishangae ukawa katika huo ubunge kwa kipindi kimoja kama L. Masha.


Mate, kurudia Ubunge na hata kupumua ni majaliwa ya Mwenyezi Mungu, siyo maamuzi au utashi wangu!
 
Nayaheshimu mawazo ya H.K japo yanaibua maswali mengi ambayo bnafsi nayaona

ila kwa heshima yako ya ubinadamu uliyonayo kama yangu mbeba zege(kwa maana mwanadamu awaye ana heshima yake),kwa niaba ya wengi,naomba ukanushe/ukiri madai yaliyopo dhidi ya umilikaji/utumiaji wa jina la kuadopt,ndo hilo ndugu!
 


Kada wa CHADEMA, Ndg. Mikael Aweda,

Naomba nikujuve kuwa sibishani sana kuhusu uwezo wake kama kiongozi bali nahoji uhalali wa yeye kugombea URais ilhali elimu yake ina mashaka makubwa, na hivyo watanzania wana haki ya kuhoji uhalali wa elimu yake maana ni kigezo cha kuwa mgombea wa nafasi hiyo ya ajira kubwa kuliko zote nchini. Jinsi ilivyo kuna Utata mkubwa. Na wachunguzi pia nawataka wahakiki kama kweli alichokisoma chuo kikuu cha Pontifical Urbaniana University ni J.C.D (Juris Canonici Doctor) au ni kitu kingine tu anachokijua vizuri yeye - fellowship or something of that sort, na pia aliingia kwenye chuo hiki kwa sifa zipi? Pengine TCU wakague vyeti vyake na uhalali wa digrii yake hiyo. Apparently, he happens to have only one degree - a J.C.D, which is a tertiaty level degree! Kabla ya hii angetakiwa awe na Licentiate degree, na hii huwezi ipata kama hauna Masters na Bachelor. How come Slaa would have a tertiary degree (a J.C.D) without the requisite qualifications - the Bachelor as well as a Magister, kama inavyosomeka website ya chuo hicho? Labda kama yeye alipewa msamaha maalum!



1. Kwanza ni kwenye Entry Qualifications zake kwenye masomo ya udaktari - Bio yake inaonesha hana digrii hata moja zaidi ya ya hiyo J.C.D!?

2. Muda aliosoma masomo ya Udaktari na yale ya Stashahada za juu vimekanganyika humo humo

Bio yake inasema, kuwa Slaa baada ya kumaliza Diploma kule Makerere alienda PhD kule Pontifical Urbaniana University kusoma JCD ya Canon Law, hii ilikuwa mwaka 1979 na alimaliza 1981; Pia alisoma Advanced Diploma Mbili Tofauti na katika nchi 2 tofauti katika muda huo huo, kama inavyoonekana hapa chini; alisomaje mwenzetu huyu? Kozi tatu tofauti katika kipindi kile kile!

1979 - 1981> Juris Canonici Doctor (JCD) The Pontifical Urbaniana University
1980-1980 ADV.Diploma-Socio-Political Studies,Koln,Germany(KAF) Advance diploma
gani ya kusoma Mwaka Mmoja?

1981-1981 St.Thomas Aquinas University,Rome,AD.Diploma Rural Development
Advanced Diploma gani hii nayo tena?

1985-1985 London COR.College, Principles and Practice of Management Certificate.

>>>>Doctor of Canon Law (Latin: Juris Canonici Doctor; J.C.D.) is the doctoral-level terminal degree in the studies of canon law of the Roman Catholic Church.


Sasa kada wa CHADEMA, hebu tufafanulie hili hapa kidogo. Ni zito hili na wafukuaji wa mambo watalifanyia kazi, kama hamkujipanga vizuri basi mnalo hili!

Best regards,
HK.
 

Angalia hapo penye nyekundu. Ni mwanzo tu wa kiingereza cha mtu mwenye Masters degree in Public Health (MUHAS)

Hamis clean your bad history of using names that are not yours. Secondly, you were good in peeping during exams from CPL to MPL, and MD3 Lecture theatres, are you proud of that bad character?
 

Dah! Ina maana CCM kuna mambumbu kiasi cha kutoliona hili wakati Dr Slaa alipogombea urais mwaka jana? How come you did not raise this issue during the last year election? Au alikua hatishi kama anavyotisha sasa? Pia naomba ufafanuzi wa U-Dr. wako. Unapenda kujiita Dr. Do you mean una Ph.D au tuu ni fani yako ya udaktari? Naomba unifahamishe b'se personally sijaelewa kama una Ph.D or wewe ni daktari wa hosipitali.

Unahoji uhalali wa Dr. Slaa kugombea urais wakati elimu yake ina mashaka makubwa. Kwani kugombea urais unatakiwa uwe na elimu kiasi gani? Ibara ya 39(1) ya Katiba inasema kuwa mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Sheria ya Uraia.
(b) ametimiza umri wa miaka arobaini;
(c) ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;
(d) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi,
(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katika Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.

Mkuu nifafanulie hapo unless Katiba ibadilishwe, Dr. Slaa ha-meet hizo requirements?

Mwisho, miezi mchache ijayo utatimiza mwaka mmoja tokea uwe mbunge. Nafikiri cha muhimu sana ni wewe na timu yako kukaa chini na kutakafari kwa makini mambo ambayo tayari umeshawafanyia wapiga kura wako in the last year and what is left to be done in the next four years. Nafikiri hilo ndilo la muhumu zaidi mkuu wangu. I am sure you must have a yearly based pilot scheme on what you want to achieve jimboni kwako in five years. By the way kuna kupindi ulikuwa unawaalika watu jimboni kwako kuandamana kupinga mgodi kama sijakosea. Tufafanulie mkuu kama maandamano yalifanyika and what was the results.

Angalia usije ukawa kama Donald Trump alivyokuwa anamkandia Obama kuwa sio Mmarekani only to be shown the birth certificate na akaamua kabisa kuacha hata kugombea Urais. As Obama said: "We do not have time for this kind of silliness. We've got better stuff to do. I have better stuff to do. We've got big problems to solve, and I'm confident we can solve them, but we're going to have to focus on them - not on this."
 
Mhhh hiawa kina Kingwala ndo CCM itayorithi CCM magamba . Mbona kazi ipo ?
 
Slaa bonge la bomu! :hatari: :hatari:

Mtu kama wewe unayediriki kutomheshimu mwenzio hasa wa kiwango kama cha Slaa na kumwita Bomu una utindio na malezi ya kutia shaka ya wazazi wako. Kwa kweli mabomu ni nyinyi na makuadi na ukuadi wenyu. Nyinyi msimsikilize; lakini mnahaha kumfanyia kila hila, hamajajibu hoja za ufisadi za mwembe chai acha za hivi mkaribuni. Hamjajibu kushindwa kwa serikali yenu ya kishikaji kuhusu maisha mufilisi ya watanzania na ahadi hewa za kila uchaguzi huku maisha yakidorora afadhali ya jana.

Mwaka 2010 mmechakachua matokeo ambayo kwa upuuzi wenu mlitarajia aanzishe vurugu hakuanzisha. Mwezi wa pili humu kwenye forum mmeanza kampaign ya kipuuzi kupindisha discussion ili tusizungumzie mweleka wa CCM (na wenu). Mbona wenye elimu miaka hamssini hakieleweki ni afadhali 1960.

Ebu kama mnaweza mkaitafute (mkasomee hiyo elimu) halafu msimame hadharani mseme upuuzi wenu. Kwa jinsi majina na hoja zenu zilivyo zakipuuzi inatia shaka kama hata kwenye hayo madrasa mliambulia kitu na watawaloa wenu akina JK, RA.

KAMA NYINYI MNAMUONA DOKTA SLAA SI KITU SI CHO CHOTE TUAMBIENI LENGO LENU NINI HATA BAADA YA KUCHEZEA FURSA YA MIAKA 50? KWETU WENGINE TUNAHESHIMU KWA KAULI ZAKE BILA KUJALI ELIMU YAKE. NA HII INATHIBITIKA KWA UPUUZI WENU WA KUMZUNGUMZIA YEYE NA KUSHINDWA KWENU KUTOA CHANGAMOTO ZO ZOTE ZA HOJA ZAKE ZIZAZOTUGUSA.

Upuuzi wa kulinganisha DR Slaa na akina Zito na akiana Mnyika Tundu Lissu ni mbinu iliyopitwa na wakati, ilitumika na akina Hitler wako wapi sasa? Zungumzieni mstakabali wa viongozi wenu huko Michuzi blog hakuna atakaewafuata huko.
 

wote wawili, slaa na ******, waweke shahada zao pembeni, waulizwe maswali rahisi tu yanayohusu uongozi wa kitaifa kama urais, kisha tutaona huyu mwenye digrii ya mfumo wa kikoloni uliofuata mtiririko kutoka madrasa hadi phd ya kupewa (japo british system haina madrasa) na huyu mwenye shada ya kikatoliki, tuone nani anaweza kujenga hoja zilizopevuka, kisha ubishi utakoma.
 
Khaa...yani JF watu wanapenda vibaya..sijapata kuona watu wabishi kama humu JF, yani humu unaweza ukaleta maiti na watu wakabisha kama amekufa! Mi nadhani the best way mwenye fact atujuze Dr Slaa kasoma chuo gani degree ya kwanza na ya pili
 
Mimi nasubiri Movie ya NZEGA 2015,
Starring:Hussein Bashe.
Co.Starring😀r. Hamisi Kigwangalla, MD, MPH, MBA.
Mama watoto...Popcorn zangu zipo wapi???
 
ndugu wana jf napenda leo kujua mambo matatu kuhusu daktari wilbroard peter slaa, 1. Degree yake ya kwan za na pili alichukulia wapi? 2. phd yake aliipatia wapi? 3. Na Taaluma yake ni ipi?. naomba majibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…